Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Athumani Almas Maige

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tabora Kaskazini

Primary Question

MHE. ALMAS A. MAIGE aliuliza:- Makao Makuu ya Wilaya ya Uyui yapo Isikizya eneo ambalo halina miundombinu, nyumba za kuishi na huduma rafiki kwa wafanyakazi. Shirika la Nyumba la Taifa limejenga nyumba Isikizya na lilipendekeza kuuza nyumba hizo kwa Halmashauri ya Uyui na kumaliza malipo ndani ya miaka mitatu lakini Halmashauri haina uwezo wa kumaliza malipo ndani ya miaka mitatu. Hivyo wafanyakazi wa Halmashauri wanaendelea kuishi katika nyumba za kupanga Mjini Tabora:- (a) Je, Serikali haioni umuhimu wa kuchangia ununuzi wa Nyumba za Shirika la Nyumba (NHC) ili wafanyakazi wa Halmashauri ya Uyui wahamie Isikizya? (b) Shirika la Nyumba ni wadau wa maendeleo ya makazi na kwa kuwa Serikali ina nia ya kusaidia uanzishwaji wa Makao Makuu ya Wilaya ya Uyui, je, kwa nini Serikali isishawishi Shirika la Nyumba kuongeza muda wa kuuza nyumba zake kutoka miaka mitatu hadi kumi ili kuwezesha Halmashauri kulipa polepole?

Supplementary Question 1

MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kuniruhusu niulize maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa uwezo wa kifedha wa Halmashauri ya Tabora ni mdogo sana na haiwezi kununua nyumba hizo zote kwa ajili ya mahitaji ya wafanyakazi wake. Je, Serikali inaweza kuidhamini Halmashauri ya Uyui ili iweze kukopa kwa muda mrefu kutoka Shirika la Nyumba?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa Halmashauri ya Uyui ni mpya bado na ina changamoto nyingi sana, je, Serikali haioni umuhimu wa kuibeba Halmashauri hii ili iweze kutatua matatizo yake au changamoto ambazo zinaikabili na hasa tatizo hili la nyumba?

Name

Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza Shirika la Nyumba limejenga pale nyumba za kutosha takribani nyumba 49 kama sikosei na katika bajeti ya mwaka huu wameweza kutoa gharama za ujenzi wa nyumba tatu. Suala la kuidhamini, kwa sababu Serikali ikidhamini lazima kuwe na utaratibu wa kurejesha na Mheshimiwa Mbunge alifika ofisini kwangu na timu yake na kwa analysis ya mapato yao ya ndani hata kama wakikopa zile nyumba watahitaji siyo miaka mitatu takribani miaka 10 ili kurejesha mkopo huo, kwa hiyo, hili ni suala la negotiation kati ya Halmashauri na Shirika la nyumba.
Mheshimiwa Naibu Spika, Shirika la Nyumba lilikuwa linasema kwamba, ni lazima iwe ndani ya miaka mitatu lakini ukiangalia uwezo wa Halmashauri ya Uyui kulipa katika miaka mitatu haiwezekani unless otherwise wakubaliane kulipa ndani ya miaka kumi. Kama wakikubaliana ndani ya miaka kumi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI haitosita kuangalia jinsi gani itafanya ili watumishi wale waweze kupata nyumba. Hata hivyo, lazima Halmashauri hii iangalie jinsi gani itaweza kulipa lakini ndani ya miaka mitatu kwa Uyui hawawezi kulipa lile deni.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala zima la kuibeba Halmashauri hii, naomba niseme wazi, jukumu letu kubwa ni kuhakikisha Halmashauri zote zinafanya kazi vizuri. Japo changamoto ya bajeti ni kubwa lakini tunaendelea na harakati mbalimbali za kukamilisha majengo yaliyokuwepo pale Uyui ili Halmashauri mpya ya Uyui ifike muda sasa isimame vizuri, watumishi wote wapate mazingira rafiki ya kufanya kazi na wananchi wapate huduma.

Name

Augustino Manyanda Masele

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbogwe

Primary Question

MHE. ALMAS A. MAIGE aliuliza:- Makao Makuu ya Wilaya ya Uyui yapo Isikizya eneo ambalo halina miundombinu, nyumba za kuishi na huduma rafiki kwa wafanyakazi. Shirika la Nyumba la Taifa limejenga nyumba Isikizya na lilipendekeza kuuza nyumba hizo kwa Halmashauri ya Uyui na kumaliza malipo ndani ya miaka mitatu lakini Halmashauri haina uwezo wa kumaliza malipo ndani ya miaka mitatu. Hivyo wafanyakazi wa Halmashauri wanaendelea kuishi katika nyumba za kupanga Mjini Tabora:- (a) Je, Serikali haioni umuhimu wa kuchangia ununuzi wa Nyumba za Shirika la Nyumba (NHC) ili wafanyakazi wa Halmashauri ya Uyui wahamie Isikizya? (b) Shirika la Nyumba ni wadau wa maendeleo ya makazi na kwa kuwa Serikali ina nia ya kusaidia uanzishwaji wa Makao Makuu ya Wilaya ya Uyui, je, kwa nini Serikali isishawishi Shirika la Nyumba kuongeza muda wa kuuza nyumba zake kutoka miaka mitatu hadi kumi ili kuwezesha Halmashauri kulipa polepole?

Supplementary Question 2

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili na mimi niweze kuuliza swali moja dogo la nyongeza kwa Mheshimiwa Naibu Waziri.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa matatizo ya nyumba za watumishi katika Makao Makuu ya Wilaya ya Uyui yanafanana kabisa na yale matatizo ya watumishi wa Wilaya ya Mbogwe na tayari Serikali imeshatoa shilingi milioni 45 kwa ajili ya kujenga nyumba za watumishi lakini nyumba hizo mpaka sasa hivi hazijakamilika. Je, Serikali iko tayari sasa kuongezea pesa ili nyumba za watumishi hao ziweze kukamilika?

Name

Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, katika suala la Mbogwe alilolisema, nadhani wiki iliyopita nilikuwa natoa tathmini ya Halmashauri mbalimbali mpya zilizopatiwa mgao wa shilingi bilioni mbili, milioni mia moja na arobaini kila moja, zingine zilipatiwa kati ya shilingi milioni mia tano mpaka shilingi milioni mia nane na hamsini na katika mchakato ule Mbogwe ipo.
Mheshimiwa Naibu Spika, jukumu letu kubwa ni nini? Kwa sababu bajeti imeshatengwa, jukumu la Serikali katika mwaka huu wa fedha ni kuhakikisha kwamba tunakusanya mapato ya kutosha kama tunavyofanya sasa ili mradi bajeti tulizozitenga tuweze kuzielekeza maeneo husika ili maeneo hayo ujenzi uweze kufanyika na likiwemo eneo lake la Mbogwe. Kwa hiyo, eneo lake la Mbogwe tumelishalizungumza katika bajeti yetu ya mwaka huu wa fedha.

Name

Martha Moses Mlata

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ALMAS A. MAIGE aliuliza:- Makao Makuu ya Wilaya ya Uyui yapo Isikizya eneo ambalo halina miundombinu, nyumba za kuishi na huduma rafiki kwa wafanyakazi. Shirika la Nyumba la Taifa limejenga nyumba Isikizya na lilipendekeza kuuza nyumba hizo kwa Halmashauri ya Uyui na kumaliza malipo ndani ya miaka mitatu lakini Halmashauri haina uwezo wa kumaliza malipo ndani ya miaka mitatu. Hivyo wafanyakazi wa Halmashauri wanaendelea kuishi katika nyumba za kupanga Mjini Tabora:- (a) Je, Serikali haioni umuhimu wa kuchangia ununuzi wa Nyumba za Shirika la Nyumba (NHC) ili wafanyakazi wa Halmashauri ya Uyui wahamie Isikizya? (b) Shirika la Nyumba ni wadau wa maendeleo ya makazi na kwa kuwa Serikali ina nia ya kusaidia uanzishwaji wa Makao Makuu ya Wilaya ya Uyui, je, kwa nini Serikali isishawishi Shirika la Nyumba kuongeza muda wa kuuza nyumba zake kutoka miaka mitatu hadi kumi ili kuwezesha Halmashauri kulipa polepole?

Supplementary Question 3

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Naibu Spika ahsante. Wilaya mpya ya Mkalama pamoja na kwamba ilitengewa fedha kwa ajili ya kujenga Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya hiyo, fedha hizo zimeonekana hazitoshi kwa sababu nyingi zimeenda kulipa tu fidia na hivyo kushindwa kuendelea kujenga ofisi hiyo. Naomba Mheshimiwa Naibu Waziri atuambie wako tayari sasa kuiongezea fedha Halmashauri hiyo ili iondokane na adha ya kupanga majengo?

Name

Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya mpya ya Mkalama katika orodha yangu ya zile Halmashauri nilizozizungumza ni miongoni mwa Halmashauri ambayo imo kwenye orodha. Jukumu letu sisi Wabunge kwa umoja wetu tuhakikishe bajeti ya Serikali inapita na tutaiomba sasa Wizara ya Fedha bajeti tuliyoipanga mwaka huu iweze kupatikana ili Mkalama kama tulivyoipangia bajeti katika mwaka huu iweze kupata fedha, ujenzi uweze kuendelea ile Halmashauri iweze kusimama vizuri. Kwa hiyo, Mkalama ni miongoni mwa Wilaya ambazo tunaenda kuzifanyia kazi katika mwaka huu wa fedha.

Whoops, looks like something went wrong.