Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Daimu Iddi Mpakate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kusini

Primary Question

MHE. DAIMU I. MPAKATE Aliuliza:- Jimbo la Tunduru Kusini limepakana na nchi ya Msumbiji kwa upande wa Kusini. Je, ni lini Serikali itafungua Ofisi za Mamlaka ya Mapato (TRA) Lukumbule?

Supplementary Question 1

MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini Lukumbule ni lango kubwa ambalo wafanyabiashara wanapita kupeleka bidhaa zao Msumbiji na wale wanaotoka Msumbiji wanapita Lukumbule kuleta Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Serikali imekubali kufanya tathmini na kwa kuwa wananchi wa Tanzania wanaopeleka bidhaa Msumbiji mara nyingi hunyang’anywa mali zao kwa kukosa documents za kusafirisha mizigo yao kwenda Msumbiji.

Je, Serikali haioni haja ya haraka kufanya tathmini hiyo ili kuhakikisha wananchi wetu wa Tanzania wanaoenda Msumbiji hawanyang’anywi mali zao mara kwa mara? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa Jimbo la Tunduru Kusini lina miji mitano mikubwa; Nalasi, Mchoteka, Malumba, Lukumbule pamoja na Misechela ambayo ina wafanyabiashara wengi na miji hiyo iko zaidi ya kilometa 80 kutoka ilipo Ofisi ya TRA Tunduru Mjini.

Je, Serikali haioni haja ya kupeleka agencies katika maeneo hayo ili wafanyabiashara wale waweze kulipa kodi zao wakiwa katika maeneo yao ya biashara? (Makofi)

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeona umuhimu wa ushauri wa Mheshimiwa Mbunge. Kwa hiyo, ushauri tumeupokea na tutaufanyia kazi kwa mujibu wa sheria na miongozo iliyowekwa na pale tutakapopata majibu basi tutamfikishia majibu kwa haraka sana. (Makofi)