Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ndaisaba George Ruhoro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngara

Primary Question

MHE. NDAISABA G. RUHORO Aliuliza:- (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kutengeneza mazingira wezeshi ya kuongeza bei ya zao la kahawa ili wakulima wa zao hili waweze kunufaika kama ambavyo wakulima wa nchi jirani ya Uganda wanavyonufaika? (b) Utaratibu wa ununuzi wa zao la kahawa unapitia Vyama vya Ushirika, hali inayoonekana kutovutia ushindani. Je, Serikali ina mpango gani wa kuwezesha ushiriki wa sekta binafsi ili kuvutia ushindani?

Supplementary Question 1

MHE. NDAISABA G. RUHOYO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Napenda kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri na aliyoyasema yakitekelezeka basi Tanzania ndani ya kipindi cha miaka mitatu itakuwa inaongoza kwa uzalishaji wa kahawa ukiachia Ethiopia, Uganda, Cote d’lvoire pamoja na Kenya.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sasa niulize swali langu la nyongeza.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha miche milioni 20 inayotarajiwa kuzalishwa inawafikia wakulima wa Tanzania wakiwemo wananchi wa Wilaya ya Ngara kwenye Tarafa za Kanazi, Nyamiaga, Rulenge pamoja na Murusagamba?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, mwezi Februari mwaka huu tutagawa katika Mkoa wa Kagera kuanzia tarehe 27 Februari, 2021, tutagawa jumla ya miche 1,000,000 kwa wakulima bure. Kwa hiyo hiyo ni sehemu na malengo tuliyojiwekea ni ugawaji wa jumla ya miche milioni 20.