Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Maida Hamad Abdallah

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MAIDA HAMAD ABDALLAH Aliuliza: - Pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali za kupambana na ugonjwa wa Malaria, bado ugonjwa huo unaendelea kuwaathiri wananchi wakiwemo watoto: - Je, Serikali inaweza kutuambia hatua zilizofikiwa za kutokomeza ugonjwa huo?

Supplementary Question 1

MHE. MAIDA HAMAD ABDALLAH: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ninayo maswali mawili ya nyongeza. Kwanza naipongeza sana Serikali kwa kuweza kuweka mkakati madhubuti…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa uliza swali.

MHE. MAIDA HAMAD ABDALLAH: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; kwa kuwa mapambano dhidi ya malaria nchini Tanzania yalianza toka mwaka 1890; na wengi tunafahamu kwamba suala la malaria linatokana na mbu; kwa vile tunacho kiwanda kinachozalisha dawa ya viuadudu ambayo inamaliza kabisa mazalia ya mbu: Je, Serikali haioni kwamba umefika wakati wa kuzitaka Halmashauri kutenga bajeti katika bajeti zao ili kuweza kununua dawa hizi kila Halmashauri iweze kudhibiti malaria kupitia kila Halmashauri? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa wenzetu toka nje ya nchi wanakithamini sana na kuona umuhimu wa kiwanda hiki na dawa hii inayozalishwa Tanzania: Je, Serikali kupitia Wizara hii inatoa elimu gani kwa wananchi kuhusiana na suala la dawa zinazozalishwa na kiwanda hiki kilichoko Kibaha? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Maida kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza ni namna gani tutakitumia kiwanda ambacho kiko Kibaha kuweza kushirikiana nacho kumaliza tatizo la malaria? Hili tunalichukua. Vile vile ndani ya swali la kwanza ameuliza Halmashauri itafanyaje? Tutaenda kushirikiana na TAMISEMI na hasa kwa sababu kuna tozo ambazo zimekuwa zikitozwa kule Halmashauri zinazotokana na masuala ya afya, fedha hizo zinaweza zikatumika asilimia fulani, vile vile kusaidia kugharamia eneo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili linaonekana linahusu elimu. Nafikiri kwenye strategic ya mwaka 2021 – 2025 kwa kweli tutakwenda kuwekeza kwenye eneo ambalo Mheshimiwa Mbunge amelishauri. Tunachukua ushauri wake na tutaenda kuufanyia kazi kwa nguvu zote kabisa.