Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Primary Question

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA aliuliza:- Baadhi ya minara ya simu ya Vodacom, Airtel, Tigo na Halotel katika Kata za Kipili, Kilumbi, Kiloli, Kitunda, Kisanga, Mole, Kiloleli na Ipole haifanyi kazi vizuri kwani mtandao katika Kata hizo ni mdogo sana na hivyo wananchi hawapati huduma nzuri ya mawasiliano licha ya uwepo wa minara hiyo. Aidha, katika Kata za Nyahua, Igigwa na Ngonjwa hakuna kabisa mawasiliano ya simu:- (a) Je, ni lini Serikali itawapatia mawasiliano ya uhakika wakazi wa Sikonge wanaoishi kwenye Kata zenye minara ya simu lakini isiyokamata mtando vizuri? (b) Je, Serikali itawapatia lini mawasiliano ya simu wananchi wa Sikonge ambao wanaishi kwenye Kata ambazo hazina kabisa minara ya mawasiliano ya simu?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa Serikali kujibu swali langu Na. 22 vizuri. Nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; mnara wa Airtel uliojengwa kwenye Kata ya Kipili, Kitongoji cha Madoletisa ambao haujawashwa kwa miaka miwili sasa na mnara wa Vodacom kwenye Kata ya Kilumbi ambao nao haujawashwa kwa miaka miwili hadi sasa: Je, ni lini itawashwa ili wananchi waanze kufaidika na huduma za mawasiliano?

Mheshimiwa Spika, je, Miradi ya Mawasiliano Vijijini iliyomo kwenye Mpango wa Maendeleo wa 2019/2020 ambayo orodha yake ipo kwenye randama pia kwenye kijitabu cha taarifa ya Wizara ya Julai 2019, itatekelezwa lini?

Name

Eng. Isack Aloyce Kamwelwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Answer

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Spika, mnara uliojengwa katika Kitongoji cha Madoletisa ni kweli ni wa Kampuni ya Simu ya Airtel. Mnara huu ulijengwa kama mnara wa kupeleka mawimbi ya simu kwenda katika minara mingine ya mbali (Transmission Site). Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) uliliona tatizo la mnara huo ambapo unatumika kama transmission site bila kutoa huduma kwa wananchi waliopo Madoletisa na kuiagiza Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel wauwekee vifaa vya radio ili mnara huo pia utumike kutoa huduma za mawasiliano kwa wananchi. Tumewasiliana na Airtel ili wakamilishe kazi ya kuwapelekea wananchi mawasiliano mara moja ndani ya mwezi huu wa Aprili, 2020.

Mheshimiwa Spika, Miradi ya Mawasiliano Vijijini kwenye Vijiji vya Igigwa, Migumbu, Nyahua na Tumbili kutoka Kata ya Igigwa, Vijiji vya Ipole, Makazi, Udongo na Ugunda kutoka Kata ya Ipole, Vijiji vya Kanyamsenga, Kiloleli na Mtakuja katika Kata ya Kaloleli, Vijiji vya Imalampaka na Mibono katika Kata ya Kipanga pamoja na Kijiji cha Kiyombo kutoka Kata ya kipili, havikupata watoa huduma katika zabuni ya mwezi Julai, 2019. Miradi hiyo itatangazwa tena mwezi Juni, 2020.