Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Bernadeta Kasabago Mushashu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BERNADETHA K. MUSHASHU aliuliza:- Mafuriko yanayotokea katika Mji wa Bukoba husababisha uharibifu mkubwa wa chakula, mali, barabara na hata kusababisha vifo kwa watu na mifugo; mafuriko hayo husababishwa na Mto Kanoni kujaa mchanga na takataka:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaondolea kero ya mafuriko kila mwaka ikiwemo kusafisha na kuongeza kina cha Mto Kanoni?

Supplementary Question 1

MHE. BERNADETHA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mto wa Kanoni kwa sasa umejaa sana mchanga na kina kimepungua sana, kwa watu wenyewe itakuwa si kazi rahisi kuondoa mchanga na zitahitajika fedha nyingi sana; pamoja na hatua zilizoainishwa kwenye jibu la swali ambazo ni za muda mrefu:-

Je, ni kwa nini Serikali isiwasaidie sasa hawa watu wanaohangaika na mafuriko kila mwaka kwa kutoa fedha kiasi za kuanza kusafisha mto huu angalau mara moja kwa mwaka?

Name

Mussa Azzan Zungu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ilala

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Spika, awali yote napenda kumshukuru Mheshimiwa Benadetha kwa kufuatilia kwa kina suala hili na kutupatia taarifa za kina kuhusu changamoto hii.

Mheshimiwa Spika, napenda kumhakikiashia Mheshimiwa kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi ni sikivu na inajali wananchi wake. Hivyo, Serikali inalichukulia kwa uzito suala hili na tunawasiliana na mamlaka husika ikiwemo Halmashauri ya Bukoba Mjini kuona namna bora na ya kudumu ya kutatua changamoto ya kujaa mchanga katika Mto Kanoni ili kuondoa kero ya mafuriko ya mara kwa mara.