Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Primary Question

MHE. PAULINE P. GEKUL aliuliza:- Miundombinu mibovu ya barabara zinazoelekea Hifadhini husababisha Watalii kuwa wachache Mathalan; barabara inayotoka Iringa Mjini hadi Hifadhi ya Ruaha kilometa 104 ni ya vumbi na vilevile barabara ya kutoka Babati Mjini hadi Tarangire kilometa 20 ni ya vumbi:- Je, ni lini Serikali itajenga barabara hizo kwa kiwango cha lami ili kuwavutia Watalii wengi zaidi?

Supplementary Question 1

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kunipa nafasi niulize maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Waziri nikushukuru pia kwa majibu ya Serikali ambayo ni mazuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza Mheshimiwa Waziri, Serikali haioni kwamba sasa badala ya barabara hii inayotoka Babati mjini hizi kilomita 20 kuendelea kuwekewa fedha za maintenance, ni vizuri wakatenga fedha za kuweka lami hizo kilomita 20 hadi lango la Tarangire ili watalii wanapofika Babati wasafiri vizuri mpaka hapo Hifadhini kuliko ambavyo sasa ni rough road.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Swali la pili miongoni mwa vitu ambavyo vinachochea utalii wetu ni pamoja na miundombinu mizuri barabara pamoja na viwanja vya ndege uwanja wetu wa Mkoa wa Manyara ambao uko pale Magugu sasa haujawahi kutengewa fedha na watalii wamekuwa wakilazimika sasa watue Arusha na watembee umbali mrefu.

Je, Serikali iko tayari kututengea fedha haraka iwezekanavyo kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mkoa wa Manyara ili watalii waweze kufika mapema hifadhini Tarangire?

Name

Elias John Kwandikwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI MAWASILIANO NA UCHUKUZI (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kuhusu barabara hii ya Babati kwenda Tarangire kwenye lango niseme iko kwenye mipango na sasa kama kinachofanyika ni kuhakikisha kwamba inakuwa vizuri ndiyo maana Bunge lako imetutengea fedha kwa ajili ya kufanya maboresho makubwa ili kuondoa usumbufu kabisa ili wananchi wakati tunafanya harakati za ujenzi watalii waweze kupita bila shida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuhusu ujenzi wa uwanja wa ndege kwanza niipongeze Serikali ya mkoa, kupata eneo hili la Mbuyu wa Mjerumani kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja cha ndege na nimfahamishe tu Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Wabunge na wananchi kwa ujumla ni kwamba Wizara yangu kupitia TIA inaendelea na usanifu ili sasa tuweze kujua namna uwanja utakavyokuwa na gharama zake na hatimaye tuweze kujenga uwanja huu wa ndege. Ahsante sana.