Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jaku Hashim Ayoub

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. JAKU HASHIM AYOUB aliuliza:- Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya mwaka 2014, Kisiwa cha Latham ni mali ya Zanzibar tangu kilipofunguliwa rasmi mwaka 1898. Hata hivyo, zipo taarifa zilizothibitishwa kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu iliiandikia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwaarifu kuwa Kisiwa hicho ni cha Tanzania Bara. (a) Je, ni lini Serikali hizi mbili ambazo ni ndugu wa damu watakaa kutatua kero hii ya muda mrefu? (b) Je, Serikali haioni kuwa umefika muda muafaka kulifanyia kazi suala hilo?

Supplementary Question 1

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba nizungumze kidogo kidogo ili nifahamike nisiende haraka haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina sehemu mbili ambazo ni Tanzania Bara na Tanzania Visiwani. Nilichouliza ni mipaka ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, kisiwa kile kiko sehemu gani, hicho ndicho nilichouliza. Kisiwa kile kiko Zanzibar au Tanzania Bara. Swali langu la kwanza nafikiri limefahamika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, je, ni sababu gani iliyopelekea Tanzania Bara kudai kisiwa kile ni chao na Zanzibar kudai ni chao? Hata hivyo, kuna ushahidi wa kutosha na naomba nikuletee nakala hii na kuweka record ya Bunge hili ni sababu gani iliyopelekea kuvutana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2014 Serikali mbili zilikutana, ya Mapinduzi ya Zanzibar na Tanzania Bara na ikaundwa Kamati ya Wajumbe wawili wazito akiwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na Mwanasheria Mkuu wa Tanzania Bara. Je, ni lini ripoti ile italetwa ili kuondosha fitina hii?

Name

Mussa Ramadhani Sima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu maswali madogo mawili ya Mheshimiwa Jaku kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza Mheshimiwa Jaku majibu niliyoyatoa katika swali lako la msingi yamejitosheleza kuelezea kisiwa hiki kiko wapi. Hata hivyo, nyongeza yake, kwa kuwa tayari unayo taarifa, nadhani ni jambo jema sana tukakutana ili uweze kunikabidhi tuone namna gani tunaweza kulifuatilia jambo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ni kwamba kila jambo lina utaratibu, hata kama Wanasheria wamekutana lakini ni lazima viko vikao maalum, iko Sekretarieti lakini wako Makatibu Wakuu, iko level ya Mawaziri mpaka zije zikutane Kamati zote mbili za SMZ na Jamhuri ya Muungano ili kuweza kuona ni namna gani mambo haya yanaweza kufikiwa muafaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe Mheshimiwa Jaku wala asiwe na wasiwasi. Serikali iko kazini tukutane tuone taarifa aliyonayo ili tuone ni namna gani tunaifanyia kazi. Ahsante.