Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hussein Nassor Amar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyang'hwale

Primary Question

MHE. HUSSEIN N. AMAR aliuliza:- Rais wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, katika ziara yake Wilayani Nyang’hwale tarehe 11 Novemba, 2013 akiongozana na aliyekuwa Waziri wa ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Najaliwa alitoa ahadi kwa wananchi ya kujenga barabara ya kutoka Busisi – Busolwa – Nyijundu – Kharumwa, Bukwimba hadi Nyang’holongo kuelekea Kahama Mjini kwa kiwango cha lami pamoja na kuondoa tatizo la mawasiliano ya simu:- (a) Je, ni lini ahadi hiyo ya viongozi wakuu wa nchi itatekelezwa? (b) Je, ni lini Serikali itatimiza ahadi hizo kwa kujenga minara ya mawasiliano ya simu ili maeneo ya Nyamtukuza, Kanegere, Nyugwa na maeneo mengine yaweze kusikika na kuchochea maendeleo ya nchi?

Supplementary Question 1

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kabla ya maswali kuna marekebisho kidogo katika maandishi aliyoandika hapa Mheshimiwa Naibu Waziri, inasomeka barabara ya Busisi - Busolwa, Nyijundu – Kharumwa - Bukwimbwa – Nyang’holongo siyo Nyang’hongo.

Mheshimiwa Spika, baada ya marekebisho hayo, napenda kumpongeza Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri. Kwa kuwa Serikali inakiri kutekeleza ahadi hizo za viongozi kwa kujengwa barabara ya lami kutoka Kahama hadi Busisi kupitia Kharumwa pindi pesa zitakapopatikana. Swali la kwanza, kwa nini wakati Serikali ikitafuta fedha za kutengeneza hizo kilomita nyingi tusitengewe fedha za kujenga kilomita 3 Makao Makuu ya Wilaya Kharumwa ili kupunguza vumbi kutokana na msongamano mkubwa wa magari uliopo pale?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Naibu Waziri amesema wanaendelea na kupeleka mawasiliano katika kata alizozitaja lakini Kata ya Nyijundu kuna matatizo ya usikivu. Je, Vodacom wako tayari kwenda kufunga mnara huo ili wananchi wa maeneo yale waweze kutuma na kupokea fedha kupitia Mpesa?

Name

Elias John Kwandikwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa
Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Hussein Nassor Amar, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza uniruhusu nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa sababu tumezungumza mambo mengi sana kuhusu uboreshaji wa miundombinu katika Wilaya hii ya Nyang’hwale. Tulifanya discussion na Mheshimiwa Mbunge na anakumbuka nilitoa maelekezo upande wa wenzetu wa TANROADS Mkoa wa Geita kwamba tutazame Makao Makuu ya Mji ya Nyang’hwale. Kama tulivyokubaliana tutaanza na kilometa 2 pamoja na kuboresha mitaro iliyowekwa katika Mji wa Kharumwa, Makao Makuu ya Nyang’hwale. Kwa hiyo, nimtoe hofu tumejipanga kufanya Makao Makuu ya Nyang’hwale kukaa vizuri.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mawasiliano, tunaendelea na hatua ya kuboresha mawasiliano nchi nzima. Nimsihi tu Mheshimiwa Mbunge baadaye tuonane ili tuangalie kwenye orodha maana kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote tutapeleka mawasiliano katika vijiji 521 ambavyo viko kwenye kwenye hatua ya manunuzi inawezekana vijiji vyake vikawepo. Kwa hiyo, tuonane tu, ninayo orodha hapa, nawakaribisha na Waheshimiwa Wabunge wengine ili tuone tumejipangaje kupeleka mawasiliano maeneo ambayo tumejipangia katika awamu hii ya nne. Ahsante sana.

Name

Aysharose Ndogholi Mattembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HUSSEIN N. AMAR aliuliza:- Rais wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, katika ziara yake Wilayani Nyang’hwale tarehe 11 Novemba, 2013 akiongozana na aliyekuwa Waziri wa ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Najaliwa alitoa ahadi kwa wananchi ya kujenga barabara ya kutoka Busisi – Busolwa – Nyijundu – Kharumwa, Bukwimba hadi Nyang’holongo kuelekea Kahama Mjini kwa kiwango cha lami pamoja na kuondoa tatizo la mawasiliano ya simu:- (a) Je, ni lini ahadi hiyo ya viongozi wakuu wa nchi itatekelezwa? (b) Je, ni lini Serikali itatimiza ahadi hizo kwa kujenga minara ya mawasiliano ya simu ili maeneo ya Nyamtukuza, Kanegere, Nyugwa na maeneo mengine yaweze kusikika na kuchochea maendeleo ya nchi?

Supplementary Question 2

MHE. AISHAROSE N. MATEMBE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kuniona. Tatizo la miundombinu lipo pia katika Jimbo la Ikungi Mashariki katika barabara yetu ya Makiyungu - Misughaa. Changamoto hiyo imekuwa kubwa sana wakati wa masika. Je, ni lini Serikali itajenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami ili kuunganisha Mikoa ya Singida na Dodoma na kuharakisha shughuli za maendeleo katika maeneo hayo? Nakushukuru. (Makofi)

Name

Elias John Kwandikwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa
Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Aisharose Matembe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza Mheshimiwa Aisharose Matembe amekuwa mahiri sana kufuatilia barabara mbalimbali. Barabara hii anayoitaja Mheshimiwa Mbunge ni sehemu ya kilomita 461 ya barabara inayotoka Handeni – Kibirashi – Kijungu - Chemba - Singida. Kwa hiyo, nimuombe tu Mheshimiwa Mbunge avute subira kwani katika bajeti ya mwaka huu tumetenga fedha kuanza ujenzi wa barabara hii muhimu. Tukipata fedha eneo hili litapitiwa na mradi wa barabara ya lami inayotoka Handeni – Singida.