Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Primary Question

MHE. RIDHIWANI J. KIKWETE aliuliza:- Katika kikao cha kazi, Mheshimiwa Rais akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega alitoa maelekezo ya kutoondoa Vijiji vilivyomo katika maeneo ya Hifadhi:- (a) Je, tangazo hilo linamaanisha kuwa wameruhusiwa kuendelea na shughuli za kiuchumi katika maeneo yao wanayoishi? (b) Je, ni lini sasa Serikali itashughulikia migogoro ya mipaka baina ya Vijiji hivyo na Hifadhi au kwa tamko lile maana yake Wanavijiji waendelee kama vile hakukuwahi kuwa na migogoro?

Supplementary Question 1

MHE. RIDHIWANI J. KIKWETE: Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza na kumshukuru sana Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya, lakini pia kwa kutuliza joto la wananchi katika maeneo yetu.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa na mambo mawili makubwa ambayo nilikuwa nataka niishauri Serikali. Kwanza, nimwambie Mheshimiwa Waziri, sikusudii kumzungumza au kuwatetea wavamizi wa hifadhi hizo. Ila swali langu linalenga katika hifadhi zilizovamia vijiji vyetu, maana kesi ya watu wa Chalinze ni hifadhi imevamia vijiji.

Mheshimiwa Spika, la pili, nikushukuru na kukupongeza, naona leo umemwalika Bwana Pierre Liquid, ni jambo jema, lakini ushauri wangu naomba kwa Wizara, inapofanya kazi katika kuweka hivyo vigingi na beacons itushirikishe sana sisi wawakilishi wa wananchi ili tuweze kuwapa ushirikiano na kuwakumbusha vizuri ili wasije kuvuruga kabisa zoezi zima.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Name

Constantine John Kanyasu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, kwanza, naomba nipokee pongezi hizo ambazo amempa Mheshimiwa Rais. Ni kweli kwamba hata kabla ya tamko la Mheshimiwa Rais maeneo haya yamekuwa ndani ya migogoro mingine kwa zaidi ya miaka 20; na yapo maeneo ambayo yalikuwa yana GN mbili; eneo lina GN ya uhifadhi lakini pia kuna GN ya kijiji au kata katika eneo la hifadhi. Kwa hiyo, Mheshimiwa Rais alichokifanya ni kulifanya tatizo hili liweze kushughulikiwa.

Mheshimiwa Spika, katika swali lake la kwanza, amesema kwamba hifadhi ndiyo zimevamia maeneo ya vijiji. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kama nilivyojibu katika jibu langu la msingi, baada ya kazi ya Kamati tutakwenda katika maeneo husika yote yenye migogoro na tutashirikisha wawakilishi wa wananchi, wakiwemo Wabunge na Madiwani, kuhakikisha kwamba eneo tutakaloliwekea mipaka halitakuwa na migogoro tena.