Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Primary Question

MHE. HUSSEIN M. BASHE aliuliza:- Wakati wa kampeni za Uchaguzi Jimbo la Nzega Mjini tarehe 14/10/2015, Mheshimiwa Rais aliahidi kuwa majengo yanayotumiwa na mkandarasi wa barabara ya Nzega – Tabora na majengo ya TANROADS yatakabidhiwa kwa Halmashauri ya Mji wa Nzega ili yaweze kutumika kwa ajili ya Chuo cha VETA:- (a) Je, Serikali imefikia hatua gani kutekeleza ahadi hiyo ili majengo hayo yakabidhiwe katika Halmashauri ya Nzega? (b) Je, Serikali ipo tayari kuwaambia wananchi wa Nzega lini chuo hicho kitaanzishwa?

Supplementary Question 1

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nisikitike na samahani kwa kauli nitakayosema, ni aidha Manaibu Waziri wanapokuja kutujibu au Mawaziri hawako serious, wanatuchukulia for granted ama hawafanyi kazi yao ipasavyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, Naibu Waziri anasema majengo ni mali ya mkandarasi hayawezi kurejeshwa Serikalini. Anataka kutuambia mimi na Rais tarehe 14 Oktoba, 2015, tuliwadanganya wananchi wa Nzega tukijua kwamba majengo yale ni mali ya mkandarasi na hakutakuwa na chuo?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, Mji wa Nzega una sekondari inayoitwa Bulunde, majengo yalikuwa ya mkandarasi. Je, Serikali utaratibu ule ule iliyotumia kuyapata majengo yaliyotumika kwa ajili ya sekondari ya Bulunde, inakuwa na ugumu gani leo kuyapata majengo yanayotumiwa na mkandarasi anayejenga barabara ya Nzega - Puge ili kuanzisha Chuo cha VETA.

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, kilichosemwa tarehe hiyo anayoongelea, tarehe ya 14 Oktoba, 2015 ni sahihi na tulichokisema hapa kwenye jibu la msingi ni sahihi, ila tunaongelea vitu viwili tofauti. Tulichokisema hapa ni kwa mujibu wa mkataba na Mheshimiwa Naibu Spika wewe ni Mwanasheria unafahamu. Kama mkataba umesema hivyo na sisi leo tukasema tofauti, tutaiingiza Serikali kwenye hasara.
Mheshimiwa Naibu Spika, kilichosemwa tarehe 14 Oktoba, 2015 na Mheshimiwa Rais akiwa na Mheshimiwa Hussein Bashe kule Nzega nacho bado kilikuwa ni sahihi, mchakato wake ndiyo huo unaoendelea ambao tumeuongelea hapa. Ni kitu ambacho Serikali itakifanya, lakini siyo kwa kulazimisha na kukitoa hadharani.

Name

Dr. Shukuru Jumanne Kawambwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bagamoyo

Primary Question

MHE. HUSSEIN M. BASHE aliuliza:- Wakati wa kampeni za Uchaguzi Jimbo la Nzega Mjini tarehe 14/10/2015, Mheshimiwa Rais aliahidi kuwa majengo yanayotumiwa na mkandarasi wa barabara ya Nzega – Tabora na majengo ya TANROADS yatakabidhiwa kwa Halmashauri ya Mji wa Nzega ili yaweze kutumika kwa ajili ya Chuo cha VETA:- (a) Je, Serikali imefikia hatua gani kutekeleza ahadi hiyo ili majengo hayo yakabidhiwe katika Halmashauri ya Nzega? (b) Je, Serikali ipo tayari kuwaambia wananchi wa Nzega lini chuo hicho kitaanzishwa?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama ilivyokuwa kwa Nzega Mjini, Mheshimiwa Rais wetu alipokuwa kwenye kampeni katika Jimbo la Bagamoyo aliwaahidi wananchi kuikabidhi kambi ya mkandarasi iliyopo Daraja la Makofia kwa wananchi wa Bagamoyo ili waweze kuanzisha shule ya msingi. Naomba kujua kutoka kwa Mheshimiwa Naibu Waziri taratibu zimefikia wapi?

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo nilimjibu Mheshimiwa Bashe, dhamira ya Serikali ya kuhakikisha majengo yanayojengwa na wakandarasi yanatumika baada ya mkandarasi kukamilisha kazi zake katika shughuli zingine za kijamii iko pale pale, lakini utaratibu wa kuyapata hayo majengo ndiyo tunaobishania. Namhakikishia Mheshimiwa Dkt. Kawambwa ombi lake maadam lilifika kwa utaratibu uliotakiwa, tutaendelea kulifanyia kazi kwa utaratibu huu ambao nimemweleza Mheshimiwa Bashe kwa lile eneo la Nzega na tutatumia njia ile ile tuliyotumia kwa shule ile ya Bulunde.