Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI aliuliza:- Chuo cha Mahakama Lushoto (IJA) kinatoa taaluma ya Stashahada za Sheria. (a) Je, ni lini sasa Serikali itaongeza uwezo wa Chuo hicho ili kitoe elimu ya sheria kwa ngazi ya Shahada? (b) Je, ni kwa nini Serikali sasa isione umuhimu wa kukifanya Chuo hicho kiwe Wakala wa Law School ili mafunzo ya uwakili pia yaweze kutolewa chuoni hapo?

Supplementary Question 1

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali ninayo maswali ya nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa amesema lengo la chuo hiki cha mahakama ni kutoa elimu ambayo inasaidia watumishi walioko makazini waweze kuboresha ufanisi na utendaji wao; je, haoni sasa ni muhimu kwa chuo hiki pia kuanzisha kozi maalum kwa watumishi wengine wa Idara ya Mahakama wakiwemo makarani na wakalimani? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa Serikali imeanzisha msaada wa huduma ya msaada wa kisheria na kwa kuwa kule Lushoto nako tuna watoa msaada wa kisheria; je, haoni kwamba ni muhimu chuo hiki kikasaidia watoa msaada wa kisheria katika Halmashauri ya Lushoto kuwajengea uwezo ili waende kuwasaidia wananchi huko vijijini? (Makofi)

Name

Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilosa

Answer

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, moja kuhusu kutoa elimu kwa ngazi ya makarani na watu wa masijala ya mahakama, nakubaliana naye kabisa kwamba wakati umefika na maadam chuo kimeweka kikosi kazi cha kupitia upya mitaala na mafunzo mbalimbali ya kozi mbalimbali katika chuo hicho, nachukua maoni yake na nitawasilisha katika kikosi kazi hicho.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la kutoa elimu kwa paralegal kwa ajili ya msaada wa kisheria pia wazo hilo ni zuri na siyo tu kwa Lushoto, nadhani kwa maeneo yote ya Mikoa ya Kaskazini ambayo yako karibu na Chuo cha Lushoto.