Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Haji Hussein Mponda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Malinyi

Primary Question

MHE. DKT. HADJI H. MPONDA aliuliza:- Mkoa wa Morogoro umechaguliwa kuwa ni Ghala la Chakula la Taifa hususani katika mazao ya mpunga na miwa. Katika kutaekeleza hili Serikali imepanga kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ujenzi wa skimu za umwagiliaji katika Vijiji/Kata za Usangule – Mto Lwasesa, Igawa – Mto Furua, Lupunga – Mto Mwalisi na Kilosa – Mto Mwalisi. • Je, ni lini kazi hiyo ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina itakamilika? • Katika kipindi hiki cha maandalizi ya ujenzi wa mabanio haya ya kilimo cha umwagiliaji, je, Serikali ina utaratibu gani wa usimamizi wa ardhi husika ili kuepuka migogoro ya watumiaji wa mabanio hayo siku za usoni?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. HADJI H. MPONDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, pia ninaishukuru Serikali kwa majibu mazuri ya swali la msingi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mawaziri hao wote wawili wa Wizara hii; Waziri na Naibu wake wamefika eneo hilo. Mara ya mwisho mwezi wa pili Mheshimiwa Naibu Waziri amefika na wana Malinyi tumempa jina la Dogo Janja. Ameona hali halisi pale katika Skimu ya Itete, kwa kuwa imetokana na usanifu wa kina ambao haukuwa mzuri na hata ujenzi ule uliofanyika haukuwa mzuri imesababisha skimu ile inashindwa kufanya kazi kama inavyotakiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, skimu ile haina barabara za kuingia kwenye mashamba, skimu ile wakati wa kiangazi haina maji ya kutosha kumwagilia mashamba yale na Serikali wameadhidi kwamba watafanya marekebisho swali langu la kwanza, ni lini mtafanya marekebisho ambayo mmehaidi kwenye Skimu ya Itete?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, menejimenti ya skimu ile inasimamiwa na injinia ambaye anakaa Malinyi kilometa 50 kutoka pale kwenye skimu mpaka anapoishi yule injinia; tuliomba ombi maalum apatiwe usafiri injinia yule, ni lini sasa ombi hili litatekelezwa? Nakushukuru sana.

Name

Eng. Isack Aloyce Kamwelwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli nimefika pale Itete na Mheshimiwa Naibu Waziri amefika. Tatizo moja kubwa la Itete ni kwamba skimu ipo haijakamilishwa ujenzi lakini inafanya kazi. Tatizo lililo kubwa ni kwamba sasa hivi baada ya kumaliza huu mpango kabambe tunataka kujenga bwawa kubwa ambalo litatunza maji ili wananchi waendelee kulima wakati wote. Tatizo lingine lililokuwepo ni kwamba ile Kamati iliyokuwa imeundwa ambayo inasimamia kilimo kile cha mpunga ilikuwa na makosa kidogo, tukaivunja na sasa hivi tumeweka nyingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ombi lake la kwamba injinia sasa awe sehemu ya karibu kwa ajili ya kusimamia ile skimu tutalitekeleza tuwasiliane Mheshimiwa Mbunge ili tuweze kumpatia huyo injinia. (Makofi)

Name

Devotha Methew Minja

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. HADJI H. MPONDA aliuliza:- Mkoa wa Morogoro umechaguliwa kuwa ni Ghala la Chakula la Taifa hususani katika mazao ya mpunga na miwa. Katika kutaekeleza hili Serikali imepanga kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ujenzi wa skimu za umwagiliaji katika Vijiji/Kata za Usangule – Mto Lwasesa, Igawa – Mto Furua, Lupunga – Mto Mwalisi na Kilosa – Mto Mwalisi. • Je, ni lini kazi hiyo ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina itakamilika? • Katika kipindi hiki cha maandalizi ya ujenzi wa mabanio haya ya kilimo cha umwagiliaji, je, Serikali ina utaratibu gani wa usimamizi wa ardhi husika ili kuepuka migogoro ya watumiaji wa mabanio hayo siku za usoni?

Supplementary Question 2

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kuniona. Kwa kuwa Serikali imekuwa ikipanga miradi mingi ya umwagiliaji katika mkoa wa Morogoro ambayo haitekelezeki, je, Serikali sasa haioni kuna haja ya kwuaatumia wataalam ambao wanatoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) waweze kuwasaidia wananchi wa Mkoa wa Morogoro kuendeleza kilimo cha umwagiliaji?

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi Wizarani pamoja na changamoto ambazo tumeziona tukaona haja sasa ya kupitia ule mpango kabambe, na tumejipanga katika kuhakikisha tunakuwa na miradi michache lakini yenye tija ya uzalishaji katika nchi yetu. Kwa hiyo, wazo lako na ushauri wako tumeupokea katika kuhakikisha tunaboresha miundombinu ya umwagiliaji ili iweze kuwa na tija katika nchi yetu.