Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mattar Ali Salum

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shaurimoyo

Primary Question

MHE. MATTAR ALI SALUM aliuliza:- Tatizo la makazi kwa wanajeshi wetu ni kubwa kiasi kwamba maaskari wetu kupata usumbufu na kuathiri utendaji kazi wao. (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga nyumba za makazi kwa wanajeshi wa upande wa Unguja? (b) Je, ni nyumba ngapi Serikali imepanga kujenga Zanzibar? (c) Je, ni lini ujenzi wa nyumba kwa upande wa Zanzibar utaanza?

Supplementary Question 1

MHE. MATTAR ALI SALUM: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, lakini nampongeza sana Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri ambayo ameyatoa. Nina maswali mawili madogo ya kuuliza.
Mheshimiwa Spika, zipo nyumba za zamani kabisa ambazo wanajeshi wetu wanazitumia hadi sasa na hali yake siyo nzuri kabisa.
Je, Wizara ina mikakati gani ya kuzifanyia marekebisho angalau zikaendana na hali ya sasa?
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Katika majibu ya msingi ya Mheshimiwa Waziri, amesema hana uhakika kama atajenga nyumba Unguja kwa awamu hii.
Je, ni lini anaweza kutueleza anaweza akatuanzia nyumba za Unguja wakati Unguja bado pana matatizo makubwa ya nyumba za kijeshi? Ahsante.

Name

Dr. Hussein Ali Mwinyi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwahani

Answer

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:
Mheshimiwa Spika, kuhusu nyumba za zamani kufanyiwa ukarabati, hilo liko katika bajeti zetu. Nataka niwaeleze tu kwamba kwa kawaida bajeti inakuwa na miradi mipya na fedha za ukarabati.
Mheshimiwa Spika, sasa kwa mwaka huu wa fedha tuliweka fedha za ukarabati katika Bajeti ya Ngome na ni mategemeo yetu kwamba fedha zikipatikana tutakuwa tukirekebisha nyumba hizo awamu kwa awamu.
Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili, ni lini za Unguja zitajengwa? Kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi ni kwamba mchakato wa mazungumzo ya kupata fedha ajili ya kumalizia awamu ya pili unaendelea na utakapokamilika tu, basi bila shaka tutaanza awamu hiyo. Nataka nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba awamu hiyo itahusiaha kambi zilizokuweko upande wa Unguja.