Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza:- Mwaka 2014 Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne alitoa ahadi ya kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Makao Makuu ya Wilaya ya Kilindi hadi Wilaya ya Gairo. Je, ni lini Serikali itatimiza ahadi hiyo?

Supplementary Question 1

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri wa Ujenzi, napenda kuuliza swali moja la ziada kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiopingika kwamba barabara hii ni muhimu sana kiuchumi na ukizingatia kutoka Makao Makuu ya Wilaya ya Kilindi kwa maana ya Songe hadi Gairo ni kilometa hizo alizotaja. Barabara hii nyakati za mvua ina changamoto kubwa sana na ni juzi tu Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya alipokuwa anakuja Makao Makuu ya Wilaya, alikwama maeneo ya Chanungu pale kwa takribani saa mbili.
Swali langu linakuja, je, ni lini sasa Mheshimiwa Naibu Waziri atahakikisha kwamba watu wa TANROADS Mkoa wa Tanga wanasimamia kwa dhati matengenezo maeneo yafuatayo, kwa maana katika Bonde la Chanungu, Kijiji cha Mafulila pamoja na eneo la Kikunde, karibu kabisa na Kijiji cha Gairo hapa kuhakikisha kwamba barabara hii inapitika kwa msimu mzima wa mwaka? Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nilieleza katika jibu la swali la msingi, barabara hii ni muhimu sana na Serikali inalifahamu hilo.
Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nilisema, tunatenga bajeti ya fedha na mwaka huu zimetengwa kuhakikisha kwamba barabara hii inapitika majira yote. Kwa sababu hiyo, nawaelekeza TANROADS Mkoa wa Tanga na TANROADS Mkoa wa Morogoro kuhakikisha barabara hii inapitika majira yote. (Makofi)