Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

George Malima Lubeleje

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Primary Question

MHE. PETER J. SERUKAMBA aliuliza:- Mheshimiwa Rais alipokuja kwenye kampeni aliahidi kuanza ujenzi wa barabara ya Mwandiga – Chankele – Kagunga. Je, ni lini ujenzi wa barabara hiyo utaanza?

Supplementary Question 1

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali moja la nyongeza. Kwa kuwa Meneja wa TANROADS wa Mkoa ameshaikagua barabara ya kutoka Gulwe – Berege –Chitemo – Mima – Chazima - Igodi Moja – Igodi Mbili mpaka Seluka; na kinachosubiri sasa hivi ni barabara hii ipandishwe hadhi ili iwe barabara ya Mkoa.
Je, Mheshimiwa Waziri anasemaje na kwa ombi hilo Serikali inawaambiaje wananchi wa maeneo hayo?

Name

Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lubeleje, grader la zamani, makali yale yale kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Lubeleje swali hili alikuwa akiliuliza mara kadhaa na hapa umesema kwamba ni kweli. Kwa sababu naamini wenzetu wa Wizara ya Ujenzi jambo hili walishalisikia na ninakumbuka Naibu Waziri wa Ujenzi siku ile alikuwa analizungumza suala hili kwamba jambo hili linafanyiwa kazi. Imani yangu ni kwamba kwa sababu barabara hii ni ya kimkakati nami nakiri wazi kwamba na wewe barabara hii inakuhusu katika eneo lako. Basi naamini Wizara ya Ujenzi itafanya kila liwezekanavyo barabara hii kuipa kipaumbele katika yale matakwa ya wananchi wa eneo hilo.