Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Faustine Engelbert Ndugulile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigamboni

Primary Question

MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE aliuliza:- Pamoja na Jimbo la Kigamboni ni Wilaya ya Kipolisi, majengo ya Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Wilaya (OCD) na kituo chake ni chakavu sana:- (a) Je, Serikali inachukua hatua gani kuhakikisha Wilaya hii inakuwa na ofisi nzuri za polisi? (b) Je, hatua hizi zitaanza kutekelezwa lini?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE: Mheshimiwa Spika, naomba niulize maswali ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, Wilaya ya Kigamboni ina askari takribani 100, magari yanayofanya kazi matatu na nyumba chache sana za askari. Je, Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ina mkakati gani wa kuongeza askari katika Wilaya mpya ya Kigamboni ili kukidhi mahitaji, hususan tukizingatia kwamba, Wilaya mpya ya Kigamboni ina changamoto kubwa sana ya uvuvi haramu, uhamiaji haramu pamoja na ongezeko la uhalifu?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, nilitaka kujua; katika majibu ya Mheshimiwa Waziri amejibu kwamba ujenzi wa kituo kipya cha Wilaya utajengwa katika Kata ya Kibada mara fedha zitakapopatikana. Je, Wizara inaweza ika-make commitment kwamba itaingiza ujenzi wa kituo kipya cha Polisi cha Wilaya katika bajeti hii inayokuja ya mwaka wa fedha 2017/2018?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, kuhusiana na pendekezo la Mheshimiwa Mbunge kuhusu haja ya kuongeza idadi ya Askari Kigamboni, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali kupitia Jeshi la Polisi imeliona hilo na tunategemea pengine katika askari ambao wanaweza wakaajiriwa katika mwaka ujao wa fedha tuweze kuangalia uwezekano wa kuongeza idadi ya askari katika maeneo yote ambayo kuna upungufu wa askari ikiwemo Kigamboni.
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, ametaka kujua kwamba katika bajeti ya mwaka huu wa fedha kwamba fedha hizo za ujenzi wa Kituo cha Kigamboni zitaingizwa. Naomba kwanza nimthibitishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mpaka sasa hivi hatua ambazo zimefikiwa ni hatua za kuridhisha kwani mbali na kupatikana eneo la ujenzi wa kituo, lakini tayari hatua za awali ikiwemo utayarishaji wa ramani kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho umeshafanyika.
Mheshimiwa Spika, ninaomba nichukue fursa hii kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba wazo lake tutazingatia ingawa inawezekana ikawa kwa bajeti ya mwaka huu ikawa tumechelewa, lakini tutaangalia utaratibu mwingine wa kuweza kuangalia jinsi gani ya kupiga hatua zaidi na pale ambapo tutaweza kuingiza katika bajeti ya mwaka mwingine wa fedha, tutaziingiza kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho.