Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Atupele Fredy Mwakibete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busokelo

Primary Question

MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza:- Wananchi wa Jimbo la Busokelo hasa katika Kata za Kandete, Isange, Lutebe Lwangwa, Mpata, Kabula, Mpombo, Lufilyo Kambasegela, Ntaba, Lupata, Itete, na Kisegese wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji safi na salama; na kuna maeneo mengi ambayo mabomba uyamepita lakini maji hayatoki kutokana na kukosekana kwa matenki ya maj:- (a) Je, ni lini Serikali itatatua kero hiyo ya maji kwa kujenga matenki ya maji kwenye Kata hizo? (b) Mji wa Lwangwa ni Makao Makuu ya Halmashauri mpya ya Busokelo na kuna ongezeko kubwa la watu ukilinganisha na miundombinu ya maji iliyopo; je, Serikali ina mpango gani wa kujenga miundombinu mipya ya uzalilshaji wa maji kwenye eneo hilo jipya la mipango miji?

Supplementary Question 1

MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE: Mheshimiwa Naibu Spika, asante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, lakini kwa mujibu wa swali nilivyouliza pamoja na majibu ambayo yametolewa ni dhahiri kwamba kwa vijiji ama Kata ambazo amezisema mimi mwenyewe ni shahidi kwamba kuna hela ambazo hazijafika hadi sasa hivi na katika jibu lake la msingi amesema zimefika. Kwa mfano Kata ya Mpata, nimepeleka mabomba zaidi ya milioni 10 lakini Serikali mpaka sasa hivi haijatoa chochote. Mheshimiwa Waziri unaweza ukathibitishia wananchi wa Mpata kwamba hizo fedha zimefika kule? Hilo ni swali la kwanza.
Swali la pili, kuna baadhi ya Kata ya Ntaba, kijiji cha Ilamba wananchi pamoja na wakazi wa eneo la pale wananyang’anyana maji, wananchi na mamba, na zaidi ya wananchi kumi na moja wameshauawa na mamba ama kuliwa na mamba kwa sababu ya kutafuta maji, je, Serikali inatoa tamko gani kwa ajili ya wananchi hawa na ikizingatiwa kwamba kuna mradi ambao umeshafanyiwa upembezi yakinifu tangu mwaka 2008 hadi leo hii kwa thamani ya shilingi milioni 100, haikufanya kitu chochote.

Name

Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI (TAMISEMI, UTUMISHI NA UTAWALA BORA): Mheshimiwa Naibu Spika, asante.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwa taarifa aliyosema kwamba fedha hazijafika ni kwamba ngoja nita-cross check vizuri katika Ofisi yangu nijue ni nini kilichotokea lakini kikubwa ni nini? Ni kwamba kuna changamoto ya upelekaji wa fedha, siyo mradi huo tu isipokuwa maeneo mengi sana, fedha zimeenda kwa kusuasua na hivi karibuni ndiyo maana Waziri wa Maji juzi juzi alikuwa anazungumza kwamba kutokana na kusuasua kwa kupeleka fedha katika miradi ya maji na miradi hii mingi sasa mingine ilikuwa imesimama, sasa Serikali iliamua kwamba ile outstanding payment ambazo zilikuwa zinakaribia karibuni bilioni 28, kwamba fedha hizi sasa zipelekwe katika maeneo mbalimbali ilimradi wale Wakandarasi walio-demise mitambo waweze kuendelea.
Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge naomba nikuambia kwamba nitazifuatilia kwa karibu ilimradi kwamba huu mradi lengo letu liweze kufanikiwa na wananchi waweze kupata huduma ya maji.
Lakini sehemu ya (b) ni kwamba kuna changamoto ya wananchi wanakamatwa na Mamba. Kwanza nitoe masikitiko yangu sana katika eneo hilo, kwa sababu kama watu wanaliwa na mamba ina maana kwamba ni changamoto kubwa, tunapoteza jamii ya Watanzania.
Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge naomba nikiri kwamba nimesikia hili na nakumbuka tulifanya discussion juzi juzi kwamba katika ziara yangu nitakapokuwa nimeenda katika Mkoa wa Mbeya nimesema kipambele katika Jimbo lako la Busokelo litakuwa ni sehemu mojawapo ambayo nitaenda kutembelea ilimradi mambo haya yote kwa ujumla wake tuweze kuyatazama vizuri tukiwa site na kuweze kupanga mipango mizuri, mwisho wa siku wananchi wa Jimbo hili waweze kupata huduma ya maji, kila mtu aweze kujiona ana faraja na nchi yake.

Name

Willy Qulwi Qambalo

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Karatu

Primary Question

MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza:- Wananchi wa Jimbo la Busokelo hasa katika Kata za Kandete, Isange, Lutebe Lwangwa, Mpata, Kabula, Mpombo, Lufilyo Kambasegela, Ntaba, Lupata, Itete, na Kisegese wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji safi na salama; na kuna maeneo mengi ambayo mabomba uyamepita lakini maji hayatoki kutokana na kukosekana kwa matenki ya maj:- (a) Je, ni lini Serikali itatatua kero hiyo ya maji kwa kujenga matenki ya maji kwenye Kata hizo? (b) Mji wa Lwangwa ni Makao Makuu ya Halmashauri mpya ya Busokelo na kuna ongezeko kubwa la watu ukilinganisha na miundombinu ya maji iliyopo; je, Serikali ina mpango gani wa kujenga miundombinu mipya ya uzalilshaji wa maji kwenye eneo hilo jipya la mipango miji?

Supplementary Question 2

MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Naibu Spika, Naitwa Willy Qambalo Mbunge wa Jimbo la Karatu.
Kwa kuwa, matatizo ya maji yaliyoko Busekelo yanafanana kabisa na matatizo ya maji yanayoukumba Mji wa Karatu na vijiji vinavyouzunguka. Na kwa kuwa Mji wa Karatu unakua sana kutokana na shughuli za utalii zinazoendelea katika maeneo ya jirani. Je, ni lini Serikali itamaliza kabisa matatizo ya maji katika Mji wa Karatu na vijiji vinavyozunguka?

Name

Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI (TAMISEMI, UTUMISHI NA UTAWALA BORA): Mheshimiwa Naibu Spika, ndugu yangu huyu tukiri kwanza Busokelo haifanani na Karatu kwa sababu kule Busokelo kuna mamba, na naamini Karatu hakuna mamba. Lakini kubwa zaidi ni jinsi gani kama Serikali itajielekeza kuhakikisha Mji wa Karatu unapata maji kwanza nikiri kwamba miongoni mwa Miji ambayo Tanzania tunaitegemea katika suala zima la uchumi ni Mji wa Karatu, kwa sababu ni center kubwa sana ya utalii katika nchi yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niseme kwamba Serikali kupitia Wizara ya maji katika programu ya pili tunayoenda nayo ambayo imeanza hii Januari, tumeweka kipaumbele katika Mji Mikakati yote ambayo kwanza ina vivutio vya Kitalii, lakini ni source kubwa sana ya uchumi wa nchi yetu kuipa kipaumbele katika suala zima la huduma ya maji.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikiri wazi kwamba katika suala zima la utalii kama nilivyosema awali, Karatu ni Mji tunaoutegemea sana. Kwa hiyo suala hili tunalilchukua kwa ujumla wake, Wizara ya Maji halikadhalika Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, tutahakikisha jinsi gani tutaipa kipaumbele. Ile miradi ambayo imeanza Singida haijakamilika vizuri, au ni jinsi gani tutumie vyanzo vingine ili mradi tupate maji katika Mji wa Karatu, wananchi wa Karatu waweze kupata manufaa katika nchi yao.