Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 7 Sitting 15 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 119 2017-05-02

Name

Peter Joseph Serukamba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Kaskazini

Primary Question

MHE. PETER J. SERUKAMBA aliuliza:-
Mheshimiwa Rais alipokuja kwenye kampeni aliahidi kuanza ujenzi wa barabara ya Mwandiga – Chankele – Kagunga.
Je, ni lini ujenzi wa barabara hiyo utaanza?

Name

Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), naomba kujibu swali la Mheshimiwa Peter Joseph Serukamba, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, barabara ya Mwandiga – Chankele - Kagunga yenye urefu wa kilometa 55.76 ipo katika eneo la mwambao wa Ziwa Tanganyika. Tayari upembuzi yakinifu umefanyika na kubaini kuwa zinahitajika shilingi bilioni saba kuweza kujenga barabara hiyo.
Mheshimiwa Spika, kutokana na uwezo mdogo wa Halmashauri, ilikubalika kupitia Kikao cha Bodi ya Barabara cha Mkoa wa Kigoma, iweze kuhudumiwa na Wakala wa Barabara Mkoa (TANROADS). Maombi hayo yamewasilishwa kwa Waziri mwenye dhamana na ujenzi kwa ajili ya kupata kibali.