Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Atupele Fredy Mwakibete (18 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa wingi wa rehema kwa jinsi ambavyo alituchagulia viongozi kwa ngazi zote; nikianza na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Joseph Pombe Magufuli; Makamu wa Rais, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu; na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa.
Pili, napenda kuchangia kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Busokelo ni Jimbo ambalo tunalima mazao ya chakula na mazao ya biashara. Mazao ya chakula tunayolima ni kama yafuatayo: ndizi, mahindi, maharage, viazi mviringo na viazi vitamu, matunda mbalimbali kama maparachichi, matunda damu na mengineyo. Mazao ya biashara ni kama yafuatayo: mbao, chai, kokoa, kahawa pamoja na hiliki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na mazao hayo yote, hatuna hata kiwanda kimoja kwa ajili ya kuchakata mazao hayo yote. Inasikitisha sana kuona mkulima, tena wa jembe la mkono analima kwa taabu sana, pembejeo haziwafikii kwa wakati, zinakuja wakati muda usiofaa. Kwa mfano, mbolea za kupandia zinakuja wakati wa kupalilia na mbolea za kukuzia zinamfikia mkulima wakati anavuna. Mbaya zaidi mkulima huyu akifanikiwa kuvuna,hapati sehemu za kwenda kuuza ama kuchakata (viwanda vidogo) ili mazao yao yapate thamani kubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba Mheshimiwa Waziri awakumbuke wananchi hawa wa Busokelo kwa kututafutia wawekezaji wa mazao kama kokoa, ndizi na mahindi pamoja na viwanda vya mazao ya ng‟ombe mfano, maziwa (kiwanda cha maziwa) Kata ya Bonde la Mwakaleli (Isange, Kandete, Lubeta na Mpembo).
Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba Mheshimiwa Waziri atusaidie kutafuta wawekezaji kwenye viwanda vya gesi aina ya cabondioxide gase Co2, pamoja na umeme wa joto ardhi Geothermal eneo la Ntaba, Kata ya Ntaba ndani ya Busokelo Mkoani Mbeya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni muhimu sana tuwe na kiwanda cha kusindika kokoa kwa sababu wakulima hawa wanalima kwa wingi sana hasa maeneo ya lufilyo, Ntaba na Kambasegela ili thamani ya kokoa ipande na mkulima aweze kupata zaidi kuliko hivi sasa na itaongeza morali zaidi kwa wakulima wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, miundombinu ya Jimbo la Busokelo ni mibaya sana hasa kipindi hiki cha mvua na hivyo imepelekea zaidi ya tani nyingi sana za ndizi na maparachichi kuharibika na hivyo kusababisha umasikini zaidi kwa wakulima hawa. Namwomba Mheshimiwa Waziri, ni muhimu sana viwanda hivi vikajengwa maeneo husika ili hasara ambayo inatokana na kuharibika kwa miundombinu iweze kuepukika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuchangia hayo hapo juu, naunga mkono hoja ya Mheshimiwa Waziri kwa asilimia mia moja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia katika Wizara hii ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Mheshimiwa Spika, lakini kabla sijaanza kuchangia, napenda kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa sababu tangu uchaguzi umefanyika ametuteulia viongozi na tumepata jembe, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. Pia napenda kukishukuru Chama changu cha Mapinduzi kwa jinsi ambavyo mmekuwa nami tangu kipindi chote cha uchaguzi na hadi sasa tumepata nafasi ya kuingia Bungeni. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mimi nasema afya kwanza kwa sababu hakuna Mbunge au mwananchi yeyote ambaye anaweza akafanya shughuli za maendeleo pasipokuwa na afya. Katika kampeni zangu nilikuwa nasema afya kwanza na leo hii ikibidi naomba iwe slogan ya Taifa kama Mheshimiwa Waziri atakubaliana nayo. Napenda kuwashukuru Mawaziri kwa kazi nzuri mnazozifanya pamoja na Naibu Mawaziri kwa jinsi ambavyo mnajituma na kwa kweli hakika hapa kazi tu, tunaiona hii kazi inafanyika. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, bahati nzuri nimekuwa katika sekta hii ya afya kwa kufanya kazi na mashirika ya watu wa Marekani kupitia Jeshi la Amerika. Kwa hiyo, nafikiri Mheshimiwa Waziri ataweza kupata ushauri wangu katika mambo mbalimbali. Nikianza kwanza na Jimbo langu la Busokelo. Busokelo ni Jimbo ama ni halmashauri mpya ambapo hadi sasa ninavyosema tuna watumishi wanne tu ambao ni specialist, kwa maana ya wanaume wawili na wanawake wawili. Ni sawa na kusema asilimia 100 hatuna watumishi kwa mujibu wa takwimu za kitabu cha hotuba ya Mheshimiwa Waziri, ukurasa wa 140.
Mheshimiwa Spika, lakini pia katika Halmashauri ya Busokelo, tuna kituo kimoja tu cha afya kwa maana ya kata 13, kituo kimoja. Najua hili lipo chini ya TAMISEMI lakini kwa sababu hizi ni Wizara ambazo zina mahusiano, napenda pia Mheshimiwa Waziri alifahamu hili. Pia hatuna hata hospitali ya wilaya tunatumia Hospitali ya Kanisa inaitwa CDH. Eneo tumeshaliandaa na tumeshaanza harakati lakini tunaomba pindi tutakapoomba msaada kutoka Serikalini muweze kutukumbuka katika hili.
Mheshimiwa Spika, siyo hilo tu katika Kituo cha Afya cha Kandete ambacho ndicho kituo pekee, kinahudumia wananchi wengi sana kwa maana ya Bonde zima la Mwakaleli. Ukianzia na Kata za Itete, Kandete yenyewe, Isange, Mpombo mpaka Wangwa. Huduma zinazotolewa pale ni ambazo hakika, kama hujapata huduma pale maana yake inabidi usafiri umbali wa zaidi ya kilometa 50 kufuata huduma hizo mjini ambako ni Tukuyu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaomba kituo hiki kiwezeshwe tukianzia na masuala ya mochwari hatuna na hata dawa nazo zinafika kwa kusuasua sana. Kwa mfano MSD wamepewa jukumu la kusambaza ama kusimamia tunasema Medical Store Department nchi nzima. Wakati mwingine MSD wanachokifanya utashangaa imebaki kama mwezi mmoja, ama miezi miwili kusambaza hizo dawa kwa maana zinakuwa expired lakini wanazisambaza. Kwa hiyo, zinakuwa hazina manufaa kwa wale wanaopelekewa kwa sababu kipindi kifupi tu zinakuwa tayari haziwezi tena kutumika kwa afya ya binadamu.
Mheshimiwa Spika, nizungumzie sasa suala la huduma za UKIMWI katika nchi yetu ya Tanzania. UKIMWI ni janga la Kitaifa na Kimataifa na kwa bahati mbaya sana bajeti ya Serikali imekuwa kidogo sana ukilinganisha na uhitaji wa huduma kwa ugonjwa huu wa UKIMWI. Kuna mashirika mawili hapa nchini, kuna Global Fund na PEPFAR. PEPFAR ni President’s Emergency Plan For AIDS Relief, ni shirika ambalo liko chini ya Serikali ya Marekani, lilianzishwa enzi za Rais, Mheshimiwa Bush. Pamoja na kwamba tunatumia Global Fund ambayo ni nchi mbalimbali lakini asilimia kubwa bado inachangiwa na Serikali ya Marekani.
Mheshimiwa Spika,In case imetokea hawa Wamarekani wanasema sasa stop kuchangia Afrika na Mataifa mengine hakika Tanzania hatutakuwa sehemu nzuri. Kwa hiyo, tunaiomba Serikali kupitia Wizara hii waongeze bajeti ya kutosha katika masuala ya UKIMWI. Wakati mwingine wengi wetu tunaonesha kidole kimoja hivi kwamba yule yule ndiye anaishi na HIV lakini kwa tafiti ambazo tumefanya kwa miaka yote, kumbuka vidole vitatu vinakuonesha wewe.
Mheshimiwa Spika, niwape mfano mmoja, nilipokuwa nasimamia Nyanda za Juu Kusini, Mikoa ya Ruvuma, Katavi, Rukwa, Mbeya, nililia sana nilipofika Hospitali ya Rukwa Mjini, nilimkuta bibi mmoja kizee sana ni mgonjwa, anasema mjukuu wangu hapa sina hata Sh.1,000 ya kununua dawa. Sasa umepataje huu ugonjwa? Anasema nilikuwa namlea mjukuu wangu na kwa sababu hatuna elimu ya kumtunza mtu wa aina hiyo ndiyo nikaupata maana alikuwa hatumii hata gloves. Hakika ilikuwa ni masikitiko makubwa, hata Sh.1,000 za kununua dawa hana. Kuna dawa kwa ajili ya kuzuia opportunistic infections, Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla atakuwa anafahamu, Serikali haitoi hata wafadhili pia wamejitoa.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, lazima kama Serikali tutie nguvu sana kwa upande huo kwa sababu dawa hizi za opportunistic infections zinazuia mambo mengi. Kuna zile ambazo zinazuia fungus, magonjwa ya ngozi na vitu vingi ukiachana na zile tunazoita TLE (Tenofovir/Lamivudine/Efavirenz) ambazo hizo zinatumika hasa hasa kwa upande wa matibabu kwa mama mjamzito na anayenyonyesha. Kwa hiyo, kwa sababu wafadhili nao wanajitoa kuleta hizi dawa za opportunistic infections, ni vizuri sasa tutenge bajeti ya kutosha ili kuzuia maradhi ambayo nimeyatamka hapo awali. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naomba pia nichangie kidogo katika suala la Hospitali ya Rufaa Mbeya. Hospitali hii inahudumia Kanda nzima, iwe Njombe, Iringa, Rukwa, Ruvuma, Katavi watu wanakwenda kutibiwa pale. Kipindi kile wakati inajengwa ilikuwa ni watu milioni mbili, lakini sasa ni zaidi ya watu milioni nane. Kwa hiyo, tunaomba Serikali hata kupitia Wizara ya TAMISEMI tuweze ku-expand ili iweze sasa kuendana na mahitaji ya sasa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, si hivyo tu hata Wabunge wenzangu wamezungumzia masuala la CT-Scan, hawana CT-Scan pale na hiyo ndiyo hospitali ya rufaa. Kama hakuna CT-Scan tusitegemee watu wale wanaweza wakapata huduma zilizo bora na sahihi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, pamoja na hayo, naomba nizungumzie suala la TEHAMA, mimi pia ni mtaalam wa mambo ya TEHAMA. Leo hii tunazungumzia ulimwengu wa sayansi na teknolojia ni lazima tuhusishe pia Wizara ya Afya. Mtu kutibiwa popote pale alipo. Tunazungumzia suala la uhaba wa Madaktari Bingwa lakini kuna solution ama majawabu ambayo yanaweza yakatusaidia kama tutaweza ku-adopt, inawezekana isiwe leo au kesho lakini tuwe na wazo kwamba kuna kitu hiki kinafanyika duniani na Mataifa mengine yaliyoendelea. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuna kitu kinaitwa Telemedicine. Telemedicine ni suala la kutibu mgonjwa popote pale alipo. Kwa maana ya kwamba unaweza ukafanya naye appointment lakini utafanya baada ya kumsaidia kwa kutumia hata hizi simu za mkononi, wengi wetu tunatumia tu WhatsApp, Facebook na vitu vingine lakini simu inaweza ikafanya vitu vingi zaidi ya hivi. Kwa hiyo, Wizara naomba ilichukue wazo hili. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, pia nimeshiriki sana kuandaa na kufanya analysis za Wizara kwa maana ya kutumia tools zinaitwa database, C2C database, DHIS - District Health Information System, LAS - Lap Assessment Response System. Hizi database ni nzuri sana kwa maana ya kwamba inaweza ikaunganisha nchi nzima kufanya analysis ya tuko wapi, ni mkoa gani unaongoza na tufanye nini kwa ajili ya intervention zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ninachoiomba Wizara ni kwamba, inabidi hizi system ziwe integrated. Kwa mfano, C2C database ina version nyingi sana lakini ni muhimu sasa iwe ni web-based sasa hivi ni stand-alone, nikisema stand-alone najua mnafahamu nyie Madaktari hasa wale wataalam wa Wizara kwa maana ya kwamba ukipeleka kituoni iko pale pale inabidi tena uhamishe kwa njia ya flash ama external kuipeleka sehemu nyingine. Pamoja na hayo hii LAS - Lapla Response System imekuwa na combined na Post Training Follow-up na itasaidia sana kwa maana ya ngazi ya Wilaya. Kwa ngazi ya Wilaya itakuwa inatuma ripoti moja kwa moja kwa Wizara na haya ndiyo maboresho katika sekta ya afya. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kabla sijamaliza naomba nizungumzie suala la huduma kwa mtoto, maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Kwenye hotuba ya Waziri, ukurasa wa…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia katika Wizara hii muhimu sana katika uchumi wa nchi yetu, Wizara ya Nishati na Madini. Nakushukuru wewe kwa kazi nzuri unayoifanya, pia nimshukuru Mungu kwa kutupa nafasi hata kufika mahali hapa siku ya leo.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimshukuru Mungu zaidi kwa jinsi ambavyo alimwongoza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumchagua Profesa Sopeter Muhongo katika Wizara hii ya Nishati na Madini. Profesa hakika unaitendea haki sana Wizara hii. Pia niwashukuru wale wote ambao ni Watendaji Wakuu, Katibu Mkuu, Mkurugenzi wa REA Tanzania, Dkt. Lutengano Mwakahesya, Mkurugenzi wa Geothermal Tanzania na Watendaji wengine wote katika nishati. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya shukrani hizo mchango wangu nielekeze zaidi nikianza na umeme wa vijijini (REA). Mpango huu wa umeme vijijini hakika mwaka jana wengi wetu tumeokoka sana katika mpango huu wa REA. Tumeokoka kwa sababu pamoja na kwamba siyo vijiji vyote vimepata, naamini katika awamu hii ya III vijiji vingi vitapata umeme huu. Nikija katika Jimbo langu la Busokelo, Busokelo ni miongoni mwa Majimbo ambayo tumenufaika na mpango mzima wa REA. Pamoja na kwamba kuna changamoto za hapa na pale, kuna baadhi ya maeneo kama Lupata, ukienda Isoko, ukienda Mpata, ukienda na maeneo mengine ya Kilimansanga bado umeme huu haujafika lakini tuna imani kwamba vijiji 30 vilivyosalia, tunaamini katika mpango huu wa awamu ya III vitapata umeme.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika suala zima la mpango wa umeme vijijini, kwa vile vijiji ambavyo vilikuwa awamu ya pili, tunaomba watendaji pamoja na wahusika wote vikamilike kabla ya Juni ili wananchi wale kwa sababu tulishawaaminisha kwamba watapata umeme, na walituamini, tunaomba kabla ya Juni kwisha waweze kupatiwa huo umeme.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala zima la madini. Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa mikoa ambayo imebarikiwa sana katika nchi yetu ya Tanzania. Tuna madini ya aina nyingi sana, ukienda kule Chunya utakuta kuna gold, ukienda huku Ileje utakuta kuna madini, ukienda Kyela makaa ya mawe, ukija Busokelo, kwa hiyo tuna madini ya aina mbalimbali.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikianza na madini aina ya calcium yanayopatikana pale Mlima wa Panda Hill. Mheshimiwa Waziri katika kitabu chake haya madini sijayaona hapa, lakini naamini kwamba atatuma timu yake waweze kufanya exploration na extraction kule, basi wananchi wale watafaidi sana haya madini kwa sababu tunaamini hata utengenezaji wa mbolea aina ya NPK inatokana na madini hayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, siyo hivyo tu, nikisoma kitabu cha hotuba na Waziri ameandika vizuri sana, very technical, ukurasa wa 62 kuna madini aina ya niobium, madini haya pia Mbeya yanapatikana na kazi kubwa ni kutengeneza vifaa vya elektroniki ikiwemo pamoja na engine za ndege tunaita jet, lakini pamoja na kutengenezea vitu mbalimbali, mambo kama kompyuta na simu. Kwa hiyo, tunaomba kama yataweza kuendelezwa, pamoja na kwamba upembuzi yakinifu ulishafanyika na utafiti umefanyika, sasa kazi kubwa iliyobaki ni kwamba yaanze kufanyiwa kazi kwa maana ya kuchimbwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja kujumuisha hotuba yake hapa atuambie kwamba ni lini hasa rasmi wananchi wa Mbeya, katika maeneo ya Panda Hill, Mbeya na Tanzania kwa ujumla watanufaika na haya madini ili waweze kuinua uchumi wao.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikija katika suala la geothermal (jotoardhi). Geothermal ni umeme ambao unatokana na nguvu ama joto lililoko ardhini na Busokelo tumebahatika kuwa na sehemu inayopatikana hiyo geothermal. Kwa hiyo naomba nimshukuru Waziri kwanza kwa sababu nakumbuka siku ile alikuja, alifika katika eneo hili la Mto Mbaka na alituahidi kwamba mara tu baada ya uchunguzi ama baada ya utafiti kukamilika mwezi wa Septemba wataanza kuchoronga visima vya huko, kwa hiyo tunaomba asitusahau.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunamwomba pamoja na timu yake ya wataalam waje katika eneo hili kwa sababu wananchi wakati tunahimiza kwamba wasifanye maendeleo yoyote kwa sababu hili eneo litakuwa ni sehemu mojawapo ya kuzalisha umeme na sisi tutakuwa tunauza maeneo mengine, walisikiliza ile kauli kwa sasa hivi wanasubiria.
Mheshimiwa Naibu Spika, siyo geothermal pekee tu, katika Jimbo la Busokelo pia tuna gesi aina ya carbondioxide. Hii gesi imeanza kuchimbwa tangu mwaka 1984, lakini kwa bahati mbaya hata hivi sasa ninavyoongea tuna viwanda viwili, kimoja kipo Kanyelele na hii gesi inatoka Kijiji cha Mpata, lakini pia kuna kiwanda kingine karibu na Tukuyu Mjini kwa ajili ya gesi hii na gesi hii inatumika zaidi katika masuala mazima ya kwenye soda, kwenye bia na maeneo mengine ambayo yanasababisha vitu visioze wala visiharibike.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa bahati mbaya, kwa makampuni ambayo yamewekeza kule, kuna kitu tunaita social responsibility kwa maana ya jamii inayozunguka, huwa hawafaidiki na gesi hii. Tunaomba Mheshimiwa Waziri, kwa nguvu zako zote pamoja na watendaji wako wote kuisimamia vizuri gesi hii aina ya carbondioxide kwa sababu wananchi wanaona yanakwenda magari na kurudi kuchukua, lakini hawaoni wananufaikaje na hii gesi. Hii ni changamoto kubwa sana, kwa sababu nakumbuka kipindi tunaomba kura ni miongoni mwa mambo ambayo yalitusababisha tupate wakati mgumu sana. Kwa hiyo, tunaomba sana Mheshimiwa Waziri alizingatie hilo atakapokuwa anajumuisha hotuba yake.
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na suala hilo, ukienda Kata ya Lufilyo kuna madini ambayo yanapatikana kule kwa ajili ya kutengenezea marumaru na ukiangalia Tanzania nzima hii, mara nyingi sana tuna-rely kwenye marumaru za ku-import kutoka China lakini kule kuna madini ya kufanya hivyo. Katika Kijiji hiki cha Kikuba, Kata ya Lufilyo, kuna maji ama maporomoko ambayo yanaweza yakasababisha umeme wa Hydro Electric Power kwa maana ya umeme wa maji.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa maana hiyo basi, tunaomba wataalam ama watafiti waanze kuja kuchungulia kule kwa ajili ya kuleta wataalam ili waweze kutuambia ni kitu gani pengine baada ya hapo kitafuata ili wale wananchi wasiangalie tu yale maji yanakwisha pasipo faida yoyote, naamini tukiwekeza katika umeme itatusaidia sana kama nchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala zima la matumizi ya umeme. Mara nyingi sana tunasema umeme; naishauri Serikali tuanze kutoa elimu kwa jamii kwamba umeme huu siyo kwa ajili ya kuwasha taa, siyo kwa ajili ya kupiga pasi tu, siyo kwa ajili ya kuangalia TV ama runinga, tufikiri katika uwanja mpana hasa kwa maana ya kuleta viwanda vidogovidogo, vile vya kuchakata hata kwa mikono yao. Nafikiri umeme utakuwa na faida sana na REA hii itakuwa na faida sana kwa wananchi kama tutaanza kutoa elimu ya namna hiyo. Maana wengi wetu wanafikiri kwamba umeme ni kwa ajili ya kuwasha taa na pengine kuangalia vitu vingine, lakini kumbe umeme ni zaidi ya matumizi hayo. Nafikiri elimu hii ikiwafikia na kama Wizara watakuwa na mipango ya kutoa elimu hiyo kwa jamii itapendeza sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pia naomba nizungumzie suala zima la Serikali kuhusika asilimia mia moja katika kuwekeza kwa maana ya nishati ya umeme. Umeme ni gharama kubwa sana, tunaomba Serikali kwa jinsi ambavyo wameshaanza kutafuta wadau wengine waendelee hivyo hivyo. Hakuna Taifa lolote duniani ambalo kwa nguvu zao wenyewe wanaweza wakajitosheleza katika nishati.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa bahati nzuri nilipata nafasi ya kutembea Mataifa mengine duniani, kama Ujerumani, utakuta nyumba moja ya familia moja inakuwa na vyanzo vitano vya nishati ya umeme; utakuta kuna maji, utakuta kuna solar, utakuta kuna umeme wa upepo utakuta kuna umeme wa biogas, geothermal na kadhalika, hata ukikatika umeme wa aina moja, basi umeme wa aina nyingine ule una-take up, hivyo katika nchi yetu pia tuanze kufikiri katika mfumo huo, tusi-rely tu katika vyanzo vya umeme wa aina moja, kwa maana kwamba kuna gesi halafu pia kuna umeme wa maji, lakini pia tuanze kufikiri zile energy ambazo ni renewable kwa maana ya kwa mfano geothermal.
Mheshimiwa Naibu Spika, geothermal is an energy ambayo inakuwa renewable, inaweza ikazalisha umeme na kuzalisha na kuzalisha, lakini tuki-rely katika umeme wa maji, sisi wote ni mashahidi hapa, kwa sababu wakati mwingine, kama kipindi cha miaka miwili iliyopita nchi yetu ilikuwa katika janga kubwa, kwa hiyo umeme ama mabwawa ambayo tunategemea yalikuwa hayatoi maji sawasawa kama vile ambavyo tulitegemea. Pia tukija katika gesi, gesi ile ukisha-extract hatutegemei tena kwamba itaendelea kuwepo vilevile kwa miaka na miaka. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, niunge mkono Wizara hii na hotuba ya Mheshimiwa Waziri. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mheshimiwa Waziri atakapokuwa anahitimisha aniambie ni lini umeme wa joto ardhi (geothermal) utaanza kuchimbwa uliopo Kata ya Ntaba. Je, wananchi wa maeneo hayo watanufaikaje na mradi huo?
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna vijiji ambavyo vilikuwa kwenye awamu ya pili ya REA ila hadi sasa vijiji hivyo havijapata umeme. Tunaomba vijiji hivyo vipate umeme vilivyopo ndani ya Jimbo la Busokelo visivyopungua 30.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri atusaidie migogoro ya ardhi iliyopo, moja kwenye Bonde la Mwakaleli kati ya TANAPA na wananchi wa Bonde la Mwakaleli katika Kata za Kandete, Luteba na Isange. Tunaomba irudishwe mipaka ya zamani ili wananchi hawa wapate nafasi za kufuga na kilimo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro wa Kyeruku uliopo Kata ya Kisegese, Kijiji cha Ngeleka, kwa sababu shamba hili wananchi wanalihitaji kulilima ili wajikomboe kwenye umaskini na kwa sasa shamba hili lipo tu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Busokelo tumetenga maeneo tayari kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za NHC, wananchi hawa wapo tayari kununua nyumba hizo.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa hii na mimi niweze kushiriki kuchangia maoni yangu juu ya Mpango. Kabla kuanza kuchangia kwanza, nimshukuru Mwenyezi Mungu lakini pia niwapongeze Mawaziri wote walioteuliwa na zaidi nimpongeze Mheshimiwa Mpango na Naibu wako pamoja na watendaji wote katika Wizara hii ya Mipango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma Mpango wetu ukianza na ule ukurasa wa 34 hasahasa katika suala la afya imeonesha kwamba utajikita zaidi katika kuboresha Hospitali za Kanda na Mikoa mbalimbali. Mimi nataka niongezee jambo moja kwamba katika Sera ya Afya kama ambavyo tunajua wote inatakiwa kila kijiji kiwe na zahanati, kila kata iwe na kituo cha afya na kila Wilaya iwe na hospitali. Kwa mantiki hiyo katika huu ukurasa wa 34 sijaona kama haya mmeyazingatia kufuatana na Sera ya Afya ambavyo inataka. Kwa hiyo, ningependa hili jambo mlizingatie mtakapokuwa mnaleta ile final draft.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo la pili katika jambo hilo hilo ni katika suala la matibabu (telemedicine). Nimeona mmekazia sana kupeleka ama kutibu watu ambao tayari wameshaathirika na magojwa mbalimbali, aidha, iwe nyemelezi ama yawe magojwa yale ya kuambukiza. Kwa hiyo, nilitaka nitoe maoni yangu kwamba ni muhimu sasa kutoa elimu kwa jamii kuhusu magonjwa mbalimbali kabla ya kuanza kuyatibu kwa sababu tunasema prevention is better than cure kwa maana nyingine ni kheri kinga kuliko tiba na ndiyo maana Serikali inatumia pesa nyingi sana kutibu wakati pengine tungetumia fedha nyingi zaidi kutoa elimu kwa hayo magojwa nafikiri kizazi chetu cha Tanzania tungekuwa tuko salama zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ningependekeza kwamba muongeze neno ama teknolojia ya kutibu kwa njia ya mtandao (telemedicine). Hii teknolojia nimekuwa nikizungumza humu Bungeni tangu mwaka jana kwa maana itarahisisha kupunguza kwanza muda wa mgonjwa kwenda kwa daktari lakini pili elimu hii ama teknolojia hii itatibu wagonjwa wengi zaidi kwa sababu daktari anaweza akawa yuko Dar es Salaam anatibu wagonjwa ambao wako mikoani. Kama ambavyo mnafahamu madaktari tulionao ni wachache inabidi daktari mmoja huyohuyo awe fully utilized kutibu wagonjwa wengi zaidi kwa njia ya mtandao kwa maana kwamba mgonjwa anaenda sehemu ambapo kuna mawasiliano na anawasiliana na daktari wake through telemedicine. Kwa hiyo, ningefurahi zaidi kuona hii telemedicine inakuwa implemented hapa nchini Tanzania. Najua mmeshaanza pilot study lakini ni vizuri zaidi kuweza kufanya haraka zaidi kwa mikoa mingine kwa sababu wagonjwa wengi wanarundikana mahospitalini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo lingine nikija katika suala la nishati kwa maana ya umeme, ukisoma katika Mpango wetu tumetilia mkazo zaidi kwenye umeme wa maji. Umeme huu wa maji kama mnavyofahamu kwamba unatokana zaidi na maji lakini wakati mwingine mazingira yanakuwa si rafiki sana kwa kuwa vyanzo vya maji huwa vinakauka kufuatana na mabadiliko ya tabia ya nchi ya dunia.

Kwa hiyo, ningependekeza kwamba ni vizuri sasa pia tukajikita katika umeme unaotokana na joto ardhi (geothermal), sijaona katika Mpango wetu hapa. Geothermal ni muhimu kwa sababu ule ni umeme ambao tunaita ni renewable tofauti na maji yakishatumika wakati mwingine kama vyanzo vimekauka na huku umeme hatutaweza kupata.

Umeme upo wa aina nyingi kuna ule wa upepo, wa gesi ambao tuko nao lakini nao bado haujawa effectively fully utilized pia ni vizuri tukaendelea kuu-utilize, kuna umeme wa solar energy, biomass energy lakini nikazie zaidi katika geothermal kwa sababu kuna maeneo mengi katika nchi yetu ya Tanzania geothermal ama jotoardhi umeme huu unapatikana. Zaidi katika umeme kuna hili jambo la bomba la gesi ningefurahi ama Watanzania wengi wangefurahi kuona bomba hili linaanza sasa kusambazwa mikoani kote na lisiishie tu Dar es Salaam. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nikija katika suala la maji, maji ni uzima, maji ni uhai, maji ni utu na maji ni roho. Waheshimiwa Wabunge wengi mmelalamikia hapa mara nyingi ukisoma ule ukurasa wa 32 tunaona kuna baadhi ya miradi ambayo itaendelea katika mpango ujao, ni vizuri katika Mpango wetu kama tutaunda chombo maalum kama ambavyo imeundwa TARURA kwamba chenyewe kijikite zaidi katika kuleta maji kwa maana ya vijijini na mijini. Sasa hivi kwa tafiti niliyoifanya nimeona Halmashauri nyingi sana hazina wataalamu na ndiyo maana miradi mingine mingi inashindwa kuendelea kwa sababu hamna ile M&E (Monitory and Evolution) katika ufuatiliaji wa miradi. Kwa hiyo, ombi langu ni kwamba kiundwe hicho chombo maalum kwa ajili ya suala hili la maji vijijini na mijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nikija katika suala la kilimo, ukisoma ule ukurasa wa 28 utaona kwamba kilimo kimetiliwa mkazo lakini wewe Mheshimiwa Waziri unafahamu kwamba sasa tuna shida kubwa sana na masoko ya mazao ambayo tumezalisha, kila zao bei yake imeshuka. Kwa mfano, ukichukulia mahindi yameshuka, viazi nichukulie mfano kwa mfano kule tulikokuwa tunalima nyumbani debe moja lilikuwa linauzwa shilingi 10,000 hadi shilingi 15,000 lakini sasa hivi debe moja ni shilingi 2,000 kwa maana ya gunia zima ni shilingi 10,000 badala ya shilingi 65,000.

Kwa hiyo, kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara katika Mpango wetu kama wataanzisha section ambayo itakuwa inatoa taarifa kupitia njia ya teknolojia kama simu whatever kwa wakulima wote, tuwe na database ya wakulima ambao wanalima mahindi, choroko na kila aina ya zao wanapewa taarifa kupitia hizo simu walizonazo ama hiyo database ili wawataarifu sehemu gani masoko hayo kwa sasa bei ipo juu. Kwa hiyo, kama Mpango huu ungezingatia hilo ingekuwa ni jambo zuri na lenye tija. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika kuwekeza kwenye kilimo tumeona mazao kama chai, mahindi na baadhi ya maeneo bei ya chai ipo chini sana, lakini wenzetu jirani Kenya iko bei za juu, kwa sababu wametafuta masoko nje ya nchiyao hasa hasa Uingereza. Kwa hiyo na sisi kama tungeweza kutafuta hayo masoko ingekuwa rahisi zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nikija katika suala la teknolojia, tumeona katika ukurasa ule wa kwanza wa mwongozo wa maandalizi wa mpango wa bajeti umezungumzia mifumo mingi ambayo itatengenezwa, mimi nitoe angalizo hapa. Tumeona teknolojia hii imekuja kwa kasi katika nchi yetu ya Tanzania pia nitoe angalizo kwa maana ya mifumo hiihiii ndiyo inatumika katika masuala ya udukuzi.

Kwa hiyo, lazima tuwe very sensitive sana tunapo- implement mifumo hii kwa kuwa hata wale wanaofanya programming, coding na vitu vingine vyote wanajua namna gani ya kuiba kupitia mifumo hii kwa kuwa mimi na wewe ambao ni end user hatuwezi kujua lakini kwa kuwa mimi nimeyaishi haya nafahamu. Kwa hiyo, ni vizuri sana haya mambo yazingatiwe katika Mpango wetu. Tusilete tu mifumo kama kuleta lakini tujue pia na consequences baada ya kutumia mifumo hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tumeona katika hii mifumo kwa mfano hii ya EFD, EFD ni mifumo ambayo inatumika kukadiria mapato lakini risiti zake zile baada ya muda, ukinunua leo bidhaa ukapewa risiti baada ya wiki moja ama wiki mbili au mwezi zinafutika maana yake unakuwa hakuna tena ushahidi wa kusema wewe ulitumia ile EFD. Kwa hiyo, ni vizuri zaidi kama hizo integrated systems zitakuwa na mifumo ambayo inatoa risiti ambayo ni permanent. Kwa nini mfano ukitoa photocopy karatasi idumu zaidi wakati EFD ambayo ni ya fedha isidumu, kwa hiyo, nafikiri hilo pia mliweke vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine kwa kuwa hizi teknolojia ni nyingi wakati mwingine wanatumia commercial software ambazo ni gharama zaidi, tunaweza tukafikiri tunapunguza gharama lakini kumbe tunaongeza gharama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ningeshauri watumie open software ambazo zinatumika nchi nyingi za Scandinavia na ambazo ndizo ziko applicable duniani kwa sasa, kwa sababu hizi commercial software ni gharama na tunakuwa hatujapunguza chochote kile zaidi ya kuongeza gharama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho katika suala la TEHAMA, ingependeza na ingefaa zaidi kuundwe Bodi ya wana-TEHAMA kama ambavyo kuna Bodi za Uhasibu, Bodi za Ukandarasi, kwa sababu teknolojia ndani ya nchi yetu inakuja kwa speed zaidi. Kama tutakuwa na hawa watu kwa pamoja maana yake itaturahisishia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi zingine kama Finland wameendelea zaidi kwa sababu waligundua ile Kampuni ya Nokia, ukienda Korea Kusini kuna Samsung, ukienda Marekani hivyo hivyo lakini tukiwa na Bodi…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nami fursa niweze kuchangia katika hotuba hii ya Wizara TAMISEMI. Kabla ya yote, kwanza nianze kumshukuru sana Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema ambaye ametupa nafasi na tumeweza kuamka salama na kufika ndani ya Ukumbi huu wa Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia namshukuru sana Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anazozifanya katika nchi hii ya Tanzania; na amekuwa role model pia wa Marais wengine wa Afrika na nchi nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pasipo kusahau, niendelee kuwashukuru Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kwa namna wanavyofanya kazi vizuri. Kipekee sana, nakushukuru sana kaka yangu, Mheshimiwa Jafo, Waziri mwenye dhamana ya TAMISEMI kwa kazi nzuri na kubwa unayoifanya, nawe ukiwa kijana, umekuwa role model pia kwa vijana wenzako. Tunakushukuru sana na pongezi, tumeona namna ambavyounapambana kila kona. Vilevile kwa kusaidiwa na wasaidizi wako; Naibu Mawaziri Mheshimiwa Kandege pamoja na Mheshimiwa Kakunda pasipo kuwasahau Watendaji wote wa Wizara hii TAMISEMI, kwa maana ya Katibu Mkuu - Engineer Iyombe, Naibu Katibu Mkuu - Dkt. Zainab pamoja na wengine wote na Wakurugenzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nijikite zaidi katika suala zima la TARURA. Kwanza naipongeza Serikali kwa kuanzisha chombo hiki cha TARURA. Kimekuwa msaada mkubwa sana kwetu Wabunge tunaotoka majimbo ya vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo Waheshimiwa Wabunge wengi wamesema kwamba TARURA pamoja na kwamba imeanzishwa, lakini bajeti yake ni ndogo kwa maana ya kwamba ina urefu mpana zaidi na uchumi mwingi unatoka vijijini na malighafi nyingi zinatoka kule, lakini bajeti yake ni ndogo. Asilimia 30 kwa 70 kwa maana ya TANROADS, hii hakika hawataweza kufanya kazi yao na kufikia lengo tulilokusudia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naiomba Serikali yangu sikivu kwamba kama itaridhia kupitia Waziri Mpango baada ya kuleta bajeti yake ya Wizara ya Fedha, ingekuwa asilimia 50 kwa 50 tuna uhakika kwamba chombo hiki cha TARURA kitaweza kufanya kazi zake sawa sawa na vile ilivyokusudiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na pongezi hizo, kuna changamoto mbalimbali katika Jimbo langu la Busokelo. TARURA hii baada ya kuanzishwa mwaka 2017 tuna mahusiano mazuri sana na wale managers pamoja na coordinators wa Mkoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na mahusiano hayo, barabara ambazo ziko ndani ya Jimbo langu kwa mfumo ambao sasa hivi tuko nao ni kilometa 475 kupitia District Roads Management Systems (DROMAS) ambako ndiko zinakuwa updated barabara zote 475. Bajeti ambayoHalmashauri yangu inapata ni shilingi milioni 600.6. Sasa unaweza ukapiga mahesabu hapo kwamba kilometa 475 kwa shilingi milion 606 siyo kitu. Kwa msingi huo, kwa bahati mbaya sana pia hizi fedha ambazo zilipangwa bajeti ya mwaka 2017/2018 hazijakwenda kama ilivyokusudiwa, kwa maana ya kwamba imekatwa nusu kwamba alipe madeni ya zamani kwa maana ya kwamba ile mipango ambayo tulikuwa tumepanga kwa barabara zote hadi hivi ninavyosema, haijaweza kutekelezeka kwa sababu fedha hakuna. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naliomba pia Bunge lako Tukufu kwamba kwa umoja wetu hii TARURA lazima ipewe fedha nyingi za kutosha. Zaidi pia katika hizi barabara, kuna barabara ambazo hadi sasa hivi ninavyozungumza, wananchi wangu wamenipigia simu tangu juzi, wengine jana kwamba kuna kata ambazo hakuna mawasiliano kabisa. Kuna Kata za Mpata, Isange, Kandete, Rufilyo na maeneo mengine mbalimbali ndani ya jimbo langu, hakuna mawasiliano kabisa kwa maana ya hizi mvua zinazonyesha sasa hivi kipindi hiki cha msimu wa mvua, kumekuwa na changamoto hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali yetu kwa sababu ni sikivu, wale managers wanapokuwa wanaomba fedha za dharura wapelekewe kwa haraka zaidi kwa sababu kunakuwa hakuna mawasiliano kabisa ya wale wananchi, maana wanaishi kama kisiwa. Wakiwa kama kisiwani maana yake hawawezi kufanya chochote. Ikumbukwe kwamba Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa mikoa ile tunayoiita big four ambayo inazalisha sana raw materials pamoja na chakula katika nchi hii. Kwa hiyo, kama hakutakuwa na uwezekano wa kusafirisha mazao yanayozalishwa kule kuja mijini, maana yake hata huku mijini pia tutapata taabu kupata hayo mahitaji tunayohitaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika jambo hilo hilo la TARURA, naiomba Serikali, kwa kuwa Mkoa wa Mbeya, hasa Wilaya za Rungwe, Chunya pamoja na Busokelo, zinapata mvua karibu mwaka mzima, zaidi ya milimita 2,000 kwamwaka, tungetamani sana kama suala la kutangaza zabuni kwa wakandarasi zingeanza mwezi wa saba na wa nane ili wa tisa mkandarasi aanze kufanya kazi na wa kumi awe kazini, wa kumi na moja amalizie kazi. Ingetusaidia zaidi, kuliko sasa hivi wakandarasi wengi wamekimbia site kwa sababu mvua zinanyesha usiku na mchana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo napenda kulizungumzia ni suala la afya. Afya ni uzima na roho. Kwa kweli kipekee sana Mheshimiwa Jaffo nikupongeze tena sana, niipongeze sana Serikali yangu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jinsi ambavyo mmejenga vituo vingi vya afya katika nchi hii ya Tanzania. Historia itandikwa kwamba kipindi fulani ndipo tulijenga vituo vingi vya afya. Hongereni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na pongezi hizo, nipongeze pia suala zima katika Halmashauri yangu ya Busokelo, nimeona mmetutengea bajeti ya shilingi 1,500,000,000 kwa ajili ya kujenga Hospitali ya Wilaya. Ninawashukuru sana katika jambo hili. Pia ikumbukwe kwamba katika maombi ambayo tuliomba, kuna kituo kimoja najua Mheshimiwa Jafo atakifanyia kazi, kinaitwa Isangi. Tulishaandikiwa barua na Mheshimiwa Waziri wa Afya, lakini hadi leo hii fedha hazijaingia. Ninaamini utalifuatilia na tutaweza kupata fedha hizi ili tuweze kuendelea kufanyia kazi hicho kituo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala zima la jengo la Halmashauri. Tunashukuru Halmashauri yetu mmeipa shilingi 2,300,000,000 kwa ajili ya kukamilisha jengo. Tunawashukuru sana katika jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nizungumzie kuhusiana na suala zima la utumishi. Watumishi wetu katika Halmashauri ya Busokelo limekuwa na shida na changamoto kubwa. Tuna upungufu wa watu takribani 516 katika Halmashauri yetu, kwa maana Halmashauri ni changa na watumishi 516 ni wengi kwa maana hawapo kazini. Wengine ndio hao wamefukuzwa na wengine hawana vyeti. Kwa hiyo,tunaiomba Serikali kwamba maombi maalum ambayo Mheshimiwa tulikupelekea uweze kuyafanyia kazi na bahati nzuri mzee wangu nilikupelekea uweze kuyafanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, hatuna. Ofisi hii ilijengwa tangu mwaka 1930. Kwa maana hiyo, nazishukuru sana Kamati zote za Bunge ambazo zimepita pale, ninyi ni mashahidi. Kuna Kamati ya PAC, lakini pia Kamati ya Maendeleo na Huduma za Jamii, mmeona jengo lile kwamba limekuwa la miaka mingi. Tuiombe Serikali, tunajua kwenye mwaka huu hamjatenga fedha, lakini tukuombe Mheshimiwa Waziri kwamba mwakani tuweze kujenga Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ikizingatiwa kwamba Mbeya ni miongoni mwa mikoa ambayo pato lake la Taifa sasa hivi ni Mkoa wa pili baada ya Dar es Salaam. Kwa hiyo, ni vizuri tungeweza kuuboresha zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo napenda kuzungumzia ni suala zima la mifumo ya computer. Mimi nikiwa mdau, nimeona katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri amezungumzia mifumo mingi ya computer na wana mifumo mingi kweli kweli. Niwapongeze sana kwamba sasa nchi yetu inaenda katika digitali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ningeweza kutoa mapendekezo ama maono kwa maana ya moja, mifumo hii mingi baadhi yake inatoka nchi za nje.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.
MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Naibu Spika, Ahsante kwa kunipa fursa hii na mimi niweze kuchangia katika Wizara hii muhimu katika uchumi wa nchi yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametupa uzima na afya njema hata tumepata kufika kuiona siku ya leo. Nimshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kumwongoza vema Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na leo hii anafanya kazi iliyotukuka katika nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nimshukuru Mungu pia kwa jinsi Mawaziri wanavyofanya kazi vizuri, Mawaziri wote, Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu na Watendaji wengine. Lakini kipekee sana niwashukuru baadhi ya Mawaziri ambao walifika Jimboni kwangu, nikianzia na kaka Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, ulinyeshewa sana na mvua kipindi kile! Pia Mheshimiwa Engineer Stella Manyanya, pamoja na Mheshimiwa Profesa Sospeter Muhongo, tunawashukuru sana! (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sasa nichangie kama ifuatavyo:-
Nikianza na suala la uwanja wa ndege wa Songwe, uwanja huu umejengwa zaidi ya miaka 14 sasa, tangu ambapo ulipendekezwa, tunashukuru Serikali ilipofikia, lakini bado unahitaji kuboreshwa zaidi! Uwanja huu ni muhimu sana kwa sababu unaunganisha Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini iwe Mbeya, Njombe, Katavi, Rukwa na Ruvuma, tunautumia uwanja huu wa Songwe.
Mheshimiwa Naibu Spika, uwanja huu wa Songwe, nilikuwa nasoma kwenye vitabu umetengewa shilingi bilioni 10, lakini bilioni 10 hii naamini kwa suala la kujenga taa pamoja na kujenga ujenzi kwa maana ya fence, hakika Mheshimiwa Waziri hazitatosha kwa bajeti ambayo imetengwa pale! (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaamini uwanja huu utakapojengwa, utafungua fursa nyingi sana za kiuchumi Nyanda za Juu Kusini. Wawekezaji wengi sana ambao wamekuja ili wawekeze, lakini wanasema hatuwezi kusafirisha mizigo kutoka Mbeya, ama kutoka Songwe, ama kutoka Njombe mpaka kwenda Dar es Salaam halafu ndipo iende Ulaya, wanataka ndege Emirates zitoke huko ziende moja kwa moja Mkoani Mbeya kwa ajili ya kuchukua hizo raw products na pia ziweze kuwa processed. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pia uwanja huu ni muhimu kwa sababu kuna baadhi ya viwanda ambavyo vilikwishaanzishwa pale, vinashindwa kuendelea kwa sababu hakuna njia madhubuti; ukiangalia TAZARA, nayo haifanyi vizuri. Kwa hiyo, tunaomba uwanja huu uweze kukamilika kwa wakati ili uweze kufungua fursa nyingi za kiuchumi.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikija katika suala la barabara, suala la barabara kwa Jimbo langu la Busokelo ni changamoto kubwa sana. Nakumbuka kuna barabara ambayo iliahidiwa ni zaidi ya miaka 12 sasa inasemwa itajengwa kwa kiwango cha lami. Nikichukua kitabu cha Ilani ya Chama chetu ukurasa wa 49, hii ni Ilani ya Chama mwaka 2015 imeandikwa ile barabara pale kwamba Katumba – Mbambo - Tukuyu, kilomita 80 kwa kiwango cha lami, lakini kwa miaka yote hiyo hata hivi ninavyoongea, nakumbuka nilishawahi kuleta swali na Mheshimiwa Naibu Waziri, alilijibu kwamba ifikapo mwaka huu mwezi Septemba ama Oktoba itakuwa imekamilika.
Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, tukija katika bajeti ukifungua ule ukurasa wa 243, imeandikwa upgrading to DSD of Katumba-Lwangwa- Mbambo- Tukuyu road kilometa 83, lakini hapa inaonyesha ni kilometa moja tu! Tunamwomba sana, Mheshimiwa Waziri, barabara hii ni ya enzi na enzi, alikuja Mheshimiwa Rais Benjamin William Mkapa aliahidi, lakini alikuja Mzee, Mheshimiwa Dkt. Kikwete aliahidi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tarehe 28 Agosti, 2015 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, saa sita na dakika thelathini mchana aliahidi barabara hii na wananchi walipiga sana makofi wakiamini kwamba itajengwa. Hakika tunawaombeni sana, kwa sababu barabara hii, kule tuna vitu vingi kwanza kuna gesi asilia. Hii gesi asilia, kuna viwanda viwili ambavyo vinafanya extraction na exploration za minerals, lakini zinaharibika kwa sababu barabara haziko imara!
Mheshimiwa Naibu Spika, si gesi asilia tu, kuna suala zima la geothermal, karibu tutaanza kuchimba, umeme wa kutumia joto ardhi pia unatoka kule! Nakumbuka alipokuja Mheshimiwa Profesa Sospeter Muhongo yeye mwenyewe alijionea ile barabara hadi akauliza Mheshimiwa Mbunge hapa vipi, nikasema na mimi nitalia kilio kwa Mheshimiwa Waziri wa Miundombinu ili aweze kutuwezesha kwa barabara hii. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini si hivyo tu, hivi ninavyoongea Mheshimiwa Waziri, barabara ile nilipita mwezi wa nne hakika ilikuwa ni worse, worse, worse, nusura nipate ajali! Watano walikufa kwa sababu ya mvua ambazo zimenyesha sana kipindi hiki. Kwa hiyo, tunaomba mtukumbuke, mtukumbuke kwa maana ya kwamba, sehemu ambapo ilitakiwa tusafiri umbali wa kilometa pengine 20 inatulazimu tuzunguke sana. Kama mnakumbuka kipindi ambacho kumetokea mafuriko ya kule Kyela, watu wa Kyela wanalazimika kupita Ipinda, waje Mbambo, waje Masoko, waje Tukuyu wanatumia barabara hii na ndiyo kiunganishi pekee cha Halmashauri zote tatu, maana yake Halmashauri ya Rungwe, Wilaya ya Rungwe, Busokelo na Kyela. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunaombeni sana na si hivyo tu, ni zaidi ya tani 20 kama si 30 zimeharibika wiki mbili zimepita kwa sababu ya barabara kutopitika, kwa maana ya kwamba malori yameweza kuzuia njia na hakuna abiria anayeweza kupita pale na utelezi ni mkali sana. Kwa hiyo, wananchi ambao wanalima wanashindwa kwenda kupeleka mazao yao kwenda mjini kwa sababu hakuna magari yanayokwenda kule kuchukua bidhaa zao, kwa hiyo tunawaombeni sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini siyo hivyo tu, kuna suala zima la madaraja. Madaraja ni changamoto kubwa, ni changamoto kubwa kwa sababu sasa mvua zilivyonyesha zimesababisha baadhi ya madaraja hayo kuondoka, kwa maana ya kwamba wananchi wanatumia tunaita madaraja utepe. Sasa baadhi ya wanafunzi hawawezi kwenda ng‟ambo ya pili ya mto kwenda kusoma kwa sababu hawawezi kuning‟inia kwenye zile nyaya ama zile kamba ambazo zimewekwa pale. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba kama kuna emergency plan yoyote iweze kutusaidia ili haya madaraja yaweze kujengwa hasahasa daraja la Nsanga. Halafu kuna daraja ambalo lipo Kata ya Kisiba ambalo linaitwa Kibundugulu, hii Kibundugulu imesababisha hata kwenye mitandao, ambao mna WhatsApp, baadhi ya akinamama wanatembea juu ya kamba, inasikitisha sana! Kwa mfano, kama huyo mama ni mjamzito kwa vyovyote vile hawezi kuvuka pale kwa sababu inahitaji apite mmoja baada ya mwingine. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaombeni sana Wizara hii kupitia Wizara ya Miundombinu mtusaidie kutengeneza hata emergency, wakati bado tunaendelea kusubiri hiyo long plan kwa ajili ya kutusaidia kujenga madaraja. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mbali na hayo, pia kuna suala hili la mitandao ya simu; mitandao ya simu ina-diverge sana kulipa kodi na kwa bahati mbaya sana pengine sijui tuna mtambo ama hatuna mtambo, lakini ni muhimu kupitia TCRA wawe na mtambo ambao unaweza uka-filter ama ukajua ni kiwango gani cha course ambazo kila siku zinaingia na kiwango gani cha mapato hata kama ni hizi M-pesa, Tigo pesa ili Serikali ipate mrabaha wake sawasawa, iwezekanavyo. Kwa maana hiyo basi, ni muhimu kuanzisha mitambo kama nchi zingine ambapo inarahisisha sana kutokuwa katika quarrels na Serikali kwa maana ya kufuatilia masuala ya kodi, mara hapa, mara pale, wewe unaingia tu kwenye system unajua bwana wewe umefanya hivi na hivi then lipa kodi.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja, ahsanteni sana!
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kushauri Serikali kwenye Mpango wa mwaka 2017/2018 kama ifuatavyo:-
(i) Kilimo; kuongeza nguvu kubwa ya kuwasaidia wakulima kwa kuongeza pembejeo za kilimo na mbegu yenye ruzuku, kwa mikoa inayozalisha mazao mengi ya chakula na biashara.
(ii) Mifugo; ni muhimu kupunguza ama kuondoa kabisa migogoro ya wafugaji na wakulima, kwa kuwatengea maeneo maalum kwa ajili ya malisho ya mifugo yao.
(iii) Elimu; ni muhimu kwa Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kuanza mean test mapema kwa ajili ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu wanaoomba mikopo, ili kupunguza matatizo yanayotokana na kukopeshwa kwa wahitaji hao. Elimu ya shule zetu iwe ni kwa vitendo zaidi kuliko nadharia.
(iv) Afya; ni muhimu kupanga bajeti ya afya ambayo itakuwa inalenga kujitegemea kama nchi kuliko kutegemea wafadhili. Mfano, magonjwa kama ya UKIMWI, dawa zake zinategemea zaidi Global fund na President‟s Emergency Plan for Aids and relief from America (PEPFAR) ambapo Serikali bajeti yake ni kidogo sana na hivyo inaweza kupelekea maafa makubwa kama wafadhili hawa watajitoa na ukizingatia kuwa sera za nchi zao zinabadilika.
(v) Telemedicine; ni muhimu Wizara ya Afya kufanya matibabu kwa njia za mtandao yaani telemedicine.
(vi) Barabara (Miundombinu); kuna umuhimu mkubwa wa kujenga barabara ya kutoka Katumba-Lwangwa –Mbambo-Tukuyu iliyopo Mkoani Mbeya Wilayani Rungwe. Barabara hii inatakiwa kujengwa kwa kiwango cha lami ili wananchi wa Majimbo yote matatu yaani; Busokelo, Kyela na Rungwe wanufaike kwa kuweza kusafirisha mazao mbalimbali kama ndizi, mpunga, kokoa, viazi mviringo, chai, mbao, mahindi na mazao mengine mengi, lakini pia usafirishaji wa gesi asilia aina ya carbondioxide (Co2).
(vii) Geothermal (Nishati ya Umeme); ni muhimu kama nchi kuweza kuanza kuwekeza kwenye umeme wa joto-ardhi ambao unapatikana Jimbo la Busokelo, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya eneo la Kata ya Ntaba.
Mheshimiwa Naibu Spika, nategemea mapendekezo yangu yatapewa kipaumbele.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa fursa na mimi
niweze kuchangia katika hoja iliyo mbele yetu, ya Kamati ya Miundombinu. Kwanza niipongeze
kamati kwa jinsi ambavyo wameleta taarifa ambayo iko vizuri na ipo very detailed pamoja na
Mwenyekiti wa Kamati hii. Nina mambo machache ya kuweza kuchangia.
Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza ni suala la viwanja vya ndege, nikisoma ukurasa wa
17 inaonesha kabisa viwanja vya ndege vingi katika nchi yetu vinaendelea kujengwa. Lakini
kuna viwanja ambavyo vilikuwa vilikuwa vinaendela kwa muda mrefu hadi sasa hivi
wanapoleta hii ripoti havijapelekewa pesa hata senti.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikianza na kiwanja cha ndege cha Songwe. Kiwanja cha
ndege cha Songwe mwaka 2015/2016, kilitengewa shilingi bilioni tano lakini hawakuletewa
fedha hizo, mwaka 2016/2017, tumetengewa bilioni saba hadi wanaandika ripoti hii
hawajaletewa hata senti tano, maana yake nini?
Mheshimiwa Naibu Spika, kiwanja hiki, ni mfano mzuri kwa mikoa ya Nyanda za Juu
Kusini, Mkoa wa Mbeya, Rukwa, Katavi, Njombe, Iringa mpaka Songea. Kwa maana nyingine
kwa wale wote ambao wanatumia ndege zinazokwenda Mbeya ni hivi karibuni ni majuzi tu
fastjet imerudi kwa sababu ya kutoweza kutua katika kiwanja kile. Imerudi kwa sababu ukungu
ambao unatanda eneo lile, hakuna taa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama nchi na kama Taifa tunataka tuwekeze zaidi katika
masuala ya viwanda, na wawekezaji wengi wanataka watumie usafiri huu wa njia ya ndege
kwa ajili ya kuja kuwekeza viwanda vyao hapa nchini. Kwa hiyo, naiomba Serikali kwamba, kwa
bajeti ambazo zimetengwa katika viwanja ndege mbalimbali kati nchi hii; ukizingatia
Mheshimiwa Rais, nampongeza kwa sababu ameshanunua ndege nyingi katika nchi hii, na
bado tunaendelea kununua kama Serikali. Kwa hiyo, viwanja hivi viweze kupelekewa fedha zao
kwa wakati na viweze kutengenezwa kwa wakati. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine muhimu zaidi ni suala la barabara kwa za
kuunganisha kwa kiwango cha lami. Nizipongeze Serikali ya Awamu ya Nne na ya Tano zote
zinaendelea kuthubutu kuunganisha maeneo mbalimbali katika nchi yetu kwa ajili ya
kuunganisha wananchi, lakini pia kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kiuchumi. Nimuombe pia
Mheshimiwa Waziri, kwamba kuna barabara ambayo imeahidiwa mara nyingi, na nimeisema
hapa Bungeni kwa miaka mingi; barabara ya Katumba - Lwangwa - Mbwambwa - Tukuyu,
kilomita 83, na wewe Mheshimiwa Naibu Waziri uliona jinsi ambavyo wananchi tulipokea kwa
furaha na tupo tayari hata kutoa maeneo yetu kwa ajili barabara iweze kujengwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni suala la mawasiliano. Mawasiliano katika nchi
yetu yamekuwa kwa haraka sana, lakini jambo ambalo linasikitisha kidogo kwa wenzetu hawa
wa TCRA kumekuwa na utapeli mkubwa sana kupitia mawasiliano ya simu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nilikuwa naomba Wizara, lakini pia na wataalam,
kuna wataalam wazuri katika nchi hii ambao wanaweza wakaishauri Serikali ni mechanism gani
zitumike kwa ajili ya kuwabana wale wote ambao ni matapeli kwa njia ya mawasiliamo na
ninaamini kwa kuwa na mimi pia niko kwenye fani hiyo tunaweza tukasaidiana na watu wengi
kuiwezesha Serikali ili wananchi wake wasitapeliwe.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni suala la umeme/nishati. Nakupongeza sana
Mheshimiwa Profesa Sospeter Muhongo pamoja na Naibu wako kwa kazi nzuri mnazozifanya.
Suala la REA III na REA II imekuwa ni changamoto katika baadhi ya maeneo.
Mheshimiw Naibu Spika, mara nyingi Mheshimiwa Waziri umekuwa ukisistiza kwamba
wakandarasi wanapokuja katika maeneo yetu lazima wawasiliane na viongozi ambao ama ni
Waheshimiwa Wabunge ama Madiwani. Lakini kwa bahati mbaya sana wakandarasi
wanakwenda eneo…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nipo. Kwanza nashukuru kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia Wizara hii muhimu. Nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri ambazo anazifanya katika nchi yetu ya Tanzania. Tumeshuhudia jinsi ambavyo anajenga flyovers, tumeshuhudia jinsi ambavyo nchi yetu imeingia mikataba ya kujenga standard gauge katika reli ya kati, tumeshuhudia jinsi ambavyo majengo ya hosteli Dar es Salaam yamekamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wizara hii kwa upande wetu wa Busokelo kuna barabara ambayo inaanzia Katumba – Luangwa - Mbambo mpaka Tukuyu, ina urefu wa kilometa 83. Hata kwa haya ambayo tumepata si haba, tunakushukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa jinsi ambavyo umeshiriki kikamilifu pamoja na wataalam wako. Bado tunaomba kwa kuwa kilometa ambazo umetupa sasa hivi bado hazijatosheleza zile kilometa 83. Kwa hiyo, tunaomba ikiwezekana katika bajeti yako uweze kutuongezea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona pia jinsi ambavyo Wizara inavyofanya kazi vizuri hasa katika suala la mawasiliano. Nitoe ushauri wangu katika mambo machache hasa TCRA. Tumeaona jinsi watu wengi sana tunatumia mifumo hii ya simu lakini kwa bahati mbaya inatumika hata kwa njia ya uhalifu na TCRA wanashindwa kudhibiti na hata wakati mwingine watu wanatuma meseji za kutukana wenzao, kwa hiyo tulitaka mifumo hii iboreshwe vizuri ili wawe na mfumo ambao unaweza uka-filter, maana kila utakapokwenda TCRA wanakwambia hatujui ama mfuate mwenye namba fulani. Kama kutakuwa na systems ambazo zinaweza zikafanya kazi vizuri, bila shaka uhalifu ambao unaendelea sasa hivi nchini kwa kutumia njia ya mtandao hautakuwepo tena. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nichangie katika suala la mifumo ya kompyuta, ukisoma kitabu cha Waziri ukurasa wa 202, wamesema watajenga National Internet Data Center. Napenda nishauri kama Mtaalam wa Mifumo ya Kompyuta, unapojenga Data Center ya nchi ambapo mtakuwa mna-share information mbalimbali, haitakiwi iwe centralized sehemu moja, iwe decentralizide ili ikitokea in case kuna any emergencies zile backups ziweze kufanya kazi vizuri, kama nchi za wenzetu za Ulaya wanavyofanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nashauri katika jambo hili la mawasiliano, mara nyingi sana katika nchi yetu tunatumia soft ambazo tunasema ni commercial, commercial kwa maana ya kununua hizo software, lakini kama tungekuwa tunatumia software ambazo ni open source na gharama yake ni ndogo ni rahisi kuzi –maintain kwa maana ya sustainability yake inakuwa ni kubwa kuliko hizi commercial software ambazo tunanunua kwa gharama kubwa na kuzi-maintain kwake ni gharama kubwa vilevile. (Makofi)

Kwa hiyo, ningeshauri Serikali ianze sasa kama Mataifa mengine ambayo yameanza hasa nchi za Ulaya Magharibi zinafanya hivyo, lakini ukienda Marekani wanatumia zaidi hizi microsoft ambazo ni gharama kuzi-maintain lakini pia kuna software nyingi ambazo ningeweza pengine kuzitaja kuna hizi Postgrace, Oracle, Square Server, Survey, GSMO, kwa sababu nimeishi nazo naweza nikaishauri Serikali iweze kufanya hivyo. Pia kuna software nyingi, kuna nyingine ambazo zinatumika kwa ajili ya kuisaidia nchi iweze kupata mapato yake vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe ni shahidi sasa hivi Serikali ikitaka kupata mapato mazuri kutoka kwenye mitandao ya simu lazima waende kwenye mobile operator mwenyewe kwamba sasa mwezi huu umepata kiwango gani, wakati ilitakiwa wawe na mfumo ambao wao wanapeleka direct. Kwa hiyo, kila muamala unaofanyika either uwe wa pesa ama uwe wa simu Serikali iwe inajua kwa kiwango gani inaweza kupata mapato yake kupitia kwenye mifumo hii ya simu. Kwa sasa hivi Serikali inaibiwa sana kwa sababu hatuna hiyo mifumo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi za wenzetu ambazo zimeendelea sasa ukienda kama Ethiopia, Afrika Kusini na nchi nyingine za Ulaya wana mifumo ambayo inakuwa centralized siyo kama sasa hivi ambavyo imekuwa decentralized. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niweze kumalizia kwa upande wa TBA. TBA inafanya kazi nzuri na nimeambiwa pia kwamba mmepewa kazi ya kujenga majengo ya Halmashauri mbalimbali nchini. Kwa bahati mbaya sana TBA katika baadhi mikoa hampo ikiwemo hata kule kwetu katika Jimbo la Busokelo, katika mkoa mzima wapo watatu tu. Kwa hiyo, fedha za Halmashauri nyingi mpya ambazo zimepewa zipo tu kwenye akaunti za Halmashauri na karibu mwaka wa fedha unakwisha. Tunapofuatilia na kufuatilia wanakwambia wamepewa kazi TBA. Kwa hiyo, tunaomba kama TBA watajenga na kwa kweli wanajenga kwa kiwango kizuri na kwa gharama nafuu, basi iongezewe uwezo zaidi ili iende hadi huko mikoani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, napenda kuunga mkono hoja. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunipa fursa hii ya kuweza kuchangia kwenye Wizara hii kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Busokelo lipo Mkoa wa Mbeya, Wilaya ya Rungwe. Kwa bahati mbaya sana miundombinu ya barabara haipo vizuri. Jimbo hilo tunalima mazao mbalimbali, kwa mfano, ndizi, kokoa, chai, viazi mviringo na vitamu, mihogo, mahindi, ufugaji wa ng’ombe wa maziwa, kilimo cha matunda, maparachichi, upasuaji wa mbao na shughuli zingine mbalimbali. Hata hivyo, miundombinu ya barabara ni mibovu sana, imesababisha mazao mengi kuoza, kuharibikia shambani na hivyo kuwafanya wananchi wa Busokelo kuwa maskini kwa sababu ya barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara tunazoomba kupandishwa hadhi ziwe chini ya TANROAD Mkoa wa Mbeya ni zifuatazo:-
(i) Barabara ya Lwangwa – Tiete-Lufilyo (kilomita15).
(ii) Barabara ya Kanyelele (Gesi) – Mpata –Ipembe –Suma (kilomita15).
(iii) Barabara ya Kyejo (Gesi) – Lwangwa (kilomita 5.7).
(iv) Barabara ya Lugombo-Bujingijira – Ngumbulu - Mbeya Vijijini (kilomita10).
(v) Barabara ya Itete – Kisegese – Ntaba - Ngeleka - Matema (kilomita 30).
(vi) Barabara ya Kilasi – Kitulo (Livingstone) - Makete (Njombe) (kilomita 30).

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya lami kutoka Katumba (Tukuyu) - Lwangwa - Mbambo Tukuyu, tunaomba sana iendelee kujengwa kwa kiwango cha lami kutoka Busokelo – Isange - Katumba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni muhimu TCRA waweke mifumo ya kukusanya kodi toka kwa mobile operators. Mheshimiwa Mwenyekiti, Uwanja wa Ndege wa Songwe. Uwanja huu ni muhimu sana kwa Nyanda za Juu Kusini. Uwanja unahudumia Mbeya, Njombe, Rukwa, Katavi na Ruvuma pamoja na nchi jirani kama Malawi, Zambia, Congo na nyinginezo. Tunaomba kuwekewa taa za kuongozea ndege, kwa hali ilivyo hivi sasa, ndege haziwezi kutua wakati wa usiku na wakati wa ukungu na hivyo kusababisha hatari kwa abiria na usalama kwa ndege zenyewe. Aidha, naomba jengo la utawala lililopo Songwe limaliziwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuundwa kwa Bodi ya Wanasayansi waliomaliza masomo ya computer Science and Information Technology. Nchi yetu inapita kwenye sayansi na teknolojia. Asilimia kubwa ya pato la Taifa ni kutokana na mifumo ya IT. Napendekeza kuwepo na Bodi ya wana-IT ambayo itasimamia uvumbuzi wa teknolojia ndani ya nchi yetu kuliko kutumia wataalam kutoka mataifa ya nje kama ilivyo sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, softwares & database; nashauri Serikali yetu ianze kutumia Open Source na STO Commercial Softwares ili kupunguza gharama za manunuzi na za uendeshaji. Kwa mfano, Postgress, SQL server, Geo- Network, Geo-Server, Survey Gizmo na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TTCL, National Internet Data Centre. Pamoja na kujenga data centre naomba iwe very strong na ijengwe maeneo tofauti tofauti ili back-ups ziwe mbali na systems.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE: Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza Serikali iliyo chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Busokelo ni jimbo changa na miundombinu ya maji ni tatizo kubwa sana, hasa Mji wa Lwangwa, Kandate, Ntaba na maeneo mengine. Miradi wa Masoko na Mwakaleli I na II ni miradi ya miaka mingi sana lakini hadi sasa haijakamilika. Kwa sababu hiyo, naomba Serikali iweze kutimiza ahadi ya viongozi wetu wa Serikali. Naomba majibu ya Serikali, ni lini Miradi ya Masoko, Mwakaleli I na II itakamilika?

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa dhamira yake ya dhati kuhakikisha Serikali yake inamtua ndoo kichwani mama wa Kitanzania mijini na vijijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawapongeza pia Mheshimiwa Waziri wa Maji na Naibu wake, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Wakurugenzi na watendaji wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuchangia kwenye Wizara hii ya Maji kama ifuatavyo; maji ni uhai, maji ni roho, maji ni utu, yaana zaidi ya 65% ya mwili wa binadamu na maisha ya wanyama, mimea na binadamu yanategemea maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, ndani ya Jimbo langu la Busokelo kuna miradi ya maji ambayo inaitwa Mwakaleli I tangu mwaka 2009 hadi leo hii mradi huu bado haujakamilika na mkandarasi anasuasua kiasi kwamba hadi sasa chanzo cha maji hakijajengwa na wananchi wangu wanapata shida kubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto kubwa kwenye Wizara hii ni ukosefu wa wataalam ngazi za Halmashauri na Mikoani inayosababisha miradi mingi kushindwa kuendelea na kusimama. Wataalam wa Halmashauri wapo chini ya Wizara ya TAMISEMI, lakini Wizara ya Maji ambao ndiyo wasimamiaji wakuu wa maji, hawana mamlaka juu ya wataalam hao Halmashauri na hivyo kupelekea kuwa vigumu kuwawajibisha wanapokuwa wamekosea. Ushauri wangu wataalam hawa wawe chini ya Wizara ya Maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja ya kuanzishwa kwa Wakala wa Maji Vijijini ili waweze kusimamia kwa ukaribu na ufasaha kuliko hivi ilivyo kwa sasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la miradi ya umwagiliaji limekuwa ni tatizo kubwa sana kwa wananchi wa Jimbo la Busokelo. Kuna skimu za umwagiliaji kwenye Mto Mbaka, Kata ya Kambasegela imesahaulika na kuna kituo cha umwagiliaji ambacho kilijengwa tangu mwaka 2009 hadi sasa hakuna mwendelezo wa aina yoyote na hivyo kuisababishia hasara Serikali maana kuna majengo ambayo tayari yalijengwa kama nyumba ya mtumishi, madarasa, mabweni ila bado bwalo tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja ya kuongeza shilingi 50 kwa lita moja ya mafuta aina ya dizeli ama petroli.

Mheshimiwa Naibu Spika, wataalam wetu ngazi za Halmashauri ni muhimu wapewe/kuwezeshwa namna ya ku- design na ku-survey miradi ili zoezi hili lisitegemee wataalam toka Wizarani.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia katika Wizara hii ya Afya.

Kwanza nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu tupo hapa kwa sababu ya afya na pia nimshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jinsi ambavyo ameitendea haki Wizara hii ya Afya. Tumeona na tumeshuhudia ajira zikitolewa, tumeona jinsi ambavyo magodoro pamoja na vitanda vikipelekwa kwenye Halmashauri zote nchini, pia tumeona jinsi ujenzi wa chuo pamoja na hospitali ya Mloganzila kule Dar es Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zote hizi tunasema ahsante sana Mheshimiwa Rais pamoja na wasaidizi wake wakuu ambaye ni Mheshimiwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu pamoja na Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla, hongereni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija katika Jimbo langu la Busokelo kuna changamoto ambazo mara nyingi nimekuwa nikiongea nawe Mheshimiwa Waziri kwa bahati mbaya sana hazijaweza kutekelezeka. Tuliomba mashine ya usingizi na kwa bahati mbaya pia tuna kituo kimoja tu katika Jimbo zima la Busokelo na mashine hii haipo, maana yake inawalazimu wananchi wangu kusafiri umbali wa zaidi ya kilometa 60 kufuata huduma mjini. Kwa hiyo, nitashukuru sana kama ambavyo uliniahidi kwamba unaweza kufuatilia na kutupatia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tunaomba sana katika hospitali hii ya Kandete tunasema kuna changamoto ya ultra sound na x-ray machine hatuna. Kwa hiyo, tunaomba kama mtaweza kutusaidia katika jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwashukuru sana kwa jinsi ambavyo mmejitahidi kupeleka dawa, lakini hizi dawa kwa bahati mbaya wakati mwingine ama yanachelewa kununuliwa katika Halmashauri zetu ama kunakuwa kuna technical delay hapo katikati. Kwa hiyo, tunaomba Wizara kama mtafuatilia vizuri na hii inakuwa ni nchi nzima. Wizara inatoa fedha lakini Halmashauri haziwajibiki ipasavyo. Kwa hiyo, katika hili nafikiri ingekuwa jambo jema kama tungefuatilia pia kama Wizara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine niwashukuru kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Mbeya. Hospitali ya Rufaa ya Mbeya tumeona jinsi ambavyo mmeipa kipaumbele kwa maana ya majengo pamoja na vitanda. Bado haitoshi hospitali hii kuna specialist ambao wapo pale kwa zaidi ya miaka mine, categorization zao za mishahara bado ni zilezile za zamani. Kwa hiyo, tungeomba hata hospitali nyingine katika nchi hii ambapo wamepandishwa ngazi kwa kusoma ama kwa taaluma yao waweze kulipwa kufuatana na jinsi ambavyo wanafanya kazi pale kazini kwao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nizungumzie suala hili la TEHAMA kwenye afya. TEHAMA kwenye afya ni muhimu sana katika ulimwengu wa sasa, ukizingatia kwamba kwa sasa bajeti iliyopita Wizara mlipendekeza kwamba mtaanza kutumia tele-medicine. Tele-medicine ni mfumo ambao unatumika kutibu wagonjwa ama kufanya consultation na wagonjwa kwa daktari alie mbali na eneo husika. Anaweza akawa Dar es Salaam akamtibu ama akampa ushauri mtu ambaye yupo nje kabisa na Dar es Salaam labda mikoani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaomba hii tele- medicine iweze kuwezeshwa zaidi ili daktari aweze kupata nafasi ya kuhudumia wagonjwa wengi zaidi kuliko hivi sasa mpaka mgonjwa ama client aende hospitalini kutibiwa. Ni muhimu sana hili lizingatiwe kama Wizara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ningefurahi zaidi kuona database ambazo zinatumika hospitalini hasa hizi za CTC II ambayo ni Care and Treatment Clinic pamoja na DHIS II ambayo ni District Health Information Systems kama zinakuwa developed au programmed na wazawa kuliko hivi sasa wazawa wanashiriki kwa sehemu ndogo, asilimia kubwa sana tunapewa misaada kutoka nje kwa maana kwamba hata wale specialist wa kusimamia hizi. Lengo lake ni kufanya sustainability yake iweze kuwepo kwa sababu hii misaada kuna wakati itakwisha na ikiisha hatutakuwa tena na support nyingine yoyote. Kwa hiyo, tukiwashirikisha wazawa itaturahisishia zaidi kufanya kazi vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nikija katika suala la HIV (UKIMWI) tumeona mmetenga shilingi bilioni 251.5; ninaiomba Wizara na Waheshimiwa Wabunge ninyi ni mashahidi, hivi karibuni tulikuwa na semina ya kutoka National Council of People Living With HIV humu ndani. Tuliona kwamba kuna changamoto kubwa sana kwa dawa kwa ajili ya magonjwa nyemelezi. Kwa bahati mbaya sana hizi opportunistic infections wafadhili hawatoi wala Serikali hainunui. Maana yake inaishia kuwa gharama kwa wagonjwa...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo naomba niunge mkono hoja. Ahsante.
Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari za Mwaka 2016
MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja ya Muswada wa Sheria ya Habari kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuundwa kwa ithibati ya wanahabari. Hii itasaidia kuwezesha tasnia hii ya habari kuheshimika kama ilivyo bodi za taaluma zingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuongeza hisa zaidi kwa wamiliki wa vyombo vya habari kwa Watanzania 51% na wageni toka nje 49%. Hii itasaidia sana uimarishwaji wa ulinzi kwa nchi na kupunguza habari zisizo za kweli kwa Mataifa ya nje.
Mheshimiwa Mwenyekiti, bima ya afya. Muswada huu wa sheria unatoa umuhimu wa bima ya afya kwa wananchi wote na itawasaidia wakati wanapopata matatizo wakiwa kazini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri. Ningependa kushauri kuwa pamoja na umuhimu wa Muswada huu, ni vizuri tukazingatia umuhimu wa kuandika kanuni mapema ili baada ya Mheshimiwa Rais kusaini, sheria hii ianze mapema kutumika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono Muswada huu.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi hii nami niweze kuchangia katika Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi Wizara hii ndiyo utii wa mgongo wa nchi yetu ya Tanzania lakini niwashukuru sana na kuwapongeza Mawaziri wote wawili mara nyingi sana nikiwa na changamoto huwa nawaona, Naibu Waziri amekuwa akinisaidia na Waziri amekuwa akinisaidia, kwa hiyo nawapongeza sana. Niwapongeze kipekee zaidi baada ya kutoa tozo katika mazao mbalimbali ambazo wakulima ilikuwa ni shida na changamoto kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina ushauri mchache kwa Serikali hasa tukianza na Jimbo langu la Busokelo ambako mara nyingi sana tunazalisha lita za maziwa zaidi ya 30,000,000 kwa mwaka lakini yanaharibika kabla hayajafika kiwandani kwa sababu hatuna kiwanda katika Halmashauri ya Busokelo. Tumejitahidi kujenga lakini tumeshindwa, tunaomba Serikali iweze kutusaidia katika hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, si hilo tu tunazalisha pia ama tunalima viazi mviringo, viazi vitamu, ndizi kwa wingi, mpunga na mazao mengine mbalimbali na hayo yote yanashindwa kufika sokoni kwa sababu ya miundombinu ambayo haiko rafiki kwetu. Kwa hiyo, tunaomba kama itawezekana kuanzishwa kwa viwanda vidogo vidogo katika maeneo yale kwa kuwa ninyi watu wa kilimo ndio wenyewe kwa sababu ninyi ndio mnaosimamia sekta hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna tozo ambazo zimetolewa hasa katika zao la chai. Zao la chai sisi ni wakulima wakubwa katika nchi hii ya Tanzania katika Wilaya ya Rungwe. Kuna hii tozo ambayo inaitwa gharama za uendeshaji wa vyama vya wakulima nafikiri kwa typing error imeandikwa ni Sh.5 lakini tozo hii ni Sh.9.50, ningeishauri Serikali isiiondoe kwa sababu kwanza hivi vyama ni vichanga na Serikali inahubiri habari ya ushirika. Sasa wakishawaondolea hawa maana yake watatawanyika kabisa hawatakuwa na nguvu yoyote ya kuweza kusimama na kulisimamia zao hili la chai, kuna kodi nyingi ambazo ningeshauri huko ndiko wangeweza kuondoa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya muda, zao la cocoa pia tunalima kule lakini hapa sijaona hata kidogo kutamkwa katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri. Naomba pia walizingatie kwa sababu ni muhimu na linaingiza fedha nyingi za kigeni kwa nchi yetu ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pembejeo limekuwa likizungumzwa lakini nipongeze Serikali kwa sababu tumeamua kwamba ziletwe kwa bulk procurement. Wazo langu na ombi langu kwa Serikali kwamba katika nchi ya Tanzania kila sehemu tunazalisha ila kwa bahati mbaya majira yanatofautiana. Kwa hiyo, hata kama watanunua hizo pembejeo basi ziende kwa majira husika katika maeneo husika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye suala la TEHAMA na kilimo. TEHAMA na kilimo kwa nchi ambazo zimekomboka limekuwa ni msaada mkubwa sana katika nchi hizo. Hii TEHAMA itumike vizuri katika kuendeleza mazao mbalimbali nchini si kilimo tu hata uvuvi lakini pamoja na shughuli zingine zozote za kibinadamu zinazomwingizia kipato. TEHAMA inatumika namna gani? Kama sasa hivi tukijenga data center itapunguza gap kati ya watafiti wanaofanya tafiti pamoja na mkulima kwa sababu mtafiti mara nyingi anafanya tafiti lakini zile tafiti haziwasaidii wale wakulima wadogo wala wavuvi, wala wafugaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kupitia TEHAMA maana yake watakuwa wanapata SMS direct kutoka data center hiyo kwenda kwa mkulima kama watakuwa na simu za mkononi tu inatosha kabisa. Kupitia TEHAMA pia tutapunguza majanga mbalimbali kwa kutoa taarifa kwa jamii mapema. Kwa mfano, mwaka jana tulikuwa na changamoto kubwa ya ukame, kama wakulima wa maeneo mengi wangepata taarifa kwamba kuna changamoto za ukame zinakuja kupitia simu za kiganjani mikononi mwao tusingekuwa na shida ya chakula katika maeneo tofauti tofauti katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, si hivyo tu TEHAMA itasaidia zaidi kutafuta masoko. Kama Serikali itakuwa inasaidia kutafuta masoko dunia halafu wanatuma massage moja tu kwa wakulima fulani labda wa zao la pamba, chai, kahawa na mazao mengine maana yake itasaidia wale wapate taarifa mapema kuliko vile ambavyo kila mkulima mmoja mmoja anajitafutia soko lake pale anapoona yeye inafaa. Kwa hiyo, tukiwekeza katika TEHAMA najua na nina hakika kwamba wakulima wetu hawatakuwa kama walivyo sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mchango wangu huu kidogo, naomba niunge mkono hoja, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. FREDY A. MWAKIBETE: Mheshimiwa Naibu Spika, asante sana kwa kunipa fursa na mimi niweze kuchangia katika hotuba hii ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Kabla ya yote kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa namna ambavyo anafanya maamuzi yaliyo mengi mazuri katika sekta hii ya uchukuzi na mawasiliano. Lakini pia niipongeze Wizara hii pamoja na Waziri, Naibu Mawaziri na watendaji wake wote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto kubwa katika Jimbo la Busokelo ni barabara ambayo imeahidiwa kwa miaka mingi na Marais wote waliopita ukiachana na Baba wa Taifa ambayo ni Katumba – Lwangwa – Mbambo – Tukuyu yenye kilometa 85. Bahati nzuri sana nimeenda mara nyingi kwa Katibu Mkuu na amekuwa akiniahidi mara kwa mara lakini mara nyingi pia nimewasiliana na Waziri, nimepeleka mpaka maandiko lakini hadi hivi leo ninavyozungumza katika bajeti yake hakuna jambo ambalo limefanyika ambalo lilitakiwa lifanyike mwaka jana kwa bajeti ya mwaka 2017/2018. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara hii ni muhimu sana kwa wananchi wetu wa Busokelo na Rungwe kwa sababu kwanza gesi asilia aina ya carbon dioxide inapatikana kule lakini pia kuna aina mbalimbali ya mazao kama ndizi, viazi na maziwa kwa ajili ya ufugaji lakini barabara hii hata hivi ninavyozungumza wiki iliyopita tulikuwa na Mheshimiwa Waziri wa Nishati, tulikwama kwa zaidi ya dakika kadhaa kwa sababu ya barabara hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba Serikali na Wizara hii ichukulie umuhimu mkubwa barabara hii kwa sababu hata Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 28 Agosti, 2015 saa 6.30 pale viwanja vya Tukuyu Mjini aliahidi barabara hii kwamba ataitengeneza kwa kiwango cha lami. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, niombe sana Mheshimiwa Waziri utakapokuja kujibu useme kwamba barabara hii itaanza lini kutengenezwa kwa sababu mwaka huu wa fedha unakwisha na bajeti ilishatengwa hakuna lolote ambalo limefanyika, sielewi ni nini kinachoendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni barabara ya kutoka Luteba (Mbeya) – Makete – Njombe, ni barabara mpya ambayo inaunganisha mikoa yote miwili. Nikiwa Mbunge nimekuwa mbele pamoja na wananchi wangu kulima kwa jembe la mkono. Je, Serikali inatusaidiaje katika barabara hii kuhakikisha kwamba tunaunganisha mikoa yote miwili ya Njombe pamoja Mkoa wa Mbeya kupitia Luteba mpaka Makete. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama Serikali haitakuwa na fedha basi nikuombe Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu wako na Katibu Mkuu twende wote tukalime kwa kushika jembe la mkono kwa sababu ninaona kila mara nikiandika hata maandiko tangu mwaka 2016 bado haya mambo hayaendi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hayo, kuna barabara pia ya mchepuo wa kutoka Uyole kwenda Mbalizi barabara hii ni muhimu sana kwa wananchi wa Mbeya Jiji. Kwa sababu mahali pale katikati ya Jiji kumekuwa na foleni kubwa ukizingatia kwamba ule mji unakua kwa kasi. Kwa hiyo, tunaomba mchepuo wa barabara itakayoanzia Uyole kwenda Mbalizi na Songwe airport iweze kukamilika ili magari makubwa yawe yanapita ile diversion. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna jambo kubwa hili la Uwanja wa Ndege wa Songwe. Bahati nzuri sana Kamati yetu ya PIC tulikwenda kutembelea ule uwanja na kila mara nimemsikia Mheshimiwa Waziri hapa akijibu kwamba tunatengeneza taa za kuongozea ndege. Kwa bahati mbaya sana anasema ni shilingi bilioni nne lakini kwenye bajeti hapa ipo shilingi bilioni 3.7 na hizi fedha hazitatosha kutengeneza taa za kuongozea ndege pamoja na kujenga ukuta na runway, haitawezekana kwa fedha ambazo zipo hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tuiombe Serikali kwamba iweze kutenga fedha za kutosha katika uwanja huu wa kimataifa na ikizingatiwa kuwa katika nchi yetu ya Tanzania kuna viwanja vikubwa vinne ambavyo vinaweza kusaidia viwanja vingine. Zaidi ya viwanja 54 vinahitaji kupata mapato kutoka viwanja vya Julius Kambarage Nyerere, Songwe, KIA na Mwanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwahiyo, ningeishauri Serikali kwamba laiti kama tungeweza kuviwezesha hivi viwanja na vikaweza kukamilika ili fedha zile sasa ziweze kusaidia viwanja vingine ambavyo vipo kwenye mpango wa kutengenezwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine muhimu ni suala la mawasiliano, katika sekta ya mawasiliano inachangia asilimia 13.1 ya pato la Taifa na kwa msingi huo tumeona mara nyingi database zetu ama software ambazo zinatumika katika mawasiliano zinatumia commercial software. Nikiwa mdau wa mawasiliano (TEHAMA) ningeshauri kwamba ianze kutumia open source kama vile Firefox, Fidora, Tomcat, http server na nyinginezo nyingi ili kuipunguzia gharama Serikali wakati wa kuendesha hii mifumo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu open source ni mifumo ambayo inakuwa ni wazi kwa maana kwamba own source code anaweza aka-edit mtu yeyote yule, lakini ukitumia commercial software maana yake unahitaji kununua license na zinakuwa na expiring date na running cost yake inakuwa ni kubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia niweze kuzungumzia suala zima katika suala hilo hilo la mawasiliano tumeona pia katika hii issue ya commercial software kuna baadhi ya pirates software ambazo zinatumika kwenye taasisi za Serikali ambazo hazijalipiwa license na gharama yake ni kubwa sana. Ni kubwa kwa maana kwamba wale ambao wanatengeneza software incase wakijua kwamba taasisi za Serikali zinatumia software ambazo hazina license, Serikali lazima itakuja kulipa fedha nyingi. Kwa hiyo, nitoe tahadhari hiyo kwamba haitakiwi tuingie kulipa huko wakati tungeweza kutumia hizi open source software.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, ninapenda kuunga mkono hoja, lakini nimuombe mheshimiwa Waziri aje na majibu yaliyo sahihi sana juu ya barabara ya kutoka Katumba – Luangwa – Mbambo – Tukuyu na ikibidi barabara ya kwenda Makete kutoka Busokelo twende wote tukalime kwa jembe la mkono kama fedha hazitapatikana hapa, ahsante sana.