Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Hon. Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti ahsante sana kwa kunipa nafasi nami niweze kutoa mchango wangu mbele ya Bunge lako Tukufu. Kwanza nianze kuipongeza Wizara, Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu wake kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nawapongeza Jeshi la Polisi; IGP Sirro pamoja na Makamishna na Makamanda wote katika ncni yetu. Tuko katika kipindi ambacho tunaona kabisa kwamba kuna transformation kubwa imefanyika. Matukio mengi tuliyozoea kuyaona hata katika ajali, lakini pia uhalifu kwa maana ya wizi katika mabenki, lakini pia ujambazi wa kutumia silaha, kwa kweli yamepungua kwa kiasi kikubwa sana. Sasa hatuwezi tukabeza hizi jitihada pamoja na kwamba changamoto zipo na sitarajii sisi kama viongozi tuamini kwamba changamoto zitakwisha kwa wakati mmoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunawapongeza na tunawaomba waongeze weledi katika kushughulikia matatizo mbalimbali hasa kwa maana ya kwamba sasa hivi kutokana na ukuaji wa teknolojia, uhalifu nao unakua. Tukisema tunajiunga katika kanda na uhalifu na wenyewe pia wanajiunga, wana kanda zao; tukisema tuko katika block fulani na wenyewe pia uhalifu unazidi kuongezeka. Kwa hiyo, tuhakikishe kwamba tunakuwa na jeshi lenye weledi na kuhakikisha kwamba mambo yanakwenda vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na suala la kushauri kwa sababu ndiyo kazi yetu ya msingi kama Wabunge, kushauri na kuisimamia Serikali. Katika eneo la ushauri nianze na Jeshi la Zimamoto. Jeshi la Zimamoto bado liko karne nyuma zaidi ya karne tuliyokuwanayo. Bado vifaa wanavyotumia kuzima moto haviendani na teknolojia ilivyokua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona sasa hivi tunayo majengo marefu sana hasa katika Majiji; Jiji la Dar es Salaam, Mwanza na Arusha ambako kuna majengo marefu, lakini utashangaa bado Zimamoto wana magari ambayo hayawezi kuzima moto hata ambao uko ghorofa ya pili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nitoe rai kwamba kikosi hiki cha Zimamoto kiboreshwe, kiwe na vifaa vya kisasa ambavyo vinaendana na wakati tulionao. Pia, katika Jiji kama la Dar es Salaam ambalo linazidi kupanuka, hatutarajii kuwaona Zimamoto bado wakiwa pale pale walipokuwa tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunatarajia kuwaona Zimamoto wakiwa na vituo labda maeneo kama Mbezi, Mbagala, Kigamboni, Bunju na maeneo mbalimbali ambayo hata ikihitajika huduma ile gari linafika kwa wakati. Sasa hivi bado wako maeneo yale ya kule Mjini Ilala ambapo hata akiitwa kuzima moto Mbagala, anatumia hata saa mbili kufika huko na hiyo tija haiwezi ikaonekana. Kwa hiyo, suala la msingi kwanza tuboreshe hii huduma kwa maana ya kuwapa vifaa vinavyoendana na wakati, lakini pia wajaribu ku-decentralize hii huduma kuelekea huko ambako makazi ya watu yapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni la breakdown. Unapopata ajali katika Jiji la Dar es Salaam wanatumia breakdown, hizi Land Rover za zamani. Zile Land Rover sidhani kwamba hata zinalipa kodi kwa maana ile ni biashara, lakini sidhani kama wako katika mfumo rasmi kwamba wanalipa hata mapato ya Serikali. Kwa sababu umbali ambao hauzidi kilometa moja wanachukua Sh.80,000/= kuvuta gari ambalo limeharibika ama lime-park eneo ambalo haistahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wasiwasi wangu hapa ni kwamba je, kwa vijana hawa tuliokuwa nao kama Mawaziri, Mheshimiwa Mwigulu, Mheshimiwa Engineer Masauni, bado Taifa hili tuna haja ya kuwa na breakdown aina ya Land Rover zile kweli? Yaani Land Rover ile ikaanze kuvuta BMW ya shilingi milioni 200 inavutwa na gari ambalo thamani yake haifiki hata milioni 12?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani hapa kuna tatizo. Lazima tuje na ubunifu kwa sababu hii wanaifanya kama biashara. Basi tujaribu kuitangaza hii biashara watu wenye uwezo watuletee breakdown za kisasa ambazo unapakia gari juu ya gari. Hili tuliangalie kwa makini sana. Breakdown hizi, zenyewe zinaharibu hayo magari wakati wa kuyapakia au wakati wa kuyavuta. Wanatumia minyororo ambayo ni teknolojia ya zamani sana kiasi kwamba utakapoona lile gari linavyovutwa, japokuwa wewe ni binadamu, lakini unaumia kwamba hapa kitu kinachofanyika siyo sawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba na eneo hilo waliangalie, wao ni vijana lazima walete ubunifu kwenye hii Wizara. Tumeona Mheshimiwa Augustine Mrema aliwahi kukaa kwenye Wizara hii na akatengeneza jina, nao tunatarajia wafanye vitu ambavyo vinaonekana ili viweze kuwatangaza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine, nizungumzie suala la Gereza la Kilimo, Mnaro. Nimeshamwambia Mheshimiwa Waziri mara kadhaa kwamba Gereza hili ni miongoni mwa Magereza machache ya kilimo katika nchi hii na kule kuna scheme za umwagiliaji, lakini Gereza hili ni chakavu kwa sababu ni la siku nyingi mno.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza nadhani mwaka 1973 ndiyo Gereza hili limejengwa. Kwa hiyo, wanahitaji kuboresha miundombinu ya Gereza. Pia, nimewahi kumwambia Mheshimiwa Waziri kwamba ikama ya wafungwa pale ni ndogo. Hili ni Gereza la Kilimo, tunahitaji tuone wanalima. Tunahitaji tuone wanazalisha; ni kilimo na ufugaji unaendelea pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Gereza lina uwezo wa kuchukua wafungwa mpaka 100, lakini walioko pale ni wafungwa 38. Siku moja Mheshimiwa Matiko hapa alisema kuna msongamano Gereza la Tarime, Rorya, nikamwambia sasa si awahamishie kule watusaidie kwenye shughuli za kilimo Lushoto? Hii iwe tu wazi kwamba kwa nini wafungwa ni wachache, ni kwa sababu watu wa Lushoto sio watu wa matukio. Kwa hiyo, ndiyo maana kule Magerezani huwezi hata kuwakuta Wasambaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni Kituo cha Polisi cha Mlalo. Kuna wakati kulitokea suala hili la ugaidi katika maeneo ya Mapango ya Amboni na wale watu walifika katika Milima ya Usambara. Kituo cha Polisi Mlalo kilikuwa hakijajenga amari, kwa hiyo, hatukuwa na sehemu ya kuhifadhia silaha. Sasa tumeshajenga tunaomba kikaguliwe...

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)