Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii

Hon. Rev. Peter Simon Msigwa

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Iringa Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa bahati nzuri nikiwa kama Waziri Kivuli nimefanya kazi na Mawaziri wanne. Nimefanya kazi na Mheshimiwa Maige na huyu ni Waziri wa nne. Nakumbuka mara ya mwisho nilivyochangia hotuba hii nilikuwa nimetoa ushauri kidogo kuhusiana na Wizara hii hasa Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla alipoingia kwa mara ya kwanza. Napoanza nina maswali machache sana ambayo ningeomba Waziri ayajibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, Waziri alipochukua tu Wizara alituhumu watu kwamba walikuwa wanachukua fedha kwenye Kampuni ya OBC, kwenye migogoro ya Loliondo na kwamba yeye hapokei rushwa. Hata hivyo, hivi karibuni nimeona Wizara yake imepokea magari, nilitaka kujua yeye amepokea shilingi ngapi maana alisema wataondoka mwaka huu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili, Waziri alinituhumu na mimi mwenyewe kwamba mimi pamoja na Nyalandu ni mafisadi. Pia alisema katika Bunge hili ataleta hizo taarifa za ufisadi, ningeomba aziweke hapa maana tusiharibiane majina bila sababu ili anavyoongoza Wizara yake tuwe vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii naamini Mheshimiwa Rais alipompa Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla ambaye ni kijana na Bunge lililopita tulikuwa naye, aliona misukosuko mingi ambayo Wizara hii imepitia. Mheshimiwa Zakia Meghji ndiye pekee aliyekaa katika Wizara hii kwa muda mrefu wa miaka tisa, Mawaziri wengine wote wamekuwa wanakaa miaka mitatu, miwili au mmoja wanaondoka. Nilitegemea Waziri atamsaidia vizuri sana Rais lakini kwa bahati mbaya baada ya kuingia ofisini kumetokea migongano mingi sana ndani ya Wizara hii ambayo ni uhai wa Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachonisumbua, katika Kamati yetu ambapo mimi ni Mjumbe wa Kamati hii tumezungumza matamko ambayo umeyatoa hasa katika sekta ya uwindaji ambayo yameathiri sana sekta hii. Katika vile vitalu vya uwindaji ambapo 18 vimeondoka na sasa hivi ni zaidi ya vitalu 81 viko wazi. Ukiangalia toka vitalu hivi vimegawiwa tasnia hii imekuwa ikichangia pesa nyingi katika Taifa letu. Kwa matamko yako Waziri umeondoa confidence ya wawekezaji jambo ambalo lina athari kwa sababu Serikali haina pesa za kutosha za kutunza mazingira katika vitalu hivi. Serikali haiwezi kutengeneza barabara za kwenye vitalu, haina uwezo wa kuzia anti-poaching ambapo katika Awamu ya Nne baadhi ya Mawaziri nikimchanganya Mheshimiwa Kagasheki na Mheshimiwa Nyalandu walifanya kazi kubwa sana kuleta wafadhili kuzuia anti-poaching katika nchi hii. Matamko ya Waziri yamesababisha hawa watu waondoke na yanaleta tabu katika mapori hayo na kusababisha mapori yale yaingiliwe na watu wengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka kujua kuna mkakati gani wa makusudi wa kushughulikia matamko haya ambayo yalikuwa hayana uangalifu na yametuletea hasara katika tasnia hii? Waziri kijana ambaye tunategemea awe visionary atuambie hapa ana mipango gani zaidi kuliko matamko aliyoyatoa? Hilo ni suala la kwanza ambalo lazima liangaliwe vinginevyo kama Kamati ilivyosema tunaua tasnia hii.

Mheshimiwa Mwwenyekiti, jambo lingine ambalo nataka kuzungumza ni hawa wasafirishaji wa nyama. Takwimu ninazo hapa zinaonesha jinsi ambavyo Serikali inatumia pesa nyingi sana kwa mfano kuwaua ndege. Kila mwaka Wizara ya Kilimo huwa inaua ndege zaidi ya milioni 70, hawa kweleakwelea. Hawa watu huwa wanasafirisha ngedere na tumbili wanawapeleka huko nje. Nililalamika kwenye Wizara hii mpaka mtendaji mmoja mzuri sana katika Wizara alikuwa anaitwa Mulokozi aliwekwa ndani kimakosa mpaka akafariki, kuoneaonea watu tu kwa makosa ambayo hawakufanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri amezungumza kwenye hotuba yake, time frame itakuwa lini ili hawa watu walipwe pesa zao kwa sababu wanaishi katika mazingira magumu. Hawaachi kuja hapa Bungeni kutaka wasaidiwe kwa sababu kwa kweli tumewa-cripple na Serikali haipo kwa ajili ya ku-cripple watu, hawa watu wa TWEA naomba hili suala lao liangaliwe kwa mapana kwa sababu kwa kweli wanapata tabu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo nataka nizungumze katika Wizara hii ni matangazo. TANAPA pamoja na Ngorongoro wamekuwa wakifanya kazi kubwa sana lakini Serikali imechukua kodi za matangazo ikapeleka Serikali Kuu ikayatoa kwenye maeneo yake, that is fine. Hata hivyo, Serikali hii imeamrisha, kwa mfano, ule utalii wa fukwe uende ukawe chini ya Wizara ya Mifugo, Mheshimiwa Mpina ana matatizo mengi sana ambayo hawezi kuyabeba hapa, Wizara hiyo haiwezi kutatua matatizo ya mifugo na uvuvi lakini bado Wizara imepelekewa kwamba ndiyo washughulike na utalii wa fukwe. Ningeshauri Serikali, ule utalii wa fukwe urudi tena kama ulivyokuwa kwenye TANAPA na Wizara badala ya kupeleka kwenye Mifugo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kibaya zaidi kwenye masuala ya matangazo, Serikali imekuwa ikichukua matangazo na tuna-encourage TANAPA wafanye utalii wa ndani, watangaze zaidi, TANAPA wakijaribu kuweka mabango nchi nzima ili wa-encourage Watanzania waende kuangalia maeneo ya utalii utakuta bango moja la TANAPA lina-cost karibu shilingi milioni 4 kwa mwaka, kwa hiyo unakuta kwamba TANAPA au Ngorongoro hawawezi kulipia matangazo kama hayo. Kwa hiyo, ningeishauri Serikali iliangalie kwa umakini suala hilo kwamba watoe hizo tozo katika maeneo kama hayo kwa sababu tunataka tuingize pesa na tu-encourage utalii wa ndani ili uchumi uweze kukua. Naomba hilo liangaliwe kwa ndani sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa masikitiko makubwa naona Serikali imeamua kwa nguvu zote mradi wa Stiegler’s Gorge. Mradi wa Stiegler’s Gorge, ukiiangalia Selou, Selou is the one of the world heritage, ni urithi wa dunia, ni moja ya identity ya nchi yetu, huwezi kupata mahali pengine pazuri kama Selou. Hata hivyo, Serikali imeamua na inataka kwa nguvu zote, mpaka sasa hivi tumeomba Environmental Impact Assessment hapa tuoneshwe ni madhara gani yatapatikana lakini haya mambo hayajaletwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini taarifa tulizonazo ni kwamba mradi unasukumwa kwa nguvu na miti inataka kukatwa kule, tunataka tuharibu maeneo yale. Miti milioni tatu inataka iangushwe na wataalam wanasema maeneo yale ni mahali ambapo wanyama wanazalia, Wizara inasema nini kuhusiana na suala hilo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Selou ni kitambulisho cha nchi. Mara ya mwisho tulikwenda kule Urusi kwenye mkutano wanaisifu Selou inaitambulisha nchi yetu. Tutakapoweka hilo Bwawa faida yake ni ipi? Naunga mkono juhudi zinazofanywa kuwekeza utalii upande wa Kusini na Word Bank wanasema kama tukiwekeza vizuri Southern Circuit mapato tutakayoyapata ni dola karibu bilioni 16 ambazo zitatusaidia
kuongeza kipato katika nchi. Hili bwawa ukilitengeneza ambapo halitaanza kuzalisha mpaka baada ya miaka saba, mapato yake tutakayopata ni karibu bilioni 2 tukiuza umeme na kama tukipata wateja lakini ukiangalia nchi jirani zote, Malawi, Mozambique na Zambia nao wanatengeneza umeme wao, tutauza wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya ni mambo ambayo kama Taifa lazima tufikiri kwa pamoja, tusiende kwa kukurupuka. Nina wasiwasi kwamba kwa mara ya kwanza CCM mmeshindwa kuidhibiti Serikali, mmedhibitiwa na Serikali. Chama cha Mapinduzi mmeshindwa kuidhibiti Serikali kwa sababu mna wajibu wa kukaa kwenye vikao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Kagasheki aliondoka hapa kwa Operesheni Tokomeza. Kuna watu waliuawa, walipigwa, walilazimishwa kufanya tendo la sex mbele ya watu, tulipiga kelele humu Bungeni akiwemo Mheshimiwa Pinda kama Waziri Mkuu hapa. Nilitegemea Waziri na Wizara hii itakuwa imejifunza na kuacha kuonea watu. Serikali inaoneaonea watu, inapigapiga watu hovyo, wapo wengine wanakufa, nilitegemea Wizara hii watakuwa wamejifunza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yanayozungumzwa sasa hivi, haya mambo ya vigingi, watu wanavyoonewa ina maana wakati ule wa Mheshimiwa Kagasheki hatukujifunza, hatukuwa na somo kwa sababu tunafanya yaleyale. Uendawazimu ni kufanya jambo lile lile, kwa njia ile ile halafu unategemea matokeo tofauti, huo ndiyo uendawazimu, hii ni simple definition ya uendawazimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Bunge tumezungumza sana suala hili, Serikali haipo kwa ajili ya kuonea watu, watu wanaonewa katika nchi yao wenyewe, wamejikuta wamezaliwa katika maeneo hayo, kwa nini hatuna njia ya kudumu ya kutatua matatizo? Mojawapo ni tatizo la Loliondo, nako kumekuwa na matatizo nenda, rudi. Waziri alikuja hapa kwa gear kubwa kwamba atatatua tatizo la Loliondo limefikia wapi mpaka leo? Juzi Waziri ulikwenda kupokea magari tena kule kule ulikosema watu wanapokeaga rushwa, wewe umepokea shilingi ngapi? Tuambie uko hapa tunakuona, umepokea shilingi ngapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanyama wameuawa, hawa askari tunawapenda sana wanalinda mapori lakini sasa tunawaona kwenye mapori ya akiba wana-shoot wanyama wa watu ambao ndiyo urithi na utajiri wao. Kwa kodi za wananchi zile risasi zimenunuliwa, wanawapiga bunduki ng’ombe kwa kodi ya wananchi. Yaani mtu analenga ng’ombe anasema piga hilo, lenga hilo, uchumi wa wananchi, hatuwezi kukubaliana na mambo haya. Wananchi wanavuliwa nguo katika nchi hii, nchi ambayo tumepata uhuru halafu tuseme hapa business as usual, hatuwezi kukubaliana. Haya ni mambo ambayo Waziri lazima atoe majibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hotuba ya Waziri sijaona mikakati yoyote, mnakimbilia mnasema mmenunua ndege, mlikuwa mnawaiga Rwanda sasa hivi ndege zinaporomoka. Wataalam wanasema hata Emirates ku-break even iliwachukua miaka 20. Hatukatai kununua ndege lakini hiyo shilingi trilioni 1 ambayo imewekezwa huko ingeweza kufanya vitu vya msingi halafu secondary itajichukulia yenyewe, tunafanya mambo kwa mihemko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshauri Mheshimiwa Waziri, sasa hivi naona kama kidogo ametulia, akae ajifunze Wizara vizuri, Wizara ina mambo mengi. Sasa hivi ametulia kidogo, Wizara ina mambo mengi na ni Wizara tunayoitegemea iinue uchumi katika nchi yetu.