Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Hon. Eng. Joel Makanyaga Mwaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chilonwa

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

MHE. JOEL M. MAKANYAGA: Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi nashukuru sana kunipa nafasi hii ya kuchangia katika Wizara hii ya Afya, na mimi nianze kwa kuwapongeza sana Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri na watendaji wote wa Wizara ya Afya kwa kazi nzuri na kubwa wanayoifanya, tumeona hata katika uwasilishaji wa bajeti yao hotuba yao ilivyosheheni mambo yaliyo ya muhimu sana kwa wananchi wa Watanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nijikite kwanza kabisa kusema Watanzania tunayo kazi kubwa sana mbele yetu, kazi hii tumedhamiria kwamba tuondoke hapa tulipo kwenye ulimwengu wa tatu, nchi maskini, tuingie angalau kwenye nchi yenye uchumi wa kati. Ili tuweze kufanikiwa katika hili kama afya zetu zitakuwa mgogoro hatutaweza kufika huko salama, tutakuwa tunasuasua sana na itatuchukua miaka mingi kufika kwenye nchi ya uchumi wa kati. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pili nichukue nafsi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu katika maadhimisho ya siku ya usafi wa mazingira na ujenzi wa vyoo bora kimkoa Dodoma yalifanyika katika Kata ya Aneti kijiji cha Umekwa katika Jimbo langu la Chilonwa. Namshukuru sana kwamba alishiriki pamoja na kushiriki aliweza kutoa ahadi mbalimbali kwamba atasaidia kumalizia ujenzi wa chumba cha upasuaji pale kwenye Kituo cha Afya cha Aneti nakushukuru sana Mheshimiwa Ummy kwa kazi hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile aliahidi kutupatia madaktari katika Zahanati za Aneti, Chinene pamoja Umekwa katika Kata hiyo ya Aneti. Kama vile haitoshi kwa sababu ya speed kali tunayokwenda nayo hadi sasa tunavyoongea katika kijiji cha Aneti tayari tumeshapewa daktari mmoja, tunakushukuru sana Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia uliahidi kuipatia shule ya msingi Umekwa shilingi 400,000 kwa ajili ujenzi wa vyoo bora pale shuleni, nashukuru sana kwa haya mambo mazito unayotufanyia. Nisimalize bila kukushukuru sana wewe pamoja na Wizara yako kwa kutuangalia Chamwino kwa jicho la huruma sana kwamba ulitupatia fedha kwa ya ajili ya kuboresha pale kituo cha afya cha Chamwino shilingi milioni 500, lakini pia ukatupatia fedha kwa ajili ya kuboresha zahanati ya Mpunguzi shilingi milioni 700 na juzi pia umetupatia tena fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Chamwino shilingi bilioni 1.5, tunakushukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa nimalize kwa kukuomba Mheshimiwa Waziri tuna mahitaji mengi sana ya afya katika Jimbo la Chilonwa, nakuomba sana uliangalie kwa huruma sana kijiji cha Kwahemu ambapo wananchi wameanza ujenzi wa zahanati, lakini wamefika njiani tukisaidiana wote pamoja na Mbunge, Diwani na nani tunasuasua, tunaomba sana utuangalie pale kama unaweza kutusaidia angalau tuweze kumalizia ile zahanati, kijiji hicho kiko ndani sana, kiasi kwamba kusafiri toka pale kwenda Aneti inakuwa shida sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hayo machache nashukuru sana, naomba kuunga mkono hoja. Ahsante.