Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.

Hon. Lucy Fidelis Owenya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia nafasi ya kuchangia. Nianze na migogoro ya ardhi katika maeneo ya Hifadhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwepo na malalamiko mengi ya mipaka kati ya hifadhi na wananchi na wafugaji kuingiza mifugo kwenye hifadhi. Hii huchangia maambukizi ya magonjwa kwa wanyama na kusababisha wafugaji na walinzi wa wanyamapori na hifadhi kugombana na wafugaji, kuanza kuua wanyama kama samba na kadhalika. Ni vizuri kabisa katika bajeti ya mwaka huu zikatengwa fedha kwa ajili ya kuweka mipaka katika hifadhi zetu ili kumaliza migogoro iliyopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee suala la uwindaji wa kitalii. Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii alitangaza kufuta leseni zote za uwindaji wa kitalii, jambo ambalo limeleta mtafaruku mkubwa katika sekta hii. Ijulikane kwamba katika utalii huu mwekezaji anatumia fedha nyingi sana kuandaa miundombinu ya uwindaji; na watalii wa uwindaji wanafanya booking zao hata miaka miwili kabla na wanalipa mapema (advance payment). Sasa leo hii ukikatisha ghafla siyo kuua kabisa utalii?

Mheshimiwa Mwenyekiti, wadau wengi wameshindwa kwenda kufanya maonesho/matangazo yaliyokuwa yafanyike mwakani, lakini mpaka sasa hivi hawana uhakika na biashara zao. Pengine Serikali ina nia njema ya kufanya mnada katika kuuza vitalu vya uwindaji, lakini lazima kufidia wale waliopo; wameshatumia kiasi gani kuendeleza vitalu? Tayari wana booking kiasi gani? Wamekata mingapi kwa miaka mingi? Bila kufanya hivyo, tutapoteza fedha nyingi sana ukizingatia sekta hii huchangia zaidi ya asilimia 17 ya pato la Taifa na huchangia kwa kiasi kikubwa kupata fedha za kigeni. Kwa sasa mapato yameshuka kutoka shilingi milioni 23.58 mwaka 2010 hadi shilingi milioni 11.28 mwaka 2015. Hii ni hatari kwa sekta hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu imejaliwa vivutio vingi sana ambavyo vingine havipatikani sehemu nyingine. Mfano, mbuga ya Saadan, bado hazijafanyika juhudi za kutosha kuendeleza kivutio hiki ambacho wanyama wanaenda mpaka baharini. Miundombinu ya barabara siyo mizuri, bado hawajashirikisha sekta binafsi ili waweze kujenga hoteli za kitalii ili kuwavutia watalii wengi zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna haja ya kuiwezesha Bodi ya Utalii ili iweze kutangaza vivutio vyetu, siyo nje ya nchi tu, hata kwa utalii wa ndani bado mwamko ni mdogo kwa wazawa kutembelea mbuga zetu. Nashauri watangaze program ya kutembelea shule na kuwahimiza kutembelea mbuga zetu, yaweza ikawa njia moja ya kupata wazawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado TANAPA haijatangaza Hifadhi ya Mkomazi ipasavyo kwa sababu hii ingeweza kutumika kama day trip kwa watalii wanaokuja kupanda Mlima Kilimanjaro. Wakiwa na siku moja ya ziada wanaweza kutembelea hifadhi hiyo na kuongeza pato la Taifa.