Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Hon. Hafidh Ali Tahir

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dimani

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

MHE. HAFIDH ALI TAHIR: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Pili, niwashukuru sana wananchi wangu wa Jimbo la Dimani kwa kunipa nafasi ya kuja tena katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya yale yaliyotokea mwaka 2010.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze na suala la Katiba ya Zanzibar Kifungu 72. Kifungu cha 72 kinazungumzia suala la Uchaguzi na Mahakama, lakini mimi niende katika kifungu cha 9 cha Katiba hiyo ya Zanzibar, Kifungu cha 13 ukiachia hicho cha 9 kinasema kama ifuatavyo naomba ninukuu:
“Hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.” (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachozungumziwa hapa ni amri ya Tume ya Uchaguzi ambayo hakuna Mahakama hata moja duniani itakayoweza kuingilia maamuzi ya Tume ya Uchaguzi. Sasa tunapofika wakati tukazungumzia mambo tusizungumze mambo nusu nusu, tutafute kipengele kinachohusika na nani kinachomhusu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine, kwa sababu nimetanguliza hili, nitakuwa sikufanya haki kama sikuwapongeza Marais wawili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nawapongeza kwa kitendo kimoja ambacho kimefanana. Mheshimiwa Magufuli katika sherehe za Mei day alitoa punguzo la kodi kwa wafanyakazi, nampongeza sana kwa hili. Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein ameongeza mshahara kutoka sh. 150,000 kima cha chini na sasa kitakuwa sh. 300,000. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nini maana yake? Maana yake Viongozi hawa wawili ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanawathamini Watanzania, wanawathamini wafanyakazi na wanataka waendelee katika shughuli zao mbalimbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo limekuwa likizungumzwa sana hapa ni suala zima la Uchaguzi ambalo bado linaendelea kuzungumzwa sehemu mbalimbali. Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nae amekuwa akiandamwa sana katika sehemu mbalimbali. Ukienda kwenye kifungu cha 9(2) kinasema kwamba:
“Kwa madhumuni ya utekelezaji wa majukumu yake, Tume ya Uchaguzi itakuwa ni Idara inayojitegemea na Mtendaji Mkuu wake atakuwa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye atateuliwa na kufanya kazi kwa mujibu wa masharti ya sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi”. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi amechaguliwa na Rais kwa mujibu wa Baraza la Wawakilishi, sasa hakuna mtu mwingine wa kuingia akasema labda kuna jambo lingine litakaloweza kufanyika. Kama hiyo haitoshi, kuna suala zima la uhuru wa Tume nalo limechukua nafasi yake. Hata hivyo, baada ya yaliyotokea katika uchaguzi na kurudiwa tarehe 20 ninachotaka kukisema hapa lazima Wazanzibari na hapa mimi nilipoita Wazanzibari, wale wa upande wa pili huwa wanasema wale CUF ndiyo Wazanzibari. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachotaka, Uzanzibari una maana yake. Uzanzibari siyo kabila, wala hakuna mtu aliyechimbuka kwenye shimo akaitwa Mzanzibari. Zanzibar ni Cosmopolitan Country, hakuna mtu anayeweza kusema mimi Mzanzibari; sote tumekuja pale, narudia tena, hakuna mtu aliyechimbuka Zanzibar. Kuna watu wamekuja kwa ngalawa, kuna watu wamekuja kwa majahazi na hao waliotoka huko wanakotaka wao, Dubai au wapi wamewakuta watu wameshafika Zanzibar. (Makofi)
Huwezi ukajiita Mzanzibari wakati unakwenda katika kisiwa kile unawakuta watu! Huwezi ukajiita Mzanzibari kwa sababu tu kuna Mfalme mmoja alitoka alikotoka akaenda akatawala watu ukawa wewe ndiyo Mzanzibari, kwa sababu umezaliwa na asili ya Kifalme, hujiiti Mzanzibari! Wazanzibari ni wale watu ambao wamekwenda pale, wakakikuta kisiwa kile, wakakianzisha na wengine wakafuata! Wale ndiyo Wazanzibari! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, iweje leo anasimama mtu anasema Wazanzibari wamesema! Akina nani Wazanzibari? Wako wapi? Jamshid! Jamshid siyo Mzanzibari pale. Pana watu pale Wazanzibari, Wazaramo, wako pale watu waliotoka sehemu mbalimbali, Wandengereko, ndiyo waliotoa kile kisiwa cha Zanzibar. Wazanzibari wale wanaojiita Wazanzibari wale uliowakuta walikuwa wana maneno yao wanaita machogo. Mmewakuta hawa hata wakiwa machogo! Wamewakaribisha, hamuwezi mkafanya vinginevyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nataka kulisema ni kwamba, tumemaliza uchaguzi juzi, nampongeza sana Katibu Mkuu wa CUF kwa sababu ni mtu anaependa ukubwa. Nampongeza kwa sababu amefika mahali akawafanya hao wanaojiita Wazanzibari waondoe Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Wameunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Katibu Mkuu na mwenzie maana hawa wote jora moja, aliyekuwa Rais wakati ule Mheshimiwa Aman, mtoto wa Mama Fatma ndiyo waliokaa na Seif Sharrif wakapanga suala la Umoja wa Kitaifa. Ninachotaka kusema hii ndiyo style yake Katibu Mkuu wa CUF na wale wafuasi wake wanaogopa kumwambia kitu, hawathubutu kusema jambo! Katika mikutano yote aliyofanya na Viongozi wa nchi hii wanashindwa kusema kwa nini anakwenda peke yake. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe mfano, Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif ameshakutana na Mheshimiwa Aman mara tatu, kaenda peke yake, Mheshimiwa Seif kakutana na Rais Magufuli kwa tatizo la uchaguzi alienda peke yake, Mheshimiwa Seif Sharrif kakutana na viongozi wengine waliokwenda, kaenda peke yake, kwa nini hawasemi wewe unakwenda peke yako hutuchukui? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushahidi Mheshimiwa Maalim Seif, kakutana na Mwalimu Nyerere limezungumzwa jambo, halijajulikana mpaka leo! Hajawaambia hawa! Hawaulizi! Waulize basi kasema nini Mwalimu? Waulize basi kasema nini Mheshimiwa Amani? Wanashindwa, hawasemi!Kwa sababu gani? Kwa sababu ni mtu ambaye…
MHE. HAFIDH ALI TAHIR: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ni mtu ambaye anapenda ukubwa bila kuwashirikisha wenzie!
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni kwamba, tumekwenda kwenye uchaguzi na wenzetu wanasema kwenye risala iliyotolewa hapa ya upande wa Upinzani, wanasema wameingia kwenye uchaguzi mara 5…
MWENYEKITI: Asante! Tunaendelea!