Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 - Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa

Hon. Augustino Manyanda Masele

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbogwe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 - Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Baada ya kuunga mkono hotuba hiyo, napenda kulipongeza Jeshi letu kwa kazi kubwa linazofanya katika kulinda usalama wa mipaka yetu na kujishughulisha na shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa letu na kushiriki katika kukabiliana na majanga mbalimbali yanayolikumba Taifa letu kwa nyakati mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kwa Serikali ni kuwa Serikali iongeze bajeti kwa Wizara hii ili kuziwezesha taasisi ndani ya Wizara hii za Nyumbu na Mzinga ili zijikite kikamilifu katika shughuli za utafiti wa kisayansi na ugunduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, historia inaonesha dhahiri kuwa taasisi za ulinzi na usalama hasa Majeshi ya Ulinzi katika nchi mbalimbali duniani zimeshiriki kikamifu katika kuleta mapinduzi ya viwanda na zana za kivita. Mfano, mifumo ya computer ilibuniwa na Jeshi la Marekani kabla ya kuingizwa katika shughuli za kiraia. Ugunduzi na ubunifu wa vifaa vya kivita kama vile vifaru, ndege za kivita, meli za kivita, makombora ya masafa mafupi, ya kati na marefu yote ni matokeo ya shughuli za kijeshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine napenda kuishauri kulitumia vema Jeshi la Wananchi katika harakati za uvuvi wa bahari kuu (deep sea fishing) ili meli za kivita ambazo zinakaa muda mrefu bila kufanya kazi, zitumike katika kukuza uchumi wa Taifa letu wakati huu amani ikitamalaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naishauri Serikali kulitumia vizuri Jeshi la Kujenga Taifa kwa kulipatia zana za kisasa za uzalishaji mali, yakiwemo matrekta ili kuzalisha mazao ya chakula na biashara kama vile kahawa, mahindi na mpunga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nashauri JKT iwezeshwe kuwa chimbuko la ufugaji bora wa ngā€˜ombe wa nyama na maziwa. Ni imani yangu kuwa Serikali ikiliwezesha Jeshi letu wakati huu, upo uwezekano mkubwa wa kuwa mchangiaji mkubwa katika shughuli za ukuzaji uchumi kama majeshi ya nchi nyingine yanavyofanya, mfano, Ethiopia hapa Barani Afrika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.