Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

Hon. Lucy Fidelis Owenya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kupata nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ugonjwa wa saratani kwa sasa hivi katika dunia ni ugonjwa hatari sana pamoja na saratani ya shingo ya kizazi imekuwa ni tishio. Zaidi ya wanawake 274,000 duniani wanafariki kwa ugonjwa huu na Tanzania ikiwa ni mojawapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru hospitali ya Ocean Road imekuwa ikitoa huduma ya mionzi na kusaidia wagonjwa wa saratani lakini hospitali ile wote tunashuhudia imezidiwa na wagonjwa ni wengi. Nashukuru hospitali ya rufaa KCMC ilipata wafadhili na wakafadhili jengo kwa ajili ya unit ya kansa, walijenga kwa shilingi bilioni 1.2 na wafadhili kwa sasa hivi wako tayari kununua vifaa kwa ajili ya mionzi, kutoa vifaa zaidi ya shilingi bilioni sita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri, kwenye kitabu cha maendeleo umetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya KCMC, jengo ambalo ni special kwa kitaalam linaitwa banker linahitajika kwa ajili ya kuweka vile vifaa vya mionzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, KCMC tunachoomba, Serikali itusaidie wanahitaji shilingi bilioni saba. Tunamwomba Waziri wa Fedha na Kamati yako ya Bajeti mkae chini muangalie ni kwa jinsi gani mnaweza mkaipatia KCMC hizi shilingi bilioni saba ili waweze kujenga lile jengo. Kwa sababu, Kanda ya Kaskazini itapunguza msongamano katika Hospitali ya Ocean Road, inaweza ika-save zaidi watu milioni 15 na kwa kiasi kikubwa tunaweza tukapunguza ugonjwa wa saratani ya kizazi kwa wanawake na kutoa huduma ya mionzi pale KCMC.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie kidogo magonjwa yasiyoambukiza (non-communicable disease). Nimekuwa nikiongea mara nyingi hapa, ninamshukuru Mheshimiwa Waziri amesema wameanzisha watu kwenda mazoezi na kadhalika, nafikiri ni vizuri sasa Wizara hizi zikashirikiana Wizara ya Miundombinu na Michezo ili muweze kujenga pavement kwa ajili ya watu kutembea kwa miguu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia pale Dar es Salaam kwa mfano, zile njia ya majitaka (sewage system) mnaweza mkazifunika na watu wakaweza kupita kwa miguu. Nchi zilizoendelea kwa sasa hivi wanahimiza watu waende kazini kwa kutumia baiskeli, kwa sehemu kama Dar es Salaam mtu atatembeaje na baiskeli? Kutembea tu kwa miguu unagongwa na bodaboda. Kwa hiyo, ni vizuri Serikali mkashirikiana kwa pamoja mkatengeneza pavement kwa ajili ya watu wa kutembea kwa miguu na kwa kiasi kikubwa sana tutapunguza magonja ya kisukari ambayo inasemekana Tanzania watu zaidi ya asilimia tisa wana ugonjwa wa kisukari mpaka watoto wadogo wana wanapata kisukari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi zilizoendelea wameacha kabisa ku-serve hivi vyakula vya junk food, lakini sasa hivi ndiyo vimeanza kuletwa Tanzania kama Kentucky, Fried Chicken na kadhalika. Ni vizuri mkazidi kutupa elimu ili watu waachane na hivyo vyakula ambavyo vinaongeza magonjwa ya shinikizo la damu ya kupanda na kushuka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kidogo nizungumzie mimba za utotoni. Mimba za utotoni imekuwa ni hatari kwa kweli. Pamoja na kusema watoto wadogo wanaweza kuolewa chini ya miaka 18 mimi napinga jambo hili, kwa sababu kwanza tunawakosesha watoto wale elimu, pili mtoto wa kike akijifungua kabla ya umri wake anaweza akapata magonjwa kama ya fistula, tatu anaweza kushindwa kujifungua inabidi atumie scissor na wengine baada ya hapo wanakuwa ni single parent, unakuta wazazi wenyewe wakati mwingine wana wanyanyapaa wanawaambia hukusoma, kwa hiyo watoto wale wanaishia kuwa watoto wa mtaani, wanashindwa kuendelea na masomo, wanaweza kwenda kuwa machangudoa na hii ni kumrudisha mtoto wa kike nyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna moja au nyingine naomba Wabunge tukubaliane na hili, tuliona wenyewe juzi tulivyoongelea suala hili, Sheria ile ya Ndoa ya mwaka 1971 ibadilishwe wengine walikuwa wanapinga kutokana na imani zao za dini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja ya Upinzani naomba muichukue na muifanyie kazi kwa sababu ina ushauri wa kutokasha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.