Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Hon. Lucy Fidelis Owenya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kupata nafasi ya kuchangia. Barabara ya Morogoro kuanzia Mlandizi mpaka Chalinze; barabara hii imekuwa ikikarabatiwa mara kwa mara, lakini bado barabara hii haipo katika kiwango chake kwa kisingizio kwamba water table ipo juu, ni kwa nini wataalam wasifanye utafiti na kuijenga kwa kisasa. Nchi zilizoendelea wanajenga mpaka juu ya bahari hapa Tanzania shida ni nini? Je, Mkandarasi huwa hatoi guarantee ni muda gani barabara itadumu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Old - Moshi iliyopo Moshi kuanzia Kiboriloni- Kikarara – Kidia hadi Tsuduni, hii ni kati ya barabara iliyokuwa katika ahadi ya Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete katika kampeni za Urais 2010 na Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati huo alikuwa Waziri wa Ujenzi na katika Bunge hili Tukufu kwenye hotuba yake ya bajeti 2016, aliahidi kutenga fedha kwa ajili ya barabara teule na si hivyo tu, niliuliza swali mwaka huu na nikajibiwa upembuzi yakinifu umekamilika na walikuwa kwenye mchakato wa kumtafuta Mkandarasi. Je, ni muda gani unaotumika kumpata Mkandarasi. Je, barabara hii ni lini itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami ukizingatia barabara hii ni muhimu sana na maendeleo ya uchumi wa nchi yetu kwenye sekta ya utalii. Sababu ni njia fupi sana ya kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro na ina vivutio kama vipepeo na ndege wengi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uwanja wa Ndege wa Moshi, uwanja huu umesahaulika kwa muda mrefu hata barabara ya kuelekea airport imefunikwa na majani, wananchi wanalima mazao katika eneo la airport. Uwanja huu ni very strategic kwa ajili ya watalii kuja moja kwa moja
kupitia nchi jirani. Serikali imekuwa ikiahidi watakarabati kiwanja kile, je, ni lini wataanza kukikarabati?

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya ya Moshi maeneo ya Kiboriloni KDC kumekuwepo na matatizo ya mawasiliano sasa licha ya kuwa karibu na Mjini na suala hili limeshapelekwa kwa mitandao yote ya simu, lakini hakuna kinachotendeka. Je, ni lini Serikali itatusaidia minara ya simu iwekwe pale KDC, Mbokomu ili wananchi wa pale waweze kupata mawasiliano.