Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru wewe kwa kunipa nafasi hii kutoa mchango wangu kwa kuandika katika Wizara hii. Pia napenda kuchukua fursa hii kutoa pongezi zangu kwa Serikali yetu namna inavyotekeleza kwa kasi ahadi zake na huduma za jamii. Vile vile, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Wizara hii pamoja na Watendaji wake kwa kazi kubwa wanayoifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia hotuba hii, napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuipongeza Serikali kwa juhudi zake za kujenga barabara na madaraja. Hii ni azma nzuri ya kuwarahisishia wananchi usafiri wa kupeleka mazao yao katika sehemu moja kwenda nyingine. Ushauri wangu katika jambo hili ni kushauri Serikali iwe makini katika kuwasimamia Makandarasi ili kukidhi viwango vya miundombinu hii. Miundombinu hii itakapokidhi viwango, itaiepushia Serikali gharama za ukarabati wa muda mfupi baada ya kujengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Posta Tanzania (TTCL) ni chombo muhimu katika kila nchi pamoja na Tanzania. Naipongeza Serikali kwa kuonesha nia ya kuliboresha shirika hili. Ushauri wangu katika uimarishaji wa shirika hili ni kwamba Serikali ilipatie shirika vifaa vya kisasa ili kwenda sambamba na ushahidi mkubwa uliopo katika wakati huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.