Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017

Hon. Raisa Abdalla Mussa

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017

MHE. RAISA ABDALLAH MUSSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa hii ya kuchangia Wizara hii muhimu kwa nchi yetu ya Tanzania. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia leo hii kuwepo hapa katika Bunge hili Tukufu la Tanzania. Pia ninamshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kumpa subira kiongozi wangu Maalim Seif Sharif Hamad na Mwenyezi Mungu azidi kumpa subira kwa mikiki yote anayoipata katika Serikali ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Na ieleweke kwamba Chama cha CUF hakikutia mpira kwapani, badala yake ni chama kinacholinda Katiba na sheria za nchi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niende moja kwa moja katika suala zima la mada iliyopo mbele yetu. Napenda niseme kwamba Wizara hii ni Wizara ambayo CAG aliilalamikia sana wakati wa kujadili fungu hili wakati tuko kwenye Kamati. ninashangaa sana, kwamba mjumbe wa Kamati ya PAC ambaye alikuwepo siku tuliyojadili fungu hili na malalamiko yaliyotolewa na CAG pale kwamba katika Wizara ambazo zinakosa mafungu basi moja ni hii, kukosa pesa ambazo zinaingizwa na Hazina. Leo anasimama hapa, badala ya kuchangia Wzara hii muhimu, tukamsaidia Mheshimiwa Waziri bado anakwenda kulalamikia hotuba ya upande wa upinzani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kumshauri au kumpa mawazo Mheshimiwa Waziri kutokana na Balozi zetu za Tanzania zilizoko nchi za nje. Nchi ya Tanzania katika balozi ambazo ziko dhaifu basi ni nchi ya Tanzania, mpaka inafikia ofisi ya ubalozi kuvuja na kuna Mheshimiwa mmoja katika Kamati yetu alisema yeye katembelea nchi ya Msumbiji, akakuta ofisi ya Balozi watu wanaingia kuuza chai, kauza nini, haina hadhi kama Balozi ya Tanzania. Leo hii tumefikia Watanzania, ukiiangalia Balozi ya nchi za nje iliyoko Tanzania ina hadhi, tunavyowanyenyekea wenzetu, lakini ni tofauti kabisa na mabalozi wetu walioko nchi za nje, jinsi ofisi zetu zilivyo kama Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri atuambie suala hili la Watanzania ambao wanakutwa na matatizo wakiwa nchi za nje, Balozi zetu wanawasaidia vipi watu hawa? Kuna watu wanaokamatwa na dawa za kulevya na mambo mengine, hasa nchi za Bara la Asia. Wizara haioni umuhimu wa watu wale, ikaundwa mbinu mbadala ambapo wale vifungo vyao wakaja wakavitumikia Tanzania kuliko kunyanyasika kule? Na je, Wizara ya Mambo ya Nje imeshughulikia vipi kwenda kukagua magereza ambayo yako nchi za nje? Watanzania wako kule na hatujui wako katika hali gani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri uje utuambie suala hili, na tunaomba ulifuatilie kwa kina suala la Watanzania walioko kule. Hatujui mateso yao na tuna uhakika wanateseka kwa sababu mtu kwao ndiyo ngao. Leo wako nje ya Tanzania, vipi watu wetu kule watapata haki au kutetewa? Sisi tunaona nchi za nje zote Balozi zao anapokamatwa mtu nje ya nchi yake Serikali ya nchi ile inasimamia kwa nguvu zote kuhakikisha kwamba watu wake wanarejeshwa katika nchi yao kwenda kuhukumiwa. Na wanapata haki zao za kibinadamu kama inavyotakiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni kwamba…
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri katika ripoti yake alituambia kwamba Watanzania waliokamatwa huko nje ni 108, kama ufahamu wangu unaniambia hivyo kwa mujibu wa alivyosema katika kitabu chake hiki. Sasa watu hawa wanashughulikiwa vipi na Serikali ya Tanzania? Ni miongoni mwa haya niliyotanguliza kuyasema kwamba Watanzania 108 ni wengi, wana watoto, wana familia wana wazee, je, Serikali imewasimamia vipi watu hawa 108? Na unatuthibitishia vipi kwamba hawa Serikali ya Tanzania inawashughulikia na inawasimamia haki zao za kibinadamu kama Watanzania wengine, ututhibitishie suala hili, kwamba makosa yao ni yapi mpaka wakafika kufunguliwa mashitaka nchi za nje?
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru, ahsante.