Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 20 16/2017 - Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora

Hon. Saada Salum Mkuya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Welezo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 20 16/2017 - Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kupata nafasi hii ya kuchangia hoja ambazo ziko mbele yetu. Awali ya yote, nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Subhana Wataala na kumtakia Rehema Mtume Muhammad (S.A.W).
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hapo sasa najikita katika hoja ambazo ziko mbele yetu. Kwanza tunaanza na suala la ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri. Tunaipongeza sana Serikali kwa kuwa ni jambo ambalo wamelitilia mkazo mara hii na tunaamini kwamba mifumo ya electronic ambayo imefungwa katika Halmashauri nyingi zaidi ya asilimia 70 kama ilivyoelezwa itakuwa inakwenda kufanya kazi ile ambayo tumeitarajia.
Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo, Mheshimiwa Waziri tunaomba Public Financial Management Reform Programme iende ikajenge uwezo wa watu wetu kuweza kukusanya mapato kwa njia ya kielektroniki. Njia za elektroniki siyo kwa kutumia tu M-PESA na Tigo Pesa lakini ni uwezo wa watu wetu kuweza ku-intergrate hizi systems katika systems zetu za kufanyia kazi. Maana yake ni kwamba tunataka hata watu ambao wanakwenda kulipa kodi walipe kwa urahisi zaidi.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi tunatumia benki kwenda kulipa kwa mfano kodi ya ardhi lakini ukishapewa risiti ya benki inabidi mtu aende tena ofisini kupata risiti nyingine, kidogo utaratibu huu unaweza kuleta usumbufu. Kwa hivyo, ni lazima tuone ni jinsi gani tunaweza tukarahishisha mifumo hii ya kielektroniki kuweza vilevile kuwafanya watu waweze kulipa kodi hizi kwa hiari kwa kuhakikisha kwamba hawapati tabu wala vikwazo vyovyote vile wakienda kulipa kodi hizi.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jambo lingine ni kuhusiana na masuala ya HIV/AIDS, tumeona katika Halmashauri nyingi zimeweka hizi component za ku-address hizi issue za HIV/AIDS, problem iliyokuwepo ni kwamba wengi wanategemea donors yaani miradi mingi ya ku-address issue hizi za UKIMWI zinategemea sana fedha za donors, nadhani huu utaratibu unaweza ukatu-cost baadaye. Sasa hivi kuna indication kwamba maambukizi ya UKIMWI yanaweza yakawa yamepungua katika maeneo fulani lakini inaweza ikatuathiri baadaye kwa sababu financing ya ugonjwa huu tunawaachia donors.
Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri katika kila component yetu ya maendeleo ni lazima issue hizi za HIV/AIDS ziwe addressed mle kwa kutumia fedha zetu za ndani. Kama jitihada hiyo hatutaifanya kwa kutegemea development partners waje watusaidie kwenye masuala haya ya UKIMWI hapo baadaye inaweza ikatuathiri.
Mheshimiwa Naibu Spika, niende katika suala la Tume ya Maadili, tuna-note kazi nzuri sana inayofanywa na Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma. Jambo langu katika Tume hii, isiishie tu kwenye masuala ya mali, madeni lakini vilevile iende ikaangalie behaviors za wafanyakazi. Jambo la msingi ambalo nataka kuli-note hapa hususani kwa watendaji wetu wa afya, sasa hivi tunatumia mitandao lakini utaona kwa mfano inawezekana mwanamke ameathiriwa labda na mumewe au amepata jambo ambalo si zuri anapigwa picha na tunajua kwamba hii picha imepigwa hospitali na imepigwa na mtaalam, anapigwa picha mwanamke yuko utupu kabisa, tunaambiwa huyu mwanamke mume wake amempiga kipigo wakati ni mjamzito yaani maelezo kama hayo, hili jambo siyo zuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, tungependa tusikie issues kama hizo kwa ajili ya kuchukua hatua lakini vitu kama hivyo visichukuliwe kama ni starehe ama visichukuliwe kwamba watu ndiyo wanapashana habari. Jambo hili linakwaza hususan sisi wanawake kwa sababu vitu vingi ambavyo vinatumwa katika mitandao ya kijamii ni vile ambavyo vimemkuta mwanamke na vina udhalilishaji wa hali ya juu. Mitandao mingi utaona picha zingine mtoto amezaliwa labda moyo wake uko nje inatumwa kwenye WhatsApp, ni vitu vya hatari.
Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma iende mpaka ikaangalie behaviors za wafanyakazi wetu wanafanya nini hasa. Tunataka watu wahudumiwe na siyo kutumia zile athari ambazo wamezipata kupashana habari ulimwenguni, kuona kwamba hili ni jambo ambalo labda tunaweza tukaliona hivi hivi, iende katika hatua hiyo pia.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni kuhusiana na Tume ya Ajira. Kwenye Kamati tulikwenda na tukaongea na Tume ya Ajira, wanafanya kazi nzuri sana. System zao ziko vizuri sana na ni system ambazo zimetengenezwa na Watanzania, tunawapongeza sana kwa kazi hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini changamoto iliyopo hapa Wazanzibari kwenye Tume ya Ajira wanapata tabu sana kufuatilia ajira ambazo wame-apply hususan katika Taasisi za Muungano. Siku za kufanya interview utawaona Wazanzibari wengi katika vyombo vya usafiri wanakuja Dar es Salaam. Jambo hili tumekuwa tukilisisitiza kuhusiana na facilitation ya Tume hii kule Zanzibar. Lazima kule Zanzibar kuwe na Ofisi za Tume ya Ajira ili iweze kuwafikia Wazanzibari bila kikwazo chochote.
Mheshimiwa Naibu Spika, hili jambo linasemwa mwaka hadi mwaka kwamba tutafungua Ofisi lakini hazijafunguliwa, kwa kweli vijana wetu wanapata tabu na wanahangaika sana. Kule kuna vijana wazuri tu, wasomi, wamemaliza degrees, they are very good lakini kwa kufuatilia hizi inawakwaza sana kwa sababu ni gharama. Vijana hawa hawajaajiriwa lakini inabidi watafute fedha za kwenda Dar es Salaam kufuatilia maombi ya ajira zao.
Mheshimiwa Naibu Spika, nakusudia kabisa kushika mshahara wa Mheshimiwa Waziri kama hatanipa commitment ambayo itatekelezeka kuona kwamba Tume ya Ajira aidha inafunguliwa Zanzibar au kunakuwa na Ofisi kwa ajili ya watu wa Zanzibar kufuatilia masuala ya kazi katika hizi Taasisi za Muungano.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni kuhusu hii asilimia 10 ya wanawake na vijana. Katika Halmashauri nyingi wanaona kwamba hili jambo ni hisani, hili jambo linaweza likafanyika katika leisure time, hii siyo sawa na hatutarajii iwe hivyo. Tunamwomba Mheshimiwa Waziri achukue hatua kwa wale Wakurugenzi wa Halmashauri ambao hawajatenga hii asilimia 10 na hawana maelezo yoyote. Maana wakati mwingine unaweza ukakuta tuna-review bajeti mtu hajatenga hii asilima 10 na hakuna maelezo ambayo tunaweza tukaridhika nayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu hili siyo jambo la kufanywa kwa wakati wanaoutaka wao au kwa mapendekezo yao ndio waweze kutenga, wengine watatenga asilimia tano wengine asilimia mbili, hapana ni asilimia 10 kwa ajili ya kwenda kuwasaidia akinamama na vijana kujiinua kiuchumi. Wengi wanaona kwamba sehemu pekee ya kupata ajira ni Serikalini, Serikalini hakuna ajira, lakini tukiweza kuwapa mtaji pamoja na mafunzo ya ujasiriamali vijana wengi wanaweza wakatoka katika dimbwi la umaskini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni madeni. Kweli hili jambo ni kubwa kidogo, ukiangalia suppliers wengi hususan wale locals wamekuwa hawapati malipo yao kwa muda muafaka. Hii inaweza ikasababisha waka-perish katika mzunguko huu wa kiuchumi kwa sababu capital yao imeliwa. Hata hivyo, naipongeza sana Serikali imeona umuhimu wa kulipa madeni hususan ya wazabuni pamoja na watumishi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hili suala la wazabuni naomba priority kubwa wapewe kwanza wazabuni wale wadogo wadogo ambao wametoa huduma kwa Serikali lakini zoezi hili liende sambamba na uhakiki wa madeni hayo. Si kila mtu anayeidai Serikali anaidai kiukweli au si kila mtu pesa anayoidai Serikali imepitia katika mifumo sahihi ya manunuzi. Naomba utaratibu uwekwe ili wale watakaolipwa walipwe kwa viwango sahihi na lazima wawe na documentation zote ambazo zinawafanya walipwe.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni hili ambalo tumekuwa tukilizungumza la viwanda. Tunaipongeza sana Serikali chini ya Rais, Dkt. John Magufuli kwa kuona kwamba sasa ni muhimu Tanzania iende katika uchumi wa viwanda. Viwanda vingi viko katika maeneo yetu…
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa umemaliza muda wako.
MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.