Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

Hon. Ali Hassan Omar King

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Jang'ombe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza nashukuru sana kupata nafasi hii. Nianze na msemo, watu wengi sana huu msemo tulikuwa hatuujui, lakini leo mimi nitautolea maana. Kuna msemo unasema heri ya nusu shari kuliko shari kamili.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa natafakari sana juu ya msemo huu, lakini jana nilipata maana yake na alichonifundisha maana msemo huu ni mzee Msekwa aliposema kumbe kulikuwa kuna changamoto kubwa zaidi ya kiusalama kule Zanzibar baada ya Mapinduzi, kwa maana hiyo kulihofiwa kuja kuvamiwa tena na kupinduliwa kwa sababu ilikuwa haina Jeshi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo hii ilikuwa ni shari kamili, lakini nusu shari ndiyo kama haya mambo madogo madogo ambayo tunayazungumza, ni mambo ambayo yanaweza yakarekebishika. Kwa maana hiyo ile shari kamili tumeepukana nayo, lakini sasa hizi nusu shari zinaweza zikaondoka kirahisi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niseme kwamba Muungano wetu huu ni Muungano mzuri sana kwa sababu katika miungano yote ya katika dunia hawana chombo cha kukaa wakazungumza mambo yao, lakini sisi kwenye Muungano wetu huu tunacho chombo ambacho ndiyo hiki cha Mheshimiwa Jafo hapa tunamwambia ambacho tunakaa tunaeleza matatizo na changamoto ambazo zimo katika Muungano na ndipo zinakuja zinatatuliwa changamoto hizo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna aya moja inasema kule kwenye Quran kwamba wanasema kulaukana fil-ardhi malaikatu yamshuna mutumainina laa-nazzalna minasamaai malaka rasula. Ingelikuwa malaika ndiyo wanaoishi kwenye ardhi basi na mitume yao ingekuwa ya kimalaika lakini wanaoishi kwenye ardhi ni binadamu na mitume yao itakuwa ni binadamu. Hii Serikali inaongozwa na wanadamu na ni watu na sisi ni wanaadamu, kwa maana hiyo tunapaswa tuiambie Serikali yetu kuwa kile ambacho kinatutaka. Kwa hiyo tuiambie Serikali ili kuondosha zile changamoto isitoshe na sisi wenyewe ni ndugu, kwa kuwa ni ndugu kwa hiyo tutakapoambizana tutasikilizana zaidi.

Mheshimiwa Spika, sasa na mimi Mheshimiwa Jafo nisikilize jambo moja, kuna makampuni ambayo yamesajiliwa Tanzania Bara yanafanya kazi Zanzibar na kuna makampuni yamesajiliwa Zanzibar yanafanya kazi Tanzania Bara, lakini kampuni zile zilizosajiliwa Tanzania Bara zinafanya kazi Zanzibar hazilipi kodi ya mapato yaani (Cooperate Tax) na kwa sababu Companies Act ya Tanzania Bara inataka mtu alipe Tax Headquarter, kwa hiyo zile Cooperate Tax hazilipwi kule na zile kampuni kule zipo ukichukulia kampuni zote za simu ziko kule, ukichukulia kama benki mengi yako kule, ukichukulia makampuni ya ujenzi yako kule, hayalipi na kule wana-operate under certificate of compliance. Sasa ushauri wangu kule alitoka Waziri mmoja wa Zanzibar alisema hivi kwamba kampuni zinazotoka Tanzania Bara zikajisajili tena Zanzibar, hicho kitu ina maana kwamba hawa ndugu zenu wanakuiteni mwingine katika mazungumzo juu ya jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo tunaomba na hili jambo la kuhusiana na mambo ya Cooperate Tax, kwa sababu tunajua Ibara ya nne iliyotaja kutakuwa na mambo ya Muungano kwenye nyongeza ya kwanza item (10) imetaja hiyo kodi ya mapato kwa watu binafsi na makampuni. Hata hivyo, kulipita makubaliano kwamba kila mmoja atakuwa anakusanya kodi hiyo ya mapato sehemu yake, lakini makampuni yale yanafanya kazi kule, lakini yanalipa kodi ya mapato Tanzania Bara, kwa maana hiyo Zanzibar pamoja na kuwahudumia wananchi ambao ni wateja wa makapuni yale kwamba inakuwa haipokei kodi kutoka makampuni yale hakuna NMB, hakuna CRDB, hakuna TCB, hakuna NBC, hakuna hizo TIGO, hizo zote hazilipi kodi ya mapato kule Zanzibar na zinafanya kazi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hili tunaliomba hili lifanyike, kikae kikao maalum hili lifanyike na Muungano huu ninavyosema tumeungana sisi ni zaidi ya haya mambo ambayo yameandikwa. Wizara ya Kilimo siyo ya Muungano lakini nenda katazame katika masoko ya Zanzibar, sisi tunaita mbatata hivi viazi mviringo utakuta kule maharage, utakuta kule kila kitu, hutokuta kule mchele labda umeandikwa huu wa Cheju, lakini mchele wa Mbeya kule utaukuta. Kwa maana hiyo tumeungana zaidi na Muungano wetu siyo wa mambo ambayo yako kwenye makaratasi, Muungano wetu ni wa mambo ambayo tumeungana kwa damu na kiudugu zaidi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo naunga mkono hoja Mheshimiwa akatutekelezee mambo yetu hayo. Nashukuru sana.