Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023

Hon. Nusrat Shaaban Hanje

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023

MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia Mpango wa Maendeleo wa Mwaka Mmoja. Nitachangia katika maeneo mawili; eneo la kwanza nitachangia kwenye elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekaa kwenye kikao hiki kwa ajili ya kupanga mpango wa maendeleo, lakini maendeleo ni elimu. Yaani elimu yetu kama Taifa ndiyo inachora ramani ya maendeleo. Tunazungumza, tunajadili, lakini kama hatutazungumza elimu, tutakuwa hatujatendea haki Taifa hili. Muda sasa tumekuwa tukijadili kuhusiana na kurekebisha Sera ya Elimu nchini ambayo ni ya mwaka 2014 na kurekebisha mtaala wa elimu ambao ni competence- based lakini 2005 mara ya mwisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili sisi kama Wabunge ambao tunapewa hizi nyaraka na tunasoma, tuone kama uhalali wetu wa kujadili haya upo, tunatakiwa tuyaone katika Mpango. Siyo kwenye bajeti wala siyo kwenye Mpango huu wa mwaka mmoja Wizara imetenga hata senti moja kwa ajili ya kufanya mchakato wa mapitio ya sera na mapitio ya mtaala wa elimu. kwa kifupi mpaka sasa Serikali haijatenga hata shilingi moja kwa ajili ya ku-facilitate wanaofanya mchakato wa mapitio ya sera na mapitio ya mtaala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia ratiba yako, wewe unafahamu zaidi na namna ambavyo tunapanga mambo yetu, unajua kwamba possibility ya kufanikisha tunachokizungumza kila siku ni ama 2023 au 2024 kwa sababu watu hawawezi kwenda kufanya kazi ngumu ya kukusanya maoni na kufanya mapitio, kuita wadau ambao ni professionals, ambao ni Watanzania ambao wanaitakia mema nchi hii, bila kutumia gharama. Haiwezekani! Kwa hiyo hapo nimesema kwa kweli kwa kutoa masikitiko yangu sana kwa sababu nilitegemea mpango uwe na at least hata pesa kidogo kwa ajili ya kuanza mchakato wa mapitio ya mtaala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nitakuwa nimekwenda mbali sana Wizara ilishakutana na Wajumbe wa Kamati inayohusiana na masuala ya elimu, Kamati ya Huduma na kwa taarifa zilizopo ni kwamba tarehe 11 Novemba wanakutana na Wabunge wote kwa ajili ya kupokea maoni. Sasa naomba niombe sasa badala ya kujadili kuhusiana na mtaala, wajadili kuhusiana na sera, kwa sababu kwa taarifa Wizara inajaribu kurekebisha mtaala na sera at the same time, kitu ambacho hakiwezekani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtaala ni zao la sera. Bunge lako litusaidie kuifanya Serikali ituletee mjadala wa kujadili Sera ya Elimu tarehe 11, siyo mtaala wa elimu. Nasema hivi kwa sababu hatuwezi kujadili sera hatujapanga tutafanya nini kutoka mwaka 2014 kwenye sera. Wabunge sehemu pekee ambayo tunaweza kuchangia sisi, ni tunaiona wapi nchi yetu after few years to come, ndiyo tutaeleza malengo. Tafsiri ya tunapotaka nchi yetu ifike ndiyo itatuambia tuandike nini kwenye sera ili sera ikatusaidie watu wanaoandika mtaala wakatoe tafsiri ya tunataka nini kwenye elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwanzo nilisema maendeleo ni elimu. Kwa hiyo kama tunapanga mpango wa maendeleo na hatujadili kuhusu nchi yetu tunataka kwenda wapi. Nitatoa mfano, Kenya wametoka kwenye competence-based, CBC – Competence-Based Curriculum na sasa wanajadili talent and professions, talanta na taaluma. Walishafanikiwa kwenye competence-based.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2005 wakati tumefanya marekebisho ya mtaala ndiyo tuliweka Competence-Based Curriculum ambayo tunayo mpaka sasa hivi. Tukiletewa Waheshimiwa Wabunge wataona kwamba hatuna shida kwenye documentation kama nchi, yaani utashangaa kwani huwa tunajadili nini kuhusiana na kurekebisha mtaala. Kwa hiyo kuna shida kutoka kwenye mtaala kwenda kwa anayepelekewa, yaani kuna shida kutoka kwenye kilichoandikwa na kinachomfikia, katikati hapo ndiyo kuna shida. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapo nitapongeza jitihada ambazo zimefanyika kwa sababu kwenye mpango wametuambia kuhusiana na, kwa kweli tunahitaji maeneo ya kujifunzia; madarasa, Walimu na vitendea kazi. Kwa hiyo tunahitaji na tumeona kwenye Mpango wameweka. Kama mdau wa elimu siwezi ku-ignore jitihada ambazo zimefanyika. Kwa hiyo tuna-encourage sana jitihada, lakini tukumbuke kwamba dunia haitusubiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, dunia inazungumza Mapinduzi ya Nne ya Viwanda (Fourth Industrial Revolution) ambayo inazungumza artificial intelligence, inazungumza algorithm, vitu ambavyo vina-replace human labour. Sisi tunazungumza competence based education ambayo inafundishwa kwa knowledge based education. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtaala wa 2005 unatuambia competence based lakini kinachokuwa delivered darasani ni knowledge based. Knowledge based maana yake mwanafunzi anasoma, anakariri na kukariri ili akafanye mtihani knowledge-based, unajaziwa madude kibao. Kwa hiyo sasa kwa sababu hatutakwenda huko leo, naomba sana kwa sababu tunatumia rasilimali zetu vizuri, dunia inazungumza hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi wakati tunasema dunia inazungumza artificial intelligence, nimpongeze sana Rais, Dkt. Mwinyi na kwa sababu kwenye umri wa vijana tunam-consider kama bado kijana mwenzetu, amejitahidi, kwa sababu amezungumza kuhusu digital currency na imechukuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze sana Mheshimiwa Rais pia kwa sababu anajaribu kuona opportunities. Kwenye hili nitasubiri mjadala ambao tutajadili Sera ya Elimu ambayo tunasubiri muda mrefu kwa sababu ya resources, twende kwenye sera kwanza, tuone mwelekeo wa nchi kwenye elimu tunataka nini, halafu ndiyo tuje tujadili mtaala, kwa sababu najua pia resource scarcity.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ni-move kwenye jambo la pili ambalo ni la jumla. Mimi ni Mbunge kijana, thinking yetu sisi millennials na hili nitalisema na watu wanaojua generation differences watakuwa wanaelewa. Asilimia kubwa ya Watanzania na asilimia kubwa ya Waafrika wanaitwa millennials, watu waliozaliwa mwaka 1980 mpaka mwaka 1996; thinking, smartness, activeness, watu tunataka matokeo, tupo wengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani tukawa tunaendelea kuendesha nchi kwenye mfumo wa tunapanga, kesho tunapanga tena na tena, the same way. Tunaomba tu-move. Tupo wengi tunaomba tu-move, yaani inawezekana kabisa. Watanzania wanataka majibu ya shida zao. Kwa maana tuwe tuna flagship projects, watu wanataka pesa mfukoni, watu wanataka bima za afya, wanataka price fluctuation (mfumuko wa bei) usiwepo, wanataka kula, wanataka wafanye kazi, projects zote tunazoziweka tunazitambua na ni vitu vizuri; progress, miradi mikubwa. Hata hivyo, tunakuwa irrelevant kama nchi kwa sababu Watanzania hawaoni kama hayo mambo yanawagusa directly. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ninachojaribu kusema ni kwamba, Watanzania wanataka majibu ya shida zao na shida zao tunazijua kwa sababu ndiyo wapigakura wetu. Kwa hiyo nchi ambayo inashindwa kutoa majibu ya watu wake definitely at the end of the day inakuwa irrelevant, inakuwa haiishi wanachokitaka wapigakura.

Kwa hiyo hatutachoka kuongea, hatutachoka kushauri kwa sababu haiwezekani sekta ambayo kila Mbunge akiongea anazungumza; kilimo, tunapata chakula, inachangia pato la Taifa, lakini kila mwaka tunapanga the same. Kwa nini hatuweki pesa kwenye kilimo? Inachosha na inavunja moyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naongea kwa sababu hii nchi, mimi Muislam, kuna kitu kinatwa masuulia, yaani ukiwa una nafasi kwenye Taifa unatakiwa ufanye maamuzi, ukishindwa kufanya maamuzi, kesho Mwenyezi Mungu atakuhoji kwa kushindwa kufanya wajibu wako.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Hanje kengele ya pili hiyo.

MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania wanataka majibu ya shida zao, naomba tuwasaidie kuwapatia. (Makofi)