Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Nishati

Hon. Eng. Ezra John Chiwelesa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Nishati

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi pia niweze kuchangia mchango wangu katika hotuba ya Wizara yetu ya Nishati, kwanza nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri kwa hotuba nzuri ambayo ameitoa na Naibu Waziri pamoja na Watendaji wote wa Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, lakini pia nitoe shukrani kwa Wizara hawa kwa Waziri na Naibu Waziri nakumbuka mwezi Desemba na mwingine mwezi Januari mlifanya ziara Biharamulo mkatutembelea sehemu kubwa mkilenga katika kituo chetu cha kupoozea umeme cha Nyakanazi ambacho kinajengwa kwa hiyo niwashukuru sana kwa visit ile ambayo mmeifanya na sehemu zote ambazo tulitembelea na ahadi nzuri ambazo zilitolewa base done contract ambayo ilikuwepo pale ambayo tunategemea itamalizika tarehe 30 mwezi wa tatu kama ulivyosema wakati tumetembelea Nyakanazi pale. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kwa bahati mbaya mpaka sasa contract ile haijamalizia na wale wakandarasi bado wapo site. Labda niseme jambo moja tu tumekuwa na tatizo kubwa sala la kukatika umeme sehemu za Biharamula na Ngara na halikadhalika na Chato, lakini Chato nadhani kuna unafuu ila kwangu kwa sehemu ya Biharamulo tatizo kubwa tupo kwenye low voltage umeme unaotoka geita kuja Chato substation unakuja kwenye 34 Kv lakini kutoka pale nadhani kuja Biharamulo unakuja uko chini sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa umeme ule hauwezi kufanya kazi na sasa hivi tuna shinda kubwa watu hata fridge kwenye supermarket pale ice-cream zinayeyuka napigiwa simu Mbunge, maji sasa hivi tunamgao wa maji Biharamulo maji yenyewe hatuna lakini hata yale machache tuliyonayo Biharamulo tupo kwenye mgao tupo kwenye mgao kwasababu umeme uliopo ni mdogo kwa hiyo pampu zetu pale Kagango haziwezi kupampu yale maji hatimaye tukaweza kupata maji vizuri pale mjini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini baada ya kufuatilia yote haya maana nimejaribu kufanya follow up ya issue ya Nyakanazi, Nyakanazi imeahidiwa kwenye Ilani ya CCM na pia tulishaenda pale tukatembea kwamba tulikuwa inabidi tupate umeme wa Msongo wa Kilo Volt 220 kutoka Geita uje pale. Nimepita pale juzi ujenzi unaendelea vizuri, lakini lipo tatizo ambalo labda sasa kwasababu na Waziri Mkuu yupo hapa ningependa kujua tuna transfoma mbili ambazo inabidi zije kufungwa pale Nyakanazi. Tangu tarehe 20 Desemba transfoma zile zipo Bandarini hapa, tarehe 20 Desemba as we are talking sasa inaenda sasa ni miezi sita. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini shida iliyopo pale ni kwamba TANROADS na TANESCO wanashindwa kuelewana jinsi gani watalipana kwenye surcharge amount ili waweze ku- release zile transforma zile pale Nyakanazi. Lakini kipindi yote haya yanafanyika sisi pale kwetu bado ni shida ndugu zangu, maeneo ya Nyakanazi pale hata kuchaji simu wananchi wananipigia simu hawawezi kuchaji simu umeme upo chini lakini kuna watu wa Serikali hii hii ambayo inatekeleza Ilani ya CCM watu wa Serikali hii hii ambao wameapa kumsaidia Rais wanashindwa kukaa chini na kuelewana kwa vitu vidogo hivi wananchi wanatesema. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa nilikuwa naomba tunapo windup nipate kauli ya Serikali hizo transfoma zinatoka lini Serikali ni hii hii moja, maana hata mkizizuia pale mwisho wa siku zitatoka tu hata zikikaa mwaka mzima zitatoa tu sasa kinachoshindikana ni nini hizo transfoma zikatoka leo zikafungwa pale, mambo yenu ya kulipana mnatoa mfuko wa kushoto mnaingiza mfuko wa kulia mtayafanya baadaye kipindi hicho wananchi wanyonge walioko huko vijijini wanapata umeme.

Mheshimiwa Spika, naomba TANESCO tuwasaidie maana sasa TANESCO nia yetu nyie ni nzuri mlishakuja pale mkasema, lakini 2.3 bilion per one transforma hiyo fedha mnaitoa wapi? Ukiongeza 4.6 bilion umlipe TANROADS hiyo fedha si ingeenda kufanya miradi mingine ya umeme pale! Kwa hiyo, ninadhani kuna vitu vingine nadhani mkae wenyewe humo ndani muelewane lakini sisi tunachohitaji tuone zile transfoma zimefungwa pale wananchi wa Biharamulo waondokane na tatizo la kukatika katika umeme hata wenye viwanda vidogo vidogo pale Nyakanazi waweze kufanya kazi maana leo tuna viwanda lakini hakuna anayeweza kufanya kazi kwasababu umeme una run under low voltage. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hilo jambo naomba niliweke wazi kama hatutapata majibu ndugu yangu Mheshimiwa Kalemani najua tuna-share ma-generator ya pale Biharamulo otherwise sasa itabidi unipe permission Biharamulo tuanze kuwasha Generator kwa kutumia mafuta ya Diesel kipindi wewe unapata ya kutoka Geita nipate ya Biharamulo kwa kutumia mafuta ya diesel mpaka pale mtakapopata zile transforma tuweze ku-balance tukae pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini baada ya kulisema hilo lipo jambo jingine moja ambalo nilipenda pia niliongelee Biharamulo tunao mgodi wa STAMIGOLD last week nadhani kama wiki mbili nimetembelea mgodini pale. Imeletwa line ya umeme kutoka Geita Special line mpaka Mgonini STAMIGOLD lakini cha ajabu ile line ipo pale umeme bado haujaingizwa ndani na wale watu wa mgodi wa STAMIGOLD mgodi wetu wa Serikali ambao hata CSR tu wanashindwa kunisaidia vitu vidogo pale mtaani wale watu wanalipwa 1.2 bilion kila mwezi kwa ajili ya mafuta ya diesel ule mgodi ni wa Serikali ungeniambia ni GGM wanalipa hata Bilioni ngapi I don’t care kwa sababu ni fedha yao labda mna process nyingine ya kuwarudishia lakini ile ni fedha ya Serikali ule mgodi ni wetu sisi na TANESCO nyie mkishawaingizia umeme kule your assured kupata more than seven hundred million per month nyie ndio mtakuwa the large users wa umeme ukiondoa Kagera sugar kwa Mkoa mzima wa Kagera .

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, niwaombe hilo jambo mliangalie ili tatizo limalizika na hata wakati wa ku-wind up pia nipate majibu maana sisi tuna mgodi lakini mgodi unaoshindwa hata kunisaidi barabara pale Kaniha huo mgodi ni wa nini? Mgodi unaoshindwa kunisaidia hata kujenga zahanati pale ule mgodi ni wa nini. Lakini kwa sababu wana run under high cost kama hizi za kununua mafuta maana wakikulipa wewe Milioni 700 TANESCO wanabaki na Milioni 500 itaweza hata kutusaidia na sisi tukiomba CSR watusaidie kusaidia jamii iliyozunguka mgodi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kuja jambo jingine Mheshimiwa Waziri ulipotembelea Biharamulo wakati ule kuna kata kama tano ambazo bado hazijapata umeme kata ya Kalenge lakini najua Kalenge watapata umeme kutoka kwenye hii substation ya Nyakanazi pindi unaenda Kigoma kati ya vile vijiji thelathini na ngapi ambavyo vimetajwa, lakini kuna Kata ya Kaniha na pia kuna Kata ya Nyantakara kuna Kata ya Nyanza. Lakini hii Kata ya Kaniha na Nyantakara ulipokuja kuna mkandarasi pale ana umeme wake anawauzia wananchi Power Janne. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ulitoa maelekezo specific kwamba umeme ni shilingi 100 per unit huyu mtu tukakaa kwenye Baraza la Madiwani tunakuelekeza Meneja wa TANESCO na Mkuu wa Wilaya wakati ule tulikuwa pamoja leo karudi tena anawaambia watu anawachaji shilingi 2,000 TANESCO mmemruhusu, sasa nashindwa kuelewa, yaani Waziri unatoa order kuna mtu mwingine nyuma yako naye anatoa barua ingine, mwenye madaraka ni nani hapo?

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nilikuwa naomba pia hili jambo la power Janne tupate majibu humu ndani maana Diwani wa Kalenga anashinda mjini pale anahangaika kila siku, wale watu wamegoma kuwasha umeme na wamesema wanataka shilingi 2000 na wewe ulishaagiza ni shilingi mia moja, nimemuuliza Naibu Waziri, nimekuuliza wewe mwenyewe umeniambia shilingi mia moja. Kwa hiyo nilikuwa nipate majibu ya Serikali wananchi wa Kalenga wasikie, walioko Mavota wasikie na sehemu nyingine kwamba ni shilingi mia moja ile ile iliyoagizwa na Waziri ndiyo hiyo inayofanyika pale. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho nilitaka niongee kwasababu ya muda kuhusu issue ya bomba la mafuta hili la kutoka Uganda. Niishukuru sana Serikali na hasa nimpongeze Rais kwa kusaini contract hii na hatimaye sasa neema hii kubwa inakuja kwenye nchi yetu. Lakini nilikuwa nawaza katika angle ya tofauti kidogo, sehemu kubwa ya lile bomba itakuwa ni project ile ya mabomba yenyewe yanayolazwa.

Mheshimiwa Spika, sasa nikawa naomba Mheshimiwa Waziri na Serikali, kama mnaweza mkaongea na contractor najua kutengenezea bomba huko watakapozitengeneza akazisafirisha zile bomba kilomita 1000 azifikishe transportation cost tu ile anatosha kuja ku-setup kiwanda hapa, I am sure tukiangalia cost ya ku-transport bomba za kilomita 1000 yule mtu akabeba mashine Europe akaja hapa mkampa eneo na watu wake nilicho na uhakika nacho kutakuwa na transfer of technology lazima yule mtu baada ya kuondoka hapa watu wetu watakuwa wamejifunza kwa sababu tuna vijana ma-engineer tuna watu ambao wamesoma wataajiriwa kwenye kile kiwanda, kwake ni rahisi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukishampa site akaweka hapa ni rahisi kwasababu anafanya serving kwa sababu bomba atazizalishia hapa na the good thing ni kwamba badala ya kuleta meli nzima imejaa mabomba, ukakodi truck zaidi ya 600 zaidi ya 800 zikaanza kusafirisha mabomba kuelekea Uganda unampa site hapa, kila siku truck kumi anatoa zinaenda site zinashusha mabomba, truck ngapi anatoa kwake logistically itakuwa imekaa vizuri. Kama mtaturuhusu tunaolewa hivi vitu tunaweza tukawasaidia hata kama atakuja hapa ili sasa tushawishi yule mtu kwamba hatukuelekezi boma uje uzalishie hapa leta material, fanya kila kitu leta watu wako, leta mashine tumekupa site hii hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nina hakika baada ya project ile yule mtu zile mashine hatazing’oa hapa na sisi tunafanya research ya mafuta kesho na kutwa kama vijana wetu wamejifunza watatumika wao, we are sure leo tumejenga flying over pale niliwahi kusema, vijana ma-engineer wa Kitanzania waliohusika na flying over ya Ubungo leo wanahusika na kwingine baada ya muda hatutahitaji wageni vijana hawa hawa wa Kitanzania watajenga vile vitu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo niombe hilo wazo ni zuri kibiashara ni wazo zuri kwa manufaa ya nchi kama mtaweza mshawishini huyu mtu anaweza aka-set up hata sehemu mbili au tatu za kuja kutusaidia.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ya muda nashukuru sana na naunga mkono hoja ahsante. (Makofi)