Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Waziri Mkuu

Hon. Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Waziri Mkuu

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuchangia hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Nitajikita hasa katika sehemu mbili na kama kuna muda nitaongeza, lakini najikita katika ajira pamoja na elimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninapozungumzia ajira, ni kwa ajira kwa watu ambao wana ujuzi wa kutosha kufanya majukumu katika ajira hizo. Namaanisha Skilled Labor. Tunapozungumzia uchumi wa kati ambao tumeshaingia; katika hotuba hii nimeangalia sijaona vizuri namna ambavyo tumedadavua vizuri kupata ajira vizuri kwa vijana na wengine, lakini pia ajira yenye ujuzi. Nina maanisha nini?

Mheshimiwa Naibu Spika, ninapozungumzia ajira, nazungumzia ajira na watu ambao wana ujuzi wa kutosha kufanya majukumu katika ajira hizo, namaanisha skilled labour. Sasa tunapozungumzia uchumi wa kati ambao tumeshaingia uchumi wa kati, katika hotuba hii nimeangalia sijaona vizuri namna ambavyo tumedadavua vizuri kupata ajira vizuri kwa vijana na wengine, lakini pia ajira yenye ujuzi inamaanisha nini? Tumejikita kutoa elimu mpaka kufikia Vyuo Vikuu, kupata degree na na tunavyoandaa hawa watu wakiondoka pale, hawa wanakuwa katika level ya managerial, yaani wanakuwa ni supervisors, lakini katika level ile ambayo ni watendaji kazi ambao wapo hasa katika VETA, hatujajikita sana. Hapa ndipo tutaandaa wale watenda kazi, ambao watasaidia kuinua uchumi wa nchi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, tukiangalia vyuo vya VETA vilivyopo, siyo mikoa yote ina VETA, lakini kama mikoa yote haina VETA, bado Walimu wanaokwenda kufundisha wanafunzi wetu ni wachache na vyuo vinavyotoa ni vichache. Kwa hiyo hapa sasa ndio Serikali ijikite katika kui- invest huko, kuhakikisha tunapata Walimu wazuri ambao watakwenda kufundisha, yaani hao technicians watakaokwenda kufundisha VETA ili tuweze kupata watu ambao ni skilled. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, zaidi ya nusu ya Wabunge tuko hapa kila mmoja utakuta mtu anakuuliza kuna ajira wapi, vijana wanatuuliza, wanasema nataka ajira, lakini tumeweka ajira kama kitu ambacho watu wamefika university, lakini kumbe mtu akifunzwa vizuri kuhusu nyanja yake kwa mfano tukisema wafanyakazi wa majumbani qualified, wafanyakazi wa saloon qualified, gardeners qualified, tuwapate wapi watu ambao ni qualified katika nyanja tofauti hawa ndio watapata kipato na pia wataweza kuajiriwa kwa sababu wana ujuzi na wanaweza kuongeza pato la Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunahitaji kutengeneza middle class wengi ili tuweze kupata kodi na Serikali iweze kujiendesha. Sasa Serikali, haijajikita hapo. Tukiangalia katika bajeti ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kitengo Vote 65 ambapo walitengewa bilioni moja mpaka nazungumza hapa haijatoka. Hii inaonesha kwamba bado Serikali haiko serious kuangalia ajira kwa vijana. Kwa hiyo naomba Serikali iweze kuangalia hivyo na Serikali ihamasishe, kuna short courses za mambo hayo. Serikalini hawazungumzi kwamba kuna short courses ya hiki, hiki, hiki. Watu wakifikiri ajira anajua aende akasome, amalize form six, aende mpaka chuo kikuu, lakini hao wanaomaliza darasa la saba kwenda mpaka kidato cha nne tunawapeleke wapi? Tuandae katika bajeti yetu, waende wakafanye kazi waweze kuleta uchumi wa nchi hii, wafanye kazi inayotakiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wezetu China mwaka 2017 walikuwa na technicians milioni hamsini. Sasa na sisi tukijiwekea malengo angalau wanafunzi hao wanaomaliza darasa la saba mpaka form four tuwa-train katika hizo kada, wote wanaofanya decoration na whatever hivyo tutafika mbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama hiyo haitoshi, napenda nikazie pia hawa Walimu ambao wanapata diploma kwenye DTE hao Walimu ni muhimu, wako wachache, unakuta nyumba wamekutengenezea mlango, mlango haupendezi, lakini finishing kama hii wanafundisha pale na ndizo ajira, tunahitaji tupate vitu hivyo vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kimoja nataka tuzungumzie kwa watu wenye ulemavu, watu hawa wamekuwa wakitozwa kodi, niombe Serikali itoe kodi kwenye vifaa ambavyo ni vya watu wenye ulemavu…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana.

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)