Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.

Hon. Salma Mohamed Mwassa

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.

MHE. SALMA M. MWASA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchangia hoja kwenye Wizara hii ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
Kwanza niongelee upunguzfu wa Walimu wa masomo ya Sayansi, Hisabati na Lugha. Pamoja na jitihada za Serikali za kuwapeleka Walimu wachache kwenye mafunzo ya masomo ya Hisabati na Sayansi lakini bado idadi ni ndogo ukilinganisha na udahili mpya wa wanafunzi katika kipindi hiki cha elimu bure kutoka Elimu ya Msingi hadi Sekondari. Hivyo nashauri Serikali iangalie upya mpango wa kuongeza Walimu hasa katika masomo haya ya Sayansi, Hisabati na Lugha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee pia miundombinu. Kuna tatizo la upungufu wa miundombinu na udhaifu wa miundombinu.
Kwa mfano, upungufu wa madarasa, maabara, nyumba za Walimu na vyoo hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam. Kutokana na idadi ya kubwa ya wanafunzi katika Mkoa wa Dar es Salaam kuna upungufu mkubwa wa madarasa, nyumba za Walimu, madawati na vyoo hasa kwenye Shule za Msingi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia niongelee ubora wa elimu. Ubora wa elimu yetu hasa kwenye shule zetu za Serikali siyo mzuri. Nashauri Walimu wapelekwe Semina na Ukaguzi wa shule ufanyike mara kwa mara ili kuboresha ubora wa elimu. Napenda kujua kutoka Serikalini ni lini shule za Serikali zitaanza kuwa kwenye kumi bora katika mitihani ya Taifa? Kwani sasa shule zinazoongoza ni za binafsi tu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.