Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara

Hon. Salim Hassan Turky

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpendae

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara

MHE. SALIM HASSAN ABDULLAH TURKY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii. Napenda niendelee kuwapongeza waumini wote wa Kiislam kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Ramadhani zao ziwe njema, tufunge kwa raha mustarehe na wale wanaotusindikiza, tushirikiane vizuri zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla ya kuchangia, nataka ni-declare interest mimi ni mfanyabishara mwenye viwanda. Napenda ku-declare interest kwa sababu hata kule Jimboni kwangu nilipogombania watu walinipa kura nyingi sana kwa sababu waliamini ni mfanyabiashara na mwenye viwanda. Kwa hivyo, leo nikisimama hapa naomba sana watu wasinitafsiri kwamba natetea viwanda vyangu, natetea viwanda vya Tanzania kwa ujumla wake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niseme katika kukubali kauli ya Mheshimiwa Rais wetu, kampuni zetu sisi tumewekeza baada ya kuona Mheshimiwa Rais yupo tayari kupokea viwanda. Hivi sasa tumejenga kiwanda kikubwa sana East Africa nzima kiwanda cha kukoboa mpunga ambacho kiko Morogoro, kinakoboa tani 280 kwa siku na watu wa Morogoro wapo watakuwa mashahidi na baada ya miaka miwili kiwanda hicho kitakuwa kinakoboa tani 560. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama hilo halitoshi, Mheshimiwa Rais alikuwa anatuhimiza sana kiwanda cha dripu, nacho kiko tayari tukijaliwa mwezi Oktoba tutamwalika rasmi aje akifungue. Kama hilo halitoshi, hapa Dodoma tunawekeza kiwanda kikubwa kabisa cha sunflower kwa Afrika hii na tumepata hekari 90 Zuzu, tunategemea mwanzo wa mwaka ujenzi utaanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini baada ya kumuamini Mheshimiwa Rais katika viwanda tunapata changamoto kubwa sana ambapo tunaamini kwamba kuna watu wanadumaza maendeleo ya viwanda vyetu. Kuna mfano halisi, sasa hivi kuna mafuta yako bandarini ya kampuni karibu tatu au nne ikiwemo na ya Burundi, mafuta haya yalipofika nchini na kawaida ya nchi yetu mafuta yakifika bandarini yanakaguliwa na TBS, TBS walipoyakagua walisema mafuta haya ni crude, tena mabaya sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, wafanyabiashara wale walipopeleka documents zao TRA, la kushangaza sana Kamishna anazungumza pale kwamba mafuta haya ni mabaya tunayataifisha. Neno taifisha sasa hivi katika juhudi za Mheshimiwa Rais wetu jamani linatoka wapi, litatutisha wafanyabiashara. Ikiwa mfanyabiashara mwenye kiwanda mafuta yake yanataifishwa Wamachinga mitaani wanaopiga kelele wana hali gani? Wanapopiga kelele kwamba TRA wanawasumbua, hili lina ukweli wake. Kwa hiyo, naomba Wizara husika waangalie suala hili wanali-control vipi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mafuta haya baada ya yeye kuyakataa yasitoke association ya wenye viwanda wakapeleka maombi Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri Mkuu kwa utaratibu wao wenyewe wakapeleka mafuta haya yakachunguzwe na Mkemia Mkuu. Mkemia Mkuu amesema mafuta haya ni crude. Sasa wametoka watu wameenda tena TRA, Kamishna anasema mafuta haya siyo crude ni semi- finished. Yale mafuta ambayo yalikuwa yanasemwa hayafai kuliwa na binadamu, watakufa, hayawezi yakaingia nchini, sasa anasema ni mazuri yaliwe na watu hawa, hapo ndipo tulipofika sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kumkamata hapo akadai sasa vifaa ambavyo anataka uwe navyo mafuta yakingia nchini. Anakudai wewe export originally document na documents zote originally zinatokea nchi ile. Sisi wanunuzi hata wasafirishaji wa korosho wa nchi hii, unapotengeneza export certificate hiyo ni mali ya exporter siyo ya importer, sisi tunazoletewa ni copy. Hiyo sheria alianza mwaka jana copy zilikuwa zinakubaliwa lakini kwa mzigo huu sasa anakwambia lete original, tunazitoa wapi huu mwezi wa saba?

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwaambieni hili jambo sisi wenye viwanda vya mafuta bahati nzuri asilimia 90 ni Watanzania wazalendo, tunatokaje hapa? Hizi documents anazozidai kwa kweli hatuwezi tukazipata hata siku moja kwa sababu ni mali yao na sisi hapa tayari tumeshaleta copy certified ambazo ndizo zilikuwa zikitolea mzigo miaka yote hiyo, leo unaambiwa ulete originally tunatoa wapi originally? Kwa hiyo, mkae mkijua hili jambo linadumaza maendeleo ya viwanda vyetu. Leo viwanda vitano vya refinery vimefungwa, watu 280 wamekosa ajira kwa sababu …

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)