Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Hon. Eng. Joel Makanyaga Mwaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chilonwa

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. JOEL M. MAKANYAGA: Mheshimiwa Spika, nampongeza sana Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Serikali nzima ya Awamu ya Tano na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kazi kubwa inayoendelea kwenye WIzara hii. Naipongeza sana Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutoa pesa za kutosha kwa Wizara hii kulingana na bajeti ya 2018/2019 (page 10 and 11). Matumizi ya kawaida fedha iliyotoka ni asilimia 72.66 Vs asilimia 75. Miradi ya maendeleo fedha iliyotoka ni asilimia 60.98 Vs asilimia 75.

Mheshimiwa Spika, naipongeza sana miradi mikubwa ya Kitaifa kama ilivyoorodheshwa kitabuni ukurasa 53, 61, 117, 192 na kadhalika. Vile vile naipongeza sana Serikali kwa miradi mikubwa hapa Jijini na Mikoani Dodoma. Miradi hiyo ni Dodoma outer ring roads pages 47,176 and 271. Ujenzi wa Ikulu ya Chamwino zikiwemo na barabara za kwenye Mji wa Chamwino. Ujenzi wa Miji ya Kiserikali pale Mtumba. Lami barabara ya Kongwa Junction – Mpwapwa – Gulwe – Kibakwe.

Mheshimiwa Spika, nina ombi mahsusi; daraja kati ya Chilonwa na Nzali ambayo ni ahadi ya Mheshimiwa Makamu wa Rais, mama Samia Suluhu Hassan. Barabara ya Chalinze Nyama – Chilonwa – Dabalo – Itiso – Chenene. Mawasiliano ya simu za mkononi katika Kata zifuatazo: Zajilwa (ina vijiji vitatu) Segola (ina vijiji vitano) Haneti (ina vijiji vinne) Itiso (ina vijiji vinne) Dabalo (ina vijiji vitano) pia kwa sasa kuna Dabalo ni Mji mdogo na Membe (ina vijiji vitatu). Kata hizi tano zina mawasiliano hafifu tena kwa wakati fulani.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.