Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Hon. Dr. Immaculate Sware Semesi

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa nafasi ili name niweze kutoa mawazo yangu katika Wizara hii iliyo mbele yetu. Ni dhahiri kwamba uchumi wa nchi, maendeleo ya jamii na ya mtu mmoja mmoja kwa kiwango kikubwa hutegemea masuala ya elimu kwa upana wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hizi dakika chache nitagusia Sera yetu ya Elimu kwa ujumla na hali ya elimu katika vyuo vyetu vya elimu ya juu pamoja na dhana nzima ya sayansi na teknolojia. Sera yetu jinsi ambavyo tunazidi kuirekebisha nafikiri ilikuwa inakidhi wakati nchi yetu ilikuwa inasimamia sera ya ujamaa na kujitegemea lakini kwa nyakati hizi sasa za soko huru na mabadiliko mbalimbali ya kiuchumi, Tanzania Sera yetu ya Elimu na mitaala ya elimu yetu inawafanya vijana tunaowazalisha wanakuwa siyo competitive kwenye soko ndani ya nchi, East Africa Community na duniani kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kwa nini Sera yetu hii inatuweka katika dhama za zamani na siyo za kisasa. Mfano mdogo tu kwenye mitaala, mitaala yetu tunayoitunga ni mepesi na rahisi kufuatilia lakini realistically haituvushi pale tunapotaka kwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano tu mzuri tuna somo la Development Arts and Sports kwa wanafunzi wa grade one. Hili ni somo la vitendo lakini unawafundisha watoto ukuti ukuti, jumping rope theoretical na unawapa mtihani tunataka kukidhi nini wakati hili ni somo la mchezo. Kwa hiyo, tuangalie tunataka ku-achieve nini kuanzia elimu ya msingi, sekondari mpaka vyuo au technical school.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la muda wa kuanza shule na usafiri kwa wanafunzi vijijini na mijini. Kwenye bajeti ya mwaka 2017/2018 nilitoa proposal hebu tuangalie kwa upya muda watoto wanaotakiwa waanze shule hususani wa shule za msingi. Unapoanza safari yako yoyote saa kumi na moja au saa kumi na mbili alfajiri unakutana na wanafunzi vitoto vya miaka sita, saba wamelala saa ngapi, wanaamka saa ngapi, efficient inatoka wapi? Unawaambia saa kumi na mbili na nusu wafike shule, saa moja masomo yanaanza na kadhalika, wanafunzi wa vijijini wanatembea kwa umbali mrefu saa ambazo si sawa na wanafunzi wa mijini usafiri nao ni wa shida na wanapata shida, kwa hiyo, by the time mtoto anafika shuleni amechoka mentally na physically hawezi kupokea kile anachofundishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vivyo hivyo kwa walimu wanaowafundisha hawa wanafunzi wanakuwa kwenye level za stress. Ndiyo maana unakuta adhabu zinazotolewa zinaweza zikawa za kupitiliza kwa sababu kwanza mwalimu huyu hana mshahara unaomkidhi, ana malimbikizo ya mishahara na marupurupu mbalimbali kitu ambacho hakimpi motivation vya kufundisha plus anavyoenda shule tayari ana stress. Kwa hiyo, level ya elimu haiwezi kupanda au kuwa improved kwa mazingira tunayoishi sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti suala lingine kwenye sera ambalo nataka liangaliwe ni mitihani ya kuhitimu especially ya darasa la saba. Wanafunzi hawa hatuwatendei haki kwa sababu ni siku moja ya kukutathimini wewe uende kutoka level moja kwenda nyingine. Nafikiri tuangalie jinsi ya kuwafanyia tathmini wanapotoka daraja moja kwenda lingine, wale ambao labda unasema hawakufaulu kwa sababu pia kuna malalamiko mengi ya kuvuja kwa mitihani na usahihishaji mbovu, kwa hiyo, unampa one time chance ambayo siyo fair. Basi yule ambaye hajafaulu apewe nafasi ya ku-reseat au assessment nyingine zitafutwe au hawa wanafunzi ambao kwa asilimia kubwa vijana, zaidi ya vijana milioni tano au sita tunawaacha hawaendi sekondari kwa sababu hakufauli hii elimu ya msingi tuwape alternative labda za kwenda shule za vocational training au ku-reseat ile mitihani ya primary kama wana nia ya kwenda sekondari waweze kwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala linguine…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba dakika moja tu.

MWENYEKITI: Haya, chukua dakika moja.

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine adhabu kali zifuatiliwe upya kwa sababu zinaenda kinyume na haki binadamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia nigusie suala la elimu ya juu na sayansi na teknolojia. Kama Wizara inavyosomeka ni Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia lakini hii sanyansi na teknolojia haiwi reflected hata kwenye bajeti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ilitengewa shilingi bilioni moja ikasomeka sifuri hawakupata chochote safari hii, nasoma hapa kwenye randama wametengewa shilingi bilioni 3.5 tena kwa fedha za nje…

MWENYEKITI: Ahsante.