United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Mambo ya Kuzingatia wakati wa Kutembelea Bunge
Vikao vya Mikutano ya Bunge huanza saa 3:00 asubuhi na kwa kawaida huendelea hadi saa 7:00 mchana ambapo husitishwa. Wabunge hurejea tena saa 11:00 jioni na kikao huendelea hadi saa 1:45 usiku ambapo Bunge huairishwa mpaka siku inayofuata. Hivyo basi, wageni wote wanapaswa wawe wameketi katika maeneo husika kabla ya saa 2:45 asubuhi na saa 10:45 jioni kabla ya vikao kuanza.
Ndani ya Ukumbi wa Mikutano ya Bunge, wageni wanapaswa kufuata na kuzingatia masharti yafuatatayo:-
Mambo yanayoruhusiwa Bungeni
· Kukaa kimya na kwa heshima inayostahili hadi watakapotoka nje ya ukumbi huo.
· Kuingia na kutoka Ukumbini kwa staha.
· Kuzima simu za mikononi.
· Kurejesha kitambulisho wakati wa kuondoka maeneo ya Bunge.
Mambo yasiyoruhusiwa Bungeni
· Hairuhusiwi kusoma kitabu chochote, gazeti, barua au hati nyingineyo ambayo si orodha ya shughuli za Bunge.
· Hairuhusiwi kuandika wala kurekodi jambo lolote linalozungumzwa, isipokuwa tu kama ni wawakilishi wa vyombo vya habari au maafisa wa serikali.
· Hairuhusiwi kuvuta sigara au kiko wakati wowote wakiwa ndani ya Ukumbi wa Mikutano ya Bunge au mahali popote nje ya Ukumbi huo ambapo kuna mahali pa kukaa wageni.
· Hairuhusiwi kuingia na kamera wala kupiga picha kwa kutumia kifaa chochote kile.
· Hairuhusiwi kufanya jambo au kitendo chochote ambacho kinaweza kuvuruga amani na utulivu Bungeni.
Hon. Anatropia Lwehikila Theonest
Special Seats (CHADEMA)