Parliament of Tanzania

Wabunge wasisitizwa kusimamia utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametakiwa kusimamia vyema utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo kwa kuhakikisha kuwa Serikali inatekeleza mipango iliyojiwekea kwa wakati ili kuimarisha ustawi wa wananchi wanaowawakilisha na taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa leo Mjini Dodoma na Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson wakati akifungua semina fupi ya Wabunge kuhusu Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Dunia iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia mpango wake wa kufanya kazi pamoja (Delivery as One).

Dkt. Tulia alisema kuwa Wabunge wana jukumu la kuzingatia malengo hayo na kuhakikisha yanatekelezwa kwa kuwa mipango yote na mikakati ya maendeleo hupitia Bungeni hivyo hawana budi kusimamia malengo hayo ipasavyo kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu.

Akizungumza wakati wa semina hiyo Mwakilishi Mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez alibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli inafanya kazi nzuri katika utekelezaji wa Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Dunia na kuwataka Wabunge kuwa mabalozi wazuri katika utekelezaji wa malengo hayo.

Bw. Rodriguez aliongeza kuwa ni muhimu sana kwa Wabunge kuweza kuyaelewa malengo hayo ya Dunia ili waweze kufanikisha utekelezaji na ufuatiliaji wake katika ngazi zote za Taifa.

Mwaka 2015 nchi 193 ikiwemo Tanzania zilikubaliana kwa pamoja kutekeleza mkakati wa kumaliza umaskini, kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na kupigania haki na usawa. Katika kufanikisha hilo nchi hizo zilikubaliana kupitisha Malengo Endelevu 17 ambayo ni Kutokomeza Umaskini, Kukomesha Njaa, Afya Njema na Ustawi, Elimu Bora, Usawa wa Jinsia, Maji Salama na Usafi, Nishati Mbadala kwa Gharama Nafuu, Kazi zenye Staha na Ukuzaji Uchumi, Viwanda, Ubunifu na Miundombinu, Kupunguza Tofauti.

Malengo mengine yaliyoafikiwa na nchi hizo ni Matumizi na Uzalishaji wenye Uwajibikaji, Miji na Jamii Endelevu, Kuchukua Hatua dhidi ya Mabadiliko ya Tabia Nchi, Kuendeleza Uhai katika Maji, Kulinda Uhai katika Ardhi, Amani, Haki na Taasisi Madhubuti na Ushirikiano ili Kufanikisha Malengo.

Naye Naibu Katibu Mtendaji Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Maduka Paul Kessy alisema kuwa Tanzania imejipanga kutekeleza malengo hayo kwa ufanisi ili kufikia azma ya kuiondoa nchi yetu miongoni mwa nchi maskini na kuiwezesha kuwa nchi ya uchumi wa kati na maendeleo ya viwanda.

“Utekelezaji wa malengo haya utakwenda sanjari na utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambao msingi wake ni kuchochea mabadiliko ya uchumi na maendeleo ya watu.” Alisema Kessy.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

Hon. Dr. Adelardus Lubango Kilangi

None (Ex-Officio)

Supplementary Questions / Answers (0 / 3)

Contributions (25)

Profile

Hon. Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Ileje (CCM)

Questions / Answers(0 / 24)

Supplementary Questions / Answers (0 / 52)

Profile

Hon. Prof. Adolf Faustine Mkenda

Rombo (CCM)

Profile

Hon. Amina Bakar Yussuf

Special Seats (CCM)

Profile

View All MP's