Parliament of Tanzania

UTARATIBU WA UENDESHAJI WA VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE KWA KIPINDI CHA TAREHE 18 – 29 AGOSTI, 2021

Kufuatia uwepo wa Ugonjwa wa Corona hapa nchini, Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekuwa ikitoa elimu na miongozo mbalimbali ya kujikinga na maambukizi pamoja na hatua za kuchukua ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa huo. Miongoni mwa hatua inayosisitizwa ni kuepusha mikusanyiko ya watu.

Kamati 14 za Kudumu za Bunge zinakutana tarehe 16 – 29 Agosti, 2021. Vikao hivi vya Kamati vinahusisha mkusanyiko wa Waheshimiwa Wabunge, Watumishi wa Bunge, Watendaji wa Serikali, Waandishi wa Habari na Wageni wengine mbalimbali.

Katika kutekeleza kwa vitendo tahadhari za kiafya zinazotolewa na Serikali, Uongozi wa Bunge umeweka utaratibu wa uendeshaji wa Vikao vya Kamati kama ifuatavyo:-

a. Kumbi 7 kubwa ndizo zitatumika kwa Vikao vya Kamati;

b. Kamati zitakutana kwa kupishana yaani, saa 3:00 Asubuhi – 7:30 Mchana, Kamati 7 na saa 8:00 Mchana hadi saa 12:30 Jioni, Kamati 7 zilizosalia;

c. Kila Kamati itafanya vikao kwa namna inayozingatia muda uliopangwa ili kutoathiri muda wa kuanza kwa vikao vya Kamati nyingine; na

d. Idadi ya Watendaji wanaokuja na Waziri kwenye vikao vya Kamati isizidi Maafisa 5 wa Wizara kwa kikao.

Aidha, Wageni watakaoruhusiwa Bungeni kwa kipindi hiki ni Wageni wanaofika Ofisini kwa shughuli za kiofisi, Waandishi wa Habari waliosajiliwa kwa ajili ya kutoa habari za Kibunge pamoja na Wadau watakaohudhuria Vikao vya Kamati kwa ajili ya kutoa maoni ambao wataelekezwa na Kamati inayohusika kabla ya Kikao cha kupokea maoni.

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

Hon. Asya Sharif Omar

Special Seats (CCM)

Contributions (1)

Profile

Hon. Mohamed Abdulrahman Mwinyi

Chambani (CCM)

Profile

View All MP's