Parliament of Tanzania

Ufafanuzi kuhusu Chanjo ya UVIKO-19 kwa Waheshimiwa Wabunge

Ofisi ya Bunge inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa za upotoshaji zinazosambaa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii zinazodai kuwa Waheshimiwa Wabunge ambao hawatachanja chanjo ya UVIKO-19 hawataruhusiwa kuingia Bungeni.

Tunapenda kuujulisha umma kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote kwani maelekezo yaliyopo na ambayo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Y. Ndugai (Mb) amekuwa akisisitiza ni kuwahimiza Waheshimiwa Wabunge kujitokeza kuchanja chanjo hiyo kwa hiari yao.

Aidha, Ofisi ya Bunge imeandaa utaratibu utakaowawezesha Waheshimiwa Wabunge wote kupata chanjo hiyo katika viwanja vya Bunge kwa hiari yao wenyewe.

Hivyo, Waheshimiwa Wabunge wanasisitizwa kutumia hiari hiyo kujitokeza ili kupata chanjo kwa ajili ya kujikinga wao wenyewe na kuwakinga wengine.

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

View All MP's