Parliament of Tanzania

TANZIA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mhe. Irene Alex Ndyamkama Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa (CCM) kilichotokea leo tarehe 24 Aprili, 2022 katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha alipokuwa akipatiwa matibabu.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Irene Alex Ndyamkama. Natoa pole kwa familia ya Marehemu, ndugu, jamaa, Waheshimiwa Wabunge na Wananchi wa Mkoa wa Rukwa. Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Mheshimiwa Spika.

Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi, Amina.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

View All MP's