Parliament of Tanzania

TANZIA

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Y. Ndugai (Mb), anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Ushetu (CCM) na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Elias John Kwandikwa, kilichotokea tarehe 02 Agosti, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Elias John Kwandikwa (Mb). Natoa pole kwa Serikali, Waheshimiwa Wabunge, familia na wananchi wa Jimbo la Ushetu. Mwenyezi Mungu awape Moyo wa ustahimilivu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.” amesema Mhe. Spika.

Taarifa zaidi zitatolewa baada ya Ofisi kupata utaratibu na ratiba ya mazishi kutoka Serikalini.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

View All MP's