United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT.
MWIGULU L. NCHEMBA (MB), AKIWASILISHA BUNGENI TAARIFA
YA HALI YA UCHUMI WA TAIFA KWA MWAKA 2020 NA MPANGO
WA MAENDELEO WA TAIFA WA MWAKA 2021/22
DODOMA JUNI, 20211
UTANGULIZI
1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu lipokee
na kujadili Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa
Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22. Pamoja na hotuba hii, nawasilisha vitabu
vya Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa
Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22. Taarifa hizo ndiyo msingi wa bajeti ya
Serikali kwa mwaka 2021/22 nitakayowasilisha katika Bunge hili Tukufu leo alasiri.
2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote, napenda nitumie fursa hii kumshukuru
Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima na afya njema, na kutuwezesha kukutana
kwa mara nyingine katika Bunge hili baada ya majadiliano ya bajeti za mafungu
mbalimbali. Mkutano huu wa Tatu wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ni muhimu katika kujadili namna ya kuharakisha maendeleo ya nchi yetu.
3. Mheshimiwa Spika, kwa mara nyingine tena, nitumie fursa hii kutoa pole
kwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, kwako wewe Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge wote, Chama
cha Mapinduzi na Watanzania wote kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Mwenyezi
Mungu ampumzishe mahali pema peponi, Amina. Aidha, nitoe pole kwa Taifa kwa
kuondokewa na Viongozi Wakuu, Hayati Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Balozi
Mhandisi John Kijazi, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Mwenyezi Mungu azilaze
roho zao mahali pema peponi. Amina.
4. Mheshimiwa Spika, kwa moyo wa dhati, napenda kutoa pongezi kwa
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Sita
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tangu kuapishwa kwake tumeshuhudia
namna anavyoendelea kuliongoza Taifa letu kwa busara, hekima, weledi na umahiri
mkubwa na kuendeleza mashirikiano na nchi mbalimbali. Aidha, niungane na
Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wenzangu kumwombea kwa Mwenyezi
Mungu aendelee kumpa nguvu, ujasiri na afya njema ili aweze kuendelea
kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi wake kikamilifu.
5. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee, nitumie fursa hii kumpongeza
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania. Aidha, nampongeza Mhe. Othman Masoud Othman
Sharif kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar. Vilevile, natoa pongezi kwa Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), 2
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuaminiwa na Mhe. Rais
kuendelea kuwatumikia watanzania katika wadhifa wake wa Waziri Mkuu.
6. Mheshimiwa Spika, kipekee natoa shukrani zangu za dhati kwa
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa kuniamini na kuniteua kuwa Waziri wa Fedha na Mipango. Napenda
kumhakikishia Mheshimiwa Rais na Watanzania wote kuwa nitatekeleza jukumu
hili kwa bidii, weledi, uadilifu na uzalendo wa kiwango cha hali ya juu.
7. Mheshimiwa Spika, kama unavyofahamu, nchi yetu na dunia kwa ujumla
inakabiliwa na athari za UVIKO-19. Athari hizo zimesababisha kushuka kwa
shughuli za kiuchumi duniani, ikiwemo uzalishaji, biashara, sanaa na burudani,
utalii na usafirishaji wa bidhaa. Katika kukabaliana na athari hizo, Serikali
imeendelea kuchukua hatua mbalimbali, ikiwemo kufuatilia kwa ukaribu
mwenendo wa biashara duniani ili kutumia fursa zitokanazo na athari za UVIKO-19
kwa manufaa mapana ya Taifa na kuendelea kutoa elimu ya jinsi ya kujikinga na
maambukizi kwa kuzingatia miongozo ya kimataifa na ushauri unaotolewa na
wataalamu wa afya.
8. Mheshimiwa Spika, Taarifa za Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 zimezingatia dhana ya
ushirikishwaji mpana wa wadau katika hatua za uandaaji na maamuzi katika ngazi
zote serikalini. Ni vigumu kuwataja wadau wote waliotoa maoni na ushauri hadi
kufikia hapa, lakini ni vyema nitambue mchango mkubwa wa Bunge lako Tukufu
chini ya uongozi wako Mheshimiwa Spika pamoja na Naibu Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, napenda kumshukuru Mheshimiwa
Sillo Daniel Baran (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na
wajumbe wote wa Kamati kwa ushauri makini waliotupatia. Uandaaji wa taarifa
nilizowasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu umenufaika kwa kiasi kikubwa na
mchango, ushauri na busara za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.
9. Mheshimiwa Spika, Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020
imeandaliwa kwa kuzingatia mwenendo wa viashiria vya uchumi jumla na sekta
mbalimbali kwa mwaka husika, ikilinganishwa na mwaka 2019. Aidha, maandalizi
ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 yamezingatia vipaumbele
vya Serikali vilivyoainishwa katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa
Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, Ilani ya CCM kwa Ajili ya Uchaguzi Mkuu wa
Mwaka 2020 na Hotuba ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wakati akilihutubia rasmi Bunge hili la 12 la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania tarehe 22 Aprili, 2021. Aidha, Mpango umezingatia Sera na 3
Mikakati mbalimbali ya kisekta, kikanda na kimataifa zikiwemo Dira ya Maendeleo
ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) 2050; Dira ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini
mwa Afrika (SADC) 2050; Ajenda 2063 ya Maendeleo ya Afrika; na Malengo ya
Maendeleo Endelevu 2030. Vilevile, Mpango huu umeandaliwa kwa kuzingatia
misingi ya mipango ya awali iliyolenga kuimarisha na kukuza uchumi
fungamanishi, jumuishi na shindani unaohimili utandawazi. Katika kutekeleza
Mpango wa mwaka 2021/22, msukumo mkubwa utawekwa katika kuliwezesha
Taifa letu kutumia kikamilifu fursa zilizopo ili kujenga uchumi shindani na viwanda
kwa maendeleo ya watu.
MWENENDO WA HALI YA UCHUMI KWA MWAKA 2020
Uchumi wa Dunia
10. Mheshimiwa Spika, taarifa ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ya Aprili
2021 inaonesha kuwa, mwaka 2020, dunia ilikuwa na mdororo wa uchumi kwa
kupata ukuaji hasi wa asilimia 3.3 ikilinganishwa na ukuaji chanya wa asilimia 2.8
mwaka 2019. Ukuaji hasi ulisababishwa na kupungua kwa shughuli za kiuchumi
duniani hususan, biashara, usafirishaji na utalii kutokana na mlipuko wa UVIKO-19.
Hata hivyo, uchumi wa dunia unatarajiwa kuimarika na kufikia ukuaji wa asilimia
6.0 mwaka 2021 na asilimia 4.4 mwaka 2022. Hii inatokana na matarajio ya kurejea
kwa shughuli za kiuchumi kutokana na kuendelea kusambazwa kwa chanjo ya
UVIKO-19 na hatua za kuinua chumi zinazochukuliwa na nchi mbalimbali.
Uchumi wa Afrika na Kikanda
11. Mheshimiwa Spika, mwaka 2020, nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara
zilikuwa na ukuaji hasi wa uchumi wa wastani wa asilimia 1.9, ikilinganishwa na
ukuaji chanya wa wastani wa asilimia 3.2 mwaka 2019. Mdororo wa uchumi katika
baadhi ya nchi ulitokana na athari ya zuio la baadhi ya shughuli za kiuchumi na
kijamii ikiwa ni njia ya kukabiliana na mlipuko wa UVIKO-19. Aidha, zuio la baadhi
ya shughuli za kiuchumi na kijamii lilisababisha kushuka kwa mauzo ya bidhaa nje
ya kanda na kupungua kwa shughuli za utalii. Ukuaji wa uchumi katika ukanda wa
Kusini mwa Jangwa la Sahara unatarajiwa kuimarika na kufikia wastani wa asilimia
3.4 mwaka 2021 na asilimia 4.0 mwaka 2022.
12. Mheshimiwa Spika, Nchi zinazotegemea utalii kama chanzo kikubwa cha
ukuaji wa uchumi zikiwemo Carpe Verde na Mauritius na zile zinazotegemea
mafuta (Angola, Cameroon, Chad, Congo, Jamhuri ya Guinea, Gabon, Nigeria na
Sudan ya Kusini) zilipata athari kubwa kutokana na UVIKO-19 na kuchangia ukuaji
hasi wa nchi za Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa ujumla mwaka 2020, 4
nchi 32 kati ya nchi 45 za Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara zilikuwa na ukuaji
hasi wa uchumi sawa na asilimia 71.1 ya nchi zote, nchi mbili zilikuwa na ukuaji wa
asilimia sifuri (0) na nchi kumi na moja (11) ikiwemo Tanzania zilikuwa na ukuaji
chanya wa uchumi.
Uchumi wa Taifa
Pato la Taifa
13. Mheshimiwa Spika, licha ya mlipuko wa UVIKO-19 ulioathiri uchumi wa
nchi nyingi duniani, Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani zilizokuwa na
ukuaji chanya wa uchumi kwa mwaka 2020. Pato la Taifa lilikua kwa asilimia 4.8
ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 7.0 mwaka 2019. Ukuaji chanya ulitokana na
hatua ya Serikali ya kuruhusu shughuli za kiuchumi na kijamii kuendelea na wakati
huohuo wananchi wakisisitizwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu
wa afya. Aidha, kupungua kwa kasi ya ukuaji wa uchumi nchini kulichangiwa na
athari za UVIKO-19 katika nchi washirika wa kibiashara pamoja na mafuriko
yaliyosababisha uharibifu wa miundombinu ya usafirishaji na kuchelewesha
utekelezaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo.
14. Mheshimiwa Spika, athari za janga la UVIKO-19 zilijitokeza zaidi katika
shughuli za kiuchumi za malazi, huduma ya chakula pamoja na sanaa na burudani
ambazo zilikuwa na ukuaji hasi kwa mwaka 2020. Sekta zilizokua kwa viwango vya
juu kwa mwaka 2020 ni pamoja na: Sekta ya Ujenzi (asilimia 9.1); Habari na
Mawasiliano (asilimia 8.4); Uchukuzi na Uhifadhi wa Mizigo (asilimia 8.4); Huduma
zinazohusiana na Utawala (asilimia 7.8); Shughuli za Kitaalamu, Sayansi na Ufundi
(asilimia 7.3); Madini na Mawe (asilimia 6.7); na Afya na Huduma za Jamii (asilimia
6.5).
15. Mheshimiwa Spika, Pato ghafi la Taifa lililozalishwa nchini lilikuwa shilingi
trilioni 148.5 mwaka 2020, ikilinganishwa na shilingi trilioni 139.6 mwaka 2019.
Aidha, mwaka 2020, Tanzania Bara ilikadiriwa kuwa na watu milioni 55.9,
ikilinganishwa na watu milioni 54.2 mwaka 2019. Hivyo, Wastani wa Pato kwa Mtu
lilikadiriwa kufikia shilingi 2,653,790, sawa na dola za Marekani 1,151.0 mwaka 2020
ikilinganishwa na shilingi 2,573,324, sawa na dola za Marekani 1,118.9 mwaka 2019,
ikiwa ni ongezeko la asilimia 3.1.
Mwenendo wa Bei
16. Mheshimiwa Spika, mfumuko wa bei umeendelea kubaki katika wigo wa
tarakimu moja ambapo ulipungua kutoka wastani wa asilimia 3.4 mwaka 2019 hadi 5
asilimia 3.3 mwaka 2020. Aidha, mfumuko wa bei umebaki katika wigo wa asilimia
3.3 Mei 2021. Mwenendo wa mfumuko wa bei umeendelea kuwa tulivu kutokana na
upatikanaji wa chakula cha kutosha, kushuka kwa bei ya mafuta kwenye soko la
dunia, utulivu wa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani na
sarafu nyingine duniani na usimamizi madhubuti wa sera za fedha na bajeti.
Utekelezaji wa Sera ya Fedha 2020/21
17. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2020/21, malengo ya sera ya fedha
yalikuwa ni kama ifuatavyo:
(i) Ukuaji wa wastani wa fedha taslimu usiozidi asilimia 9.0;
(ii) Ukuaji wa ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi (M3) usiozidi asilimia 10.0;
(iii) Ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi usiozidi asilimia 13.5; na
(iv) Kuwa na akiba ya fedha za kigeni inayotosheleza uagizaji wa bidhaa na
huduma kutoka nje ya nchi kwa kipindi kisichopungua miezi 4.0.
18. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Benki Kuu imeendelea kusimamia
utekelezaji wa sera ya fedha ya kuongeza ukwasi kwenye uchumi ambayo imesaidia
kupunguza baadhi ya viwango vya riba katika masoko ya fedha hususan riba za
mikopo. Wastani wa riba za mikopo ya benki kwa ujumla katika kipindi cha mwaka
unaoishia Aprili 2021 ulipungua hadi asilimia 16.58, ikilinganishwa na wastani wa
asilimia 16.91 katika kipindi kama hicho mwaka 2020, na riba za mikopo ya kipindi
cha mwaka mmoja zilipungua na kufikia wastani wa asilimia 16.05 kutoka asilimia
16.37. Aidha, wastani wa riba za amana kwa ujumla ulikuwa asilimia 6.95 katika
kipindi cha mwaka unaoishia Aprili 2021, ikilinganishwa na wastani wa asilimia
6.69 katika kipindi kama hicho mwaka 2020. Riba za amana za kipindi cha mwaka
mmoja ziliongezeka na kufikia wastani wa asilimia 8.77 katika kipindi cha mwaka
unaoishia Aprili 2021 ikilinganishwa na asilimia 8.01 katika kipindi kama hicho
mwaka 2020.
Ujazi wa Fedha na Karadha
19. Mheshimiwa Spika, ujazi wa fedha uliendelea kukua kwa kasi inayoendana
na mahitaji ya shughuli mbalimbali za kiuchumi. Wastani wa ukuaji wa ujazi wa
fedha kwa tafsiri pana zaidi (M3) uliongezeka na kufikia shilingi trilioni 31.0 Aprili
2021 ikilinganishwa na shilingi trilioni 28.76 Aprili 2020, sawa na ongezeko la
asilimia 7.8. Aidha, ujazi wa fedha kwa tafsiri pana (M2) uliongezeka kufikia shilingi
trilioni 23.59 Aprili 2021 ikilinganishwa na shilingi trilioni 22.03 Aprili 2020, sawa na
ongezeko la asilimia 7.1. Ongezeko hili la ujazi wa fedha ni matokeo ya usimamizi
thabiti wa sera ya fedha.6
Mwenendo wa Mikopo kwa Sekta Binafsi
20. Mheshimiwa Spika, Mikopo kwa sekta binafsi ilikua kwa wastani wa
asilimia 4.8 katika kipindi cha mwaka unaoishia Aprili 2021 ikilinganishwa na
ukuaji wa wastani wa asilimia 5.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2020. Ukuaji
mdogo wa mikopo kwa sekta binafsi ulitokana na athari za UVIKO - 19 kwenye
shughuli za kiuchumi nchini. Aidha, sehemu kubwa ya mikopo ilielekezwa katika
shughuli binafsi ambazo zilipata asilimia 35.8 ya mikopo yote, ikifuatiwa na
shughuli za biashara asilimia 15.7, uzalishaji viwandani asilimia 10.1 na kilimo
asilimia 8.0.
Ukuzaji Rasilimali
21. Mheshimiwa Spika, mwaka 2020, ukuzaji rasilimali kwa bei za miaka husika
ulifikia shilingi trilioni 59.2 kutoka shilingi trilioni 55.8 mwaka 2019, sawa na
ongezeko la asilimia 6.2. Aidha, ukuzaji rasilimali za kudumu kwa bei za miaka
husika uliongezeka kwa asilimia 7.8 kutoka shilingi trilioni 59.4 mwaka 2019 hadi
shilingi trilioni 64.0 mwaka 2020. Vilevile, thamani ya limbikizo la rasilimali kwa bei
za miaka husika ilipungua kwa shilingi trilioni 4.8 mwaka 2020 ikilinganishwa na
upungufu wa shilingi trilioni 3.7 mwaka 2019. Ukuzaji rasilimali katika sekta ya
umma uliongezeka kwa asilimia 7.8 kufikia shilingi trilioni 19.0 mwaka 2020 kwa bei
za miaka husika wakati katika sekta binafsi uliongezeka kwa asilimia 7.8 kufikia
shilingi trilioni 45.0 mwaka 2020.
Sekta ya Nje
22. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka unaoishia Aprili 2021, urari
wa biashara ya bidhaa, huduma na uhamisho mali nchi za nje uliimarika kufikia
nakisi ya dola za Marekani milioni 1,177.2, ikilinganishwa na nakisi ya dola za
Marekani milioni 1,443.6 katika kipindi kama hicho mwaka 2020. Kupungua kwa
nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa kulichangiwa na kuongezeka kwa mauzo ya
dhahabu na bidhaa za maua na mbogamboga sambamba na kupungua kwa thamani
ya uagizaji wa mafuta na vyombo vya usafiri.
23. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka unaoishia Aprili 2021,
thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma ilifikia dola za Marekani bilioni 8.5 kutoka
dola za Marekani bilioni 9.6 katika kipindi kama hicho mwaka 2020. Upungufu huo
ulitokana na kupungua kwa mapato yatokanayo na shughuli za utalii, ikiwa ni
matokeo ya hatua zilizochukuliwa na mataifa mengine duniani ili kupunguza kasi 7
ya maambukizi ya UVIKO-19, hususan kuzuia safari za kimataifa. Aidha, katika
kipindi hicho, thamani ya bidhaa na huduma zilizoagizwa kutoka nje ilifikia dola za
Marekani bilioni 9.3, ikilinganishwa na dola za Marekani bilioni 10.5 katika kipindi
kama hicho mwaka 2020. Hali hiyo ilitokana na kupungua kwa thamani ya uagizaji
wa mafuta, vyombo vya usafiri na vifaa vya ujenzi.
24. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka unaoishia Aprili 2021,
thamani ya mauzo ya bidhaa iliongezeka kufikia dola za Marekani bilioni 6.35
kutoka dola za Marekani bilioni 5.67 kipindi kama hicho mwaka 2020, sawa na
ongezeko la asilimia 12.0. Ongezeko hilo lilitokana na kuongezeka kwa mauzo ya
bidhaa asilia na zisizo asilia ikiwemo dhahabu, madini mengineyo, bidhaa za maua
na mbogamboga pamoja na bidhaa za viwandani. Aidha, thamani ya bidhaa
zilizoagizwa kutoka nje ilipungua kwa asilimia 7.4 kutoka dola za Marekani bilioni
8.75 katika kipindi cha mwaka unaoishia Aprili 2020 hadi dola za Marekani bilioni
8.11 katika kipindi kama hicho mwaka 2021. Hali hiyo ilitokana na kupungua kwa
uagizaji wa baadhi ya bidhaa kufuatia kuimarika kwa uzalishaji katika viwanda vya
ndani, hususan bidhaa za ujenzi kama vile marumaru, nondo na saruji.
25. Mheshimiwa Spika, mapato yatokanayo na huduma yalipungua kutoka dola
za Marekani bilioni 3.89 katika kipindi cha mwaka unaoishia Aprili 2020, hadi dola
za Marekani bilioni 2.20 Aprili 2021. Aidha, malipo ya huduma yalipungua na
kufikia dola za Marekani bilioni 1.19 kutoka dola za Marekani bilioni 1.73 kutokana
na kupungua kwa malipo yanayohusiana na usafiri wa nje.
Akiba ya Fedha za Kigeni
26. Mheshimiwa Spika, akiba ya fedha za kigeni imeendelea kuwa ya
kuridhisha kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi.
Hadi Aprili 2021, akiba ya fedha za kigeni ilikuwa dola za Marekani bilioni 4.97
ambayo inatosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa kipindi
cha takribani miezi 5.8. Kiwango hicho ni zaidi ya lengo la nchi la kukidhi mahitaji
ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa muda wa miezi 4.0 na ni
zaidi ya lengo la miezi 4.5 kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mwenendo wa Thamani ya Shilingi
27. Mheshimiwa Spika, thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya
Marekani imeendelea kuwa tulivu ambapo dola moja ya Marekani ilibadilishwa
kwa wastani wa shilingi 2,298.5 Aprili 2021, ikilinganishwa na wastani wa shilingi
2,291.3 Aprili 2020. Utulivu wa shilingi umetokana na hatua mbalimbali
zilizochukuliwa na Serikali katika usimamizi wa Sera za Fedha na Bajeti, kupungua 8
kwa nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa, huduma na uhamisho wa mali nje ya
nchi pamoja na mwenendo chanya wa baadhi ya shughuli mbalimbali za kiuchumi
na kijamii. Vilevile, hatua zilizochukuliwa na Benki Kuu ya Tanzania katika
kusimamia misingi ya uwazi katika ununuzi na uuzaji wa fedha za kigeni nchini
zimechangia thamani ya shilingi dhidi ya sarafu nyingine kubwa duniani kuwa
tulivu.
Deni la Serikali
28. Mheshimiwa Spika, hadi Aprili 2021, deni la Serikali lilikuwa shilingi trilioni
60.9, ikilinganishwa na shilingi trilioni 55.5 kipindi kama hicho mwaka 2020. Kati ya
kiasi hicho, deni la nje ni shilingi trilioni 43.7 na deni la ndani ni shilingi trilioni 17.3.
Ongezeko hilo lilitokana na kupokelewa kwa fedha za mikopo mipya kwa ajili ya
kugharamia miradi ya maendeleo. Taarifa ya tathmini ya uhimilivu wa deni
iliyofanyika Desemba 2020 inaonesha kuwa deni la Serikali ni himilivu katika
kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu kwa kuzingatia ukomo wa viashiria
vyote vinavyokubalika kimataifa.
MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA
KWA KIPINDI CHA 2016/17 – 2020/21
29. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2016/17 hadi 2020/21,
Serikali ilikuwa inatekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka
Mitano 2016/17 – 2020/21 kupitia Mipango ya Maendeleo ya mwaka mmoja mmoja.
Dhima kuu ya Mpango wa Pili ilikuwa ni “Ujenzi wa Viwanda kwa Maendeleo ya
Watu”. Serikali ilijenga miundombinu ya msingi ili kuwezesha wananchi kujiletea
maendeleo na kuchochea uwekezaji katika viwanda. Katika kipindi hicho, mafanikio
mbalimbali yalipatikana hususan kuimarika kwa ustawi wa uchumi na maisha ya
watu. Mafanikio hayo yanajumuisha:
(i) Miundombinu ya Reli: Kufikia asilimia 91 ya ujenzi wa Reli ya Kati ya
Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway - SGR) kipande cha Dar es
Salaam – Morogoro (km 300) na asilimia 61 kwa kipande cha Morogoro –
Makutupora (km 422); na kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa kipande cha
Mwanza - Isaka (km 341) wenye thamani ya shilingi trilioni 3.07. Mafanikio
mengine ni: kukamilika kwa ukarabati wa miundombinu ya reli ya kati
kutoka Dar es Salaam - Isaka (km 970); kukamilika kwa ukarabati na kuanza
kutoa huduma za reli ya Tanga hadi Arusha (km 439); na kukarabatiwa kwa
mabehewa 347 ya mizigo.
(ii) Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere – MW 2,115: Kukamilika 9
kwa ujenzi wa njia ya kuchepusha maji (Diversion Tunnel); kuendelea na
ujenzi wa bwawa (main dam and spillways), ujenzi wa njia kuu za kupitisha
maji (tunnels), ujenzi wa kituo cha kuzalishia umeme (Power House) na
ujenzi wa kituo cha kusafirisha umeme (Switch yard) ambapo utekelezaji wa
mradi umefikia asilimia 52.
(iii) Uboreshaji wa Shirika la Ndege Tanzania: Kununuliwa kwa ndege mpya 11
ambazo zinasafirisha abiria na mizigo ndani na nje ya nchi; kuboreshwa kwa
karakana ya ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro;
ununuzi wa jozi ya injini za akiba kwa ndege aina ya Dash 8 Q400; na kulipa
bima za ndege Boeing 787-8 Dreamliner na Dash 8 Q400.
(iv) Miradi ya Umeme: Kukamilika kwa mradi wa njia ya kusafirisha umeme kV
220 kutoka Makambako hadi Songea; kukamilika kwa ujenzi na upanuzi wa
vituo vya kupoza umeme pamoja na njia za kusafirisha umeme katika Mradi
wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 220 Bulyanhulu – Geita;
kuendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa kV 400 Singida –
Arusha – Namanga ambapo utekelezaji umefikia asilimia 91.6; kukamilika
kwa asilimia 80 ya utekelezaji wa mradi wa Kufua Umeme wa Rusumo -
MW 80; kuendelea na utekelezaji wa mradi wa Kinyerezi I Extension MW
185 ambapo utekelezaji umefikia asilimia 84; kukamilika kwa usanifu wa
miradi ya Kakono MW 87 na Malagarasi MW 45; kuendelea na kuhuisha
upembuzi yakinifu na usanifu wa miradi ya Kufua Umeme wa Maji ya
Ruhudji MW 358 na Rumakali MW 222; kukamilika kwa upembuzi yakinifu
na uthamini wa mali za wananchi watakaopisha mradi wa Njia ya
Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 400 Rufiji – Chalinze – Dodoma na
Chalinze – Kinyerezi; na kuunganishwa umeme kwa jumla ya vijiji 10,312
kati ya vijiji 12,317, sawa na asilimia 83.7 ya vijiji vyote nchini.
(v) Ujenzi na Ukarabati wa Viwanja vya Ndege: Kuendelea na ujenzi wa
viwanja vya ndege vya Geita (asilimia 95), Songea (asilimia 95) na Mtwara
(asilimia 55); kukamilika kwa maandalizi ya mradi wa ujenzi wa kiwanja cha
ndege cha kimataifa cha Msalato ambao utagharimu dola za Marekani milioni
330, sawa na shilingi bilioni 759; uzinduzi wa ujenzi na upanuzi wa viwanja
vya ndege vya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Sumbawanga
vitakavyogharimu Euro milioni 50 sawa na shilingi bilioni 136.85; kukamilika
kwa upanuzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege katika kiwanja cha
ndege cha Dodoma; na kufungwa kwa mifumo ya kuongoza ndege katika
viwanja vya ndege vya Dodoma, Tabora na Mwanza.
(vi) Uendelezaji wa Bandari: Bandari ya Dar es Salaam: Kuboreshwa kwa gati 10
namba 1 – 5; kukamilika kwa ujenzi wa gati la kupakia na kushushia magari
(RoRo); na kuendelea na uboreshaji wa gati namba 6 na 7. Bandari ya
Mtwara: kukamilika kwa ujenzi wa gati jipya lenye urefu wa mita 300 na yadi
ya kuhudumia makasha. Bandari ya Tanga: kukamilika kwa uongezaji wa
kina cha lango la kuingia meli kutoka mita nne (4) hadi mita 13, kuweka vifaa
vya kuongozea meli pamoja na ujenzi wa magati mawili (2) kwenye kina
kirefu.
Bandari za Maziwa Makuu: Kukamilika kwa ujenzi wa magati ya
Nyamirembe, Magarine, Lushamba, Ntama na Mwigobero katika Ziwa
Victoria; kukamilika kwa ujenzi wa magati ya Sibwesa na Kabwe pamoja na
kuendelea na ujenzi wa Bandari za Karema, Ujiji, Kibirizi na Lagosa katika
Ziwa Tanganyika; na kukamilika kwa ujenzi wa sakafu ngumu katika
bandari ya Kiwira na Itungi katika Ziwa Nyasa.
(vii) Kuboresha Huduma za Usafiri na Usafirishaji wa Abiria na Mizigo katika
Maziwa Makuu
Ziwa Victoria na Tanganyika: Kukamilika kwa ukarabati wa meli mbili (2) za
New Butiama Hapa Kazi Tu na New Victoria Hapa Kazi Tu; kuendelea na
ujenzi wa meli mpya ya MV Mwanza Hapa kazi Tu yenye uwezo wa kubeba
abiria 1,200 na tani 400 za mizigo ambao umefikia asilimia 74; na kukamilika
kwa ujenzi wa chelezo cha kujengea na kukarabati meli katika Bandari ya
Mwanza chenye uwezo wa kubeba meli au chombo chenye uzito kuanzia tani
moja (1) hadi tani 4,000.
Ziwa Nyasa: Kukamilika kwa ujenzi wa matishari mawili (2) yenye uwezo
wa kubeba tani 1,000 kila moja; na kukamilika na kuanza kufanya kazi kwa
meli moja mpya ya MV Mbeya II yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na tani
200 za mizigo.
(viii) Barabara na Madaraja Makubwa: Serikali imeendelea kujenga na kukarabati
mtandao wa barabara nchini kwa lengo la kufungulia fursa za kiuchumi
katika maeneo mbalimbali, kuongeza wigo wa utoaji huduma za msingi na
ustawi wa maisha ya watu. Mafanikio yaliyopatikana yanajumuisha: ujenzi
wa mtandao wa barabara kwa kiwango cha lami wenye urefu wa kilomita
3,537 (barabara kuu na za mikoa kilomita 2,209 na barabara za halmashauri
kilomita 1,328) hivyo kufanya mtandao wa barabara kwa kiwango cha lami
kufikia kilomita 13,044. Baadhi ya miradi iliyotekelezwa ni: kukamilika na
kuanza kutumika kwa daraja la juu la Kijazi (Kijazi Interchange); kukamilika 11
kwa asilimia 87.38 ya upanuzi wa barabara sehemu ya Kimara – Kiluvya (km
19.2); kuendelea na ujenzi wa daraja la Kigongo – Busisi (Mwanza) lenye
urefu wa kilomita 3.2 na upana wa mita 28.5 ambapo utekelezaji umefikia
asilimia 27; kuendelea na ujenzi wa Daraja jipya la Tanzanite (Dar es Salaam)
ambao umefikia asilimia 77.19; na Daraja Jipya la Wami (Pwani) asilimia 50.
(ix) Huduma za Afya: Ujenzi wa hospitali 99 za halmashauri ambapo hospitali 67
zimeanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje; kujengwa kwa hospitali 10
za rufaa za mikoa; kukamilika kwa ujenzi wa zahanati 1,198; kukamilika kwa
ujenzi wa jengo la wodi namba 18 ya Sewa Haji pamoja na ujenzi wa wodi za
kulaza wagonjwa binafsi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili; kukamilika
kwa ujenzi wa jengo la huduma za dharura na ukarabati wa jengo la mionzi
katika Hospitali ya Rufaa Dodoma; kukamilika kwa asilimia 98.2 ya ujenzi wa
Hospitali ya Uhuru – Dodoma ambayo imeanza kutoa huduma kwa
wagonjwa wa nje; kununuliwa kwa mashine za kidigitali za mionzi na
ultrasound, vifaa vya maabara na mashine za uchunguzi wa kifua kikuu kwa
kuotesha vimelea BACTEC 960 (Mycobacteria Growth Indicator Tube - MGIT) na
Blood culture machine katika Hospitali ya Rufaa ya Magonjwa ya Kifua Kikuu –
Kibong’oto; ununuzi wa mashine ya Positron Emmission Tomography (PET
Scan) kwa ajili ya Hospitali ya Ocean Road; ujenzi wa jengo la mama na mtoto
katika Hospitali ya Rufaa Mwananyamala umefikia asilimia 98; ujenzi wa
jengo la maabara katika Hospitali ya Rufaa Njombe umefikia asilimia 73;
kukamilika kwa ujenzi wa jengo la ghorofa moja la huduma za upasuaji,
radiolojia na maabara na kufikia asilimia 51 ya ujenzi wa jengo la mama na
mtoto katika Hospitali ya Rufaa Simiyu; kufikia asilimia 98 ya awamu ya
kwanza ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Burigi (Chato); na ununuzi
wa dawa, chanjo, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi ambapo upatikanaji wa aina
30 za dawa zenye kukidhi magonjwa ya msingi (30 tracer medicines) ulifikia
asilimia 86 na upatikanaji wa aina 312 za dawa muhimu umefikia asilimia 74.
(x) Elimu: Kuendelea kutekeleza Sera ya Serikali ya kuongeza fursa za elimu
bora kwa kila mtoto nchini kwa kugharamia elimumsingi bila ada ambapo
wastani wa shilingi bilioni 20.8 zinatolewa kila mwezi; kujengwa kwa
miundombinu muhimu katika shule 3,904 (Msingi 3,021 na Sekondari 883),
mabweni 547, nyumba 101 za walimu, majengo ya utawala 25 na maktaba 43;
kukamilika kwa ujenzi wa maboma 2,815 katika shule za msingi 2,133;
kukarabatiwa kwa shule kongwe 84 kati ya 89; kuongezeka kwa wigo wa
utoaji wa mikopo ya elimu ya juu; kuanzishwa kwa vituo vya umahiri vya
mafunzo katika taasisi za elimu ya ufundi; kuimarishwa kwa Chuo cha Taifa
cha Usafirishaji katika taaluma za anga na Chuo cha Ufundi Arusha katika 12
taaluma ya nishati; na kuendelea kugharamia chakula na malazi kwa
wanachuo wote katika vyuo 35 vya mafunzo ya ualimu vya Serikali.
(xi) Maji Mijini na Vijijini: Kukamilika kwa miradi 1,845 ya maji mijini na vijijini
hivyo kuwezesha huduma za maji kufikia asilimia 85 kwa wananchi waishio
mijini na asilimia 72.3 vijijini hadi Machi 2021. Baadhi ya miradi
iliyotekelezwa na hatua zilizofikiwa ni: kukamilika kwa miradi ya maji katika
miji ya Geita, Njombe na Songwe na kuendelea kwa ujenzi wa mradi wa maji
katika mji wa Kigoma (asilimia 90), Mwanza (asilimia 76) na Arusha (asilimia
62); na kukamilika na kuzinduliwa kwa Mradi mkubwa wa Maji wa Ziwa
Victoria kwenda katika miji ya Isaka, Tinde, Kagongwa, Tabora, Igunga, Uyui
na Nzega. Aidha, katika eneo linalohudumiwa na DAWASA (mikoa ya Dar
es Salaam na Pwani) utekelezaji wa miradi umekamilika kwa zaidi ya asilimia
90.
(xii) Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Kilimo: Kujengwa na kuboreshwa kwa miundombinu ya umwagiliaji hivyo
kuongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji kutoka hekta 461,376 mwaka 2015
hadi hekta 694,715 mwaka 2020; kukamilika kwa ujenzi na ukarabati wa
skimu 17 za umwagiliaji zenye ukubwa wa hekta 8,536 kupitia ASDP II na
skimu tano (5) za Kigugu – Mvomero (hekta 195), Msolwa Ujamaa (hekta 40),
Njage – Kilombero (hekta 75), Mvumi – Kilosa (hekta 249) na Kilangali Seed
Farm – Kilosa (hekta 400) kupitia mradi wa kuongeza uzalishaji wa mpunga –
Expanded Rice Production Project (ERPP); kuongezeka kwa uzalishaji wa
mbegu bora kutoka tani 36,614 mwaka 2015 hadi tani 76,726 mwaka 2020; na
kukamilika kwa ujenzi wa maabara ya mbegu katika makao makuu ya
Wakala wa Mbegu za Kilimo – Morogoro.
Mifugo: Kuimarishwa kwa Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji kilichopo Usa
River Arusha kwa kununua kifaa (Chiller) kwa ajili ya mtambo wa kuzalisha
kimiminika cha naitrojeni; kujengwa kwa viwanda vipya vya kimkakati vya
nyama vya Tanchoice (Pwani), Elia Food Oversees Limited (Arusha) na Binjiang
Company Limited (Shinyanga); kujengwa kwa kiwanda cha maziwa cha Galaxy
Food and Beverage Company Limited (Arusha); kujengwa kwa kiwanda cha
kuzalisha chanjo cha Hester Bioscience Africa Limited (Pwani) chenye uwezo wa
kuzalisha chanjo aina 37; kuendelea kuboresha huduma za malisho ya mifugo
na majosho; na kuendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa machinjio ya kisasa
Vingunguti.
Uvuvi: Kuongezeka kwa uvunaji wa samaki katika maji ya asili kutoka tani 13
362,645 zenye thamani ya shilingi trilioni 1.48 mwaka 2015/16 hadi tani
497,567 za samaki zenye thamani ya shilingi trilioni 2.34 mwaka 2019/20;
kuongezeka kwa usindikaji wa minofu ya samaki aina ya Sangara kutoka tani
23,000.6 mwaka 2015/16 hadi tani 27,596.3 mwaka 2019/20; kuongezeka kwa
huduma za usafirishaji wa mazao ya uvuvi kwenda masoko ya Ulaya
ambapo katika mwaka 2019/20, jumla ya tani 777.8 za mabondo
zilisafirishwa; kuongezeka kwa mauzo ya samaki na mazao ya uvuvi nje ya
nchi kutoka mauzo yenye thamani ya shilingi bilioni 379.3 mwaka 2015/16
hadi shilingi bilioni 506.2 mwaka 2019/20; na kuendelea na maandalizi ya
ujenzi wa Bandari ya Uvuvi (Mbegani) na ununuzi wa meli nne (4) za uvuvi.
(xiii) Madini: Kupitia na kutunga Sheria, Sera na mikataba ya madini; kuanzishwa
kwa kampuni mpya ya Twiga Minerals Corporation inayomilikiwa kwa ubia
kati ya Tanzania (hisa asilimia 16) na Kampuni ya Barrick (hisa asilimia 84)
ambapo imetoa gawio la shilingi bilioni 100; kuanzishwa kwa kampuni ya
Tembo Nickel Corporation ambayo ni ubia kati ya Serikali ya Tanzania (hisa
asilimia 16) na kampuni ya LZ Nickel Mining Limited (hisa asilimia 84) kwa
ajili ya uchimbaji wa madini wa Nickel Kabanga; kuanzishwa kwa kiwanda
cha Mwanza Precious Metals Refinery (MPMR) kwa ajili ya kuchenjua dhahabu;
kujengwa kwa masoko 39 ya madini na vituo 50 vya kuuzia madini;
kukamilika kwa ujenzi wa vituo vinne (4) vya umahiri katika maeneo ya
Bariadi, Musoma, Bukoba na Handeni na kuendelea na ujenzi wa vituo vya
Songea, Mpanda na Chunya; kuimarishwa kwa ulinzi wa rasilimali za madini
kwa kujenga ukuta wenye mzingo wa kilomita 24 wa Mirerani Manyara
pamoja na kujenga one stop centre, kufunga vifaa vya ulinzi ikiwa ni pamoja
na taa na CCTV Camera kuzunguka ukuta na barabara ya kuzunguka ukuta
wa ndani; na kukamilisha ujenzi wa vituo vitatu (3) vya mfano vya uchenjuaji
wa madini ya dhahabu kwa ajili ya wachimbaji wadogo katika maeneo ya
Lwamgasa (Geita), Katente (Bukombe) na Itumbi (Chunya).
30. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi hicho
umewezesha kuimarika kwa uchumi jumla, hivyo kuiwezesha Tanzania kuingia
katika kundi la nchi za hadhi ya kipato cha kati cha chini Julai 2020. Katika
kuhakikisha kuwa mafanikio ya Tanzania kuingia kipato cha kati yanakuwa
endelevu, Serikali imeweka mikakati madhubuti ya kuweza kustahimili changamoto
zozote zitakazojitokeza ikijumuisha: kuimarisha viashiria vya uchumi mpana na
kuhakikisha ukuaji endelevu wa uchumi; kuhakikikisha kuwa ukuaji wa uchumi ni
shirikishi ili kupunguza umaskini; na kujenga na kuimarisha tabaka la watu wa pato
la kati kwa kuendeleza rasilimali watu na uboreshaji wa huduma muhimu za
msingi.14
31. Mheshimiwa Spika, Mafanikio yaliyopatikana yanajenga msingi wa
kuendelea kutekeleza Mipango ya Maendeleo kwa kasi zaidi hususan kwa
kuzingatia kaulimbiu ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya “Kazi Iendelee”. Maono na miongozo yake inatoa dira
na mwelekeo mpya wa Taifa katika kutumia vema fursa mbalimbali za kikanda na
kimataifa. Natoa rai kwa watanzania wenzangu tuyaenzi mafanikio haya na
tuendelee kufanya kazi kwa bidii ili kuliletea mafanikio zaidi Taifa letu.
MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA WA MWAKA 2021/22
Malengo na Shabaha za Uchumi Jumla kwa Mwaka 2021/22
32. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2021/22, shabaha za uchumi
jumla zilizozingatiwa katika Mpango ni kama ifuatavyo:
(i) Kuongeza kasi ya ukuaji wa Pato Halisi la Taifa kufikia asilimia 5.6 mwaka
2021;
(ii) Kuendelea kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kuhakikisha kuwa unabaki
kwenye wigo wa tarakimu moja ya wastani wa asilimia kati ya 3.0 hadi 5.0
katika muda wa kati;
(iii) Mapato ya ndani (ikijumuisha mapato ya Halmashauri) kufikia asilimia 15.9
ya Pato la Taifa mwaka 2021/22 na wastani wa asilimia 16.3 ya Pato la Taifa
ifikapo mwaka 2023/24;
(iv) Mapato ya kodi kufikia asilimia 13.5 ya Pato la Taifa mwaka 2021/22 kutoka
matarajio ya asilimia 12.9 mwaka 2020/21;
(v) Kuhakikisha kuwa nakisi ya bajeti (ikijumuisha misaada) haizidi asilimia 3.0
ya Pato la Taifa ili kuendana na makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki; na
(vi) Kuwa na akiba ya fedha za kigeni kwa kiwango cha kukidhi mahitaji ya
uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa kipindi kisichopungua miezi
minne (4).
Miradi ya Kipaumbele kwa Mwaka 2021/22
33. Mheshimiwa Spika, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 ni
wa kwanza katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa
Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 wenye dhima ya “Kujenga Uchumi Shindani na
Viwanda kwa Maendeleo ya Watu”. Mpango huu utatekeleza miradi na programu
ambazo utekelezaji wake haukukamilika katika kipindi cha utekelezaji wa Mpango
wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21. Hivyo, miradi
ya kipaumbele kwa mwaka 2021/22 inaakisi maeneo matano (5) ya kipaumbele ya15
Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26.
Aidha, maeneo ya kipaumbele ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo ni: kuchochea
uchumi shindani na shirikishi; kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji
huduma; kukuza uwekezaji na biashara; kuchochea maendeleo ya watu; na
kuendeleza rasilimali watu.
34. Mheshimiwa Spika, miradi ya kipaumbele inayotarajiwa kutekelezwa katika
mwaka 2021/22 ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa
Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26. Miradi hiyo inajumuisha miradi ya
kielelezo ambayo ni: Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa (Standard
Gauge Railway) kwa kuendelea na ujenzi wa kipande cha Morogoro - Makutupora
(km 422) na kipande cha Mwanza - Isaka (km 341); Mradi wa Kufua Umeme wa Maji
wa Julius Nyerere – MW 2,115; kuboresha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL); Mradi
wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania); Mradi
wa Kusindika Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG) – Lindi; miradi ya Magadi Soda
Engaruka, Makaa ya Mawe - Mchuchuma na Chuma – Liganga; miradi ya Kufua
Umeme wa Maji ya Ruhudji (MW 358) na Rumakali (MW 222) - Njombe; ujenzi wa
madaraja makubwa na barabara za juu za Daraja la Kigongo - Busisi (Mwanza),
Tanzanite (Dar es Salaam) na Interchange ya Kamata (Dar es Salaam); Bandari ya
Uvuvi (Mbegani) na ununuzi wa meli za uvuvi; Kiwanda cha Sukari Mkulazi;
utafutaji wa mafuta na gesi katika vitalu vya Eyasi Wembere na Mnazi Bay North;
Kanda Maalumu za Kiuchumi; na kuongeza Rasilimali Watu yenye Ujuzi Adimu na
Maalumu (Ujuzi wa Kati na Wabobezi) kwa maendeleo ya viwanda na ustawi wa
jamii.
35. Mheshimiwa Spika, katika kuchochea uchumi shindani na shirikishi, msukumo
utawekwa katika miradi inayolenga kuwa na utulivu wa uchumi na uendelezaji wa
reli, barabara, madaraja, usafiri wa majini, usafiri wa anga, nishati, bandari, viwanja
vya ndege pamoja na utekelezaji wa Mpango Kazi wa kuboresha Mazingira ya
Biashara na Uwekezaji. Katika eneo hili, miradi ifuatayo itatekelezwa:
Uendelezaji wa Miundombinu
(i) Reli: Katika mwaka 2021/22, shughuli zitakazopewa kipaumbele ni pamoja
na: Ukarabati wa njia kuu ya reli katika maeneo ya Tabora - Kigoma (km 411),
Tabora – Isaka - Mwanza (km 385) na matengenezo ya njia ya reli ya Tanga - Arusha
(km 470); ukarabati wa karakana na majengo ya reli; ununuzi wa vichwa vya treni
na mabehewa na ukarabati wa mabehewa; ukarabati wa mfumo wa ishara na
mawasiliano wa reli; na uwekaji alama za mipaka katika maeneo ya reli.
(ii) Barabara na madaraja: Kipaumbele kitawekwa katika barabara za lami 16
zinazofungua fursa za kiuchumi ambazo ni: barabara za Kidatu – Ifakara – Lupilo -
Malinyi – Londo – Lumecha/Songea (km 499); Lukuyufusi – Mkenda (km 122.5);
Ifakara - Kihansi - Mlimba - Madeke – Kibena (km 220); Tabora - Ipole - Koga -
Mpanda (km 365.36); barabara ya Makutano – Natta – Mugumu/Loliondo – Mto wa
Mbu (km 235); Manyoni - Itigi – Tabora (km 259.75); Handeni– Kiberashi – Kijungu –
Kibaya – Njoro – Olboloti – Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambalo – Chemba – Kwa
Mtoro – Singida (Km 460); Dodoma – Mtera - Iringa (km 273.3); Dodoma – Babati
(km 243.8); Mbeya – Chunya – Makongolosi – Rungwa – Itigi – Mkiwa (km 528);
Kigoma – Kidahwe – Uvinza – Kaliua – Tabora (km 389.7); Barabara ya Mtwara –
Newala - Masasi (km 210); Barabara ya Masasi – Songea – Mbamba Bay (km 343.2);
Barabara ya Nzega – Tabora (km 289.7); Barabara ya Msimba – Ruaha
Mbuyuni/Ikokoto Mafinga (km 234.8); Igawa – Songwe –Tunduma na Mchepuo wa
Mbeya (km 273.5); na Makambako – Songea na Mchepuo wa Songea (km 295).
36. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea na ujenzi na ukarabati wa barabara
zinazounganisha Tanzania na nchi jirani zikiwemo: barabara ya Sumbawanga -
Matai - Kasanga Port (km 117); Isaka - Lusahunga (km 242.2); Nyakahura –
Kumubuga – Murusagamba na Kumubuga – Rulenge – Kabanga Nickel –
Murugarama (km 141); Sumbawanga - Mpanda - Nyakanazi (km 432.56); Nyanguge
– Musoma na mchepuo wa Usagara (km 202.25); Nyamuswa – Bunda – Kisorya (km
107.4); Mwigumbi - Maswa - Bariadi - Lamadi (km 121); Kidahwe - Kasulu –
Kibondo - Nyakanazi (km 341.25); Tarakea – Holili (km 53); Barabara ya Mpemba –
Isongole (km 51.2); na barabara ya Geita - Bulyanhulu - Kahama (km 120).
Aidha, Serikali itaendelea na ujenzi na ukarabati wa barabara za kupunguza
msongamano za Jijini Dar es Salaam (km 138.5) pamoja na barabara za mikoa,
kuboresha miundombinu ya mabasi yaendayo haraka kwa awamu zote nne, ujenzi
wa barabara za juu (Flyover) Jijini Dar es Salaam, barabara za mzunguko katika Jiji
la Dodoma pamoja na barabara za vijijini na mijini kupitia Wakala ya Barabara za
Vijijini na Mijini (TARURA). Vilevile, Serikali itaendelea na ujenzi wa madaraja
makubwa yakiwemo madaraja ya New Wami (Pwani), Kitengule (Kagera), Kirumi
(Mara) na Mkenda (Ruvuma).
(i) Usafiri wa Majini; Serikali itaendelea kuboresha usafiri wa majini kwa
kujenga na kukarabati meli katika maziwa makuu ikijumuisha MV Mwanza Hapa
Kazi Tu, MV Liemba na MV Umoja, ujenzi wa maegesho ya vivuko na ununuzi na
ukarabati wa vivuko. Aidha, Serikali itaendelea kuboresha Bandari za Dar es
Salaam, Tanga na Mtwara pamoja na bandari za maziwa makuu zikijumuisha
Bandari ya Ziwa Victoria na Nyasa. 17
(ii) Usafiri wa Anga: Miradi itakayotekelezwa ni: Ukarabati wa jengo la Pili la
abiria (JNIA-TB II); kuboresha huduma katika viwanja vingine vya ndege na ujenzi
wa miundombinu na ununuzi wa vifaa vya kufundishia katika Chuo cha Taifa cha
Usafirishaji – NIT. Aidha, Serikali itaendelea na uboreshaji wa viwanja vya ndege
ikiwa ni pamoja na kiwanja cha kimataifa cha Songwe, Msalato, viwanja vya mikoa
pamoja na kuanza ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege vya Kigoma,
Sumbawanga, Tabora na Shinyanga.
(iii) Nishati: Serikali itaendelea na utekelezaji wa miradi ya kufua umeme ya
Kinyerezi I Extension - MW 185, Rusumo – MW 80, Malagarasi MW 45 na Kikonge –
MW 330; Mradi wa njia za kusafirisha umeme wa Msongo wa kV 400 Rufiji –
Chalinze – Dodoma na Chalinze – Kinyerezi; mradi wa kusafirisha umeme wa
Msongo wa kV 400 - North – West Grid Extension (Iringa – Mbeya – Sumbawanga –
Mpanda – Kigoma – Nyakanazi); mradi wa kusafirisha umeme wa kV 220 Geita –
Nyakanazi na mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa Msongo wa kV 400 Singida -
Arusha – Namanga. Aidha, Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya kusambaza
umeme vijijini pamoja na miradi ya gesi asilia na mafuta ikijumuisha ujenzi wa
bomba la kusafirisha mafuta safi kutoka Dar es Salaam (Tanzania) hadi Ndola
(Zambia) na usambazaji wa gesi asilia kwa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mtwara
na Lindi.
(iv) Mapinduzi ya TEHAMA: Serikali itaendelea kuimarisha Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano kwa kuendelea na upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano; ujenzi wa Mfumo wa Anuani za Makazi na Postikodi unaojumuisha
mradi wa Tanzania ya Kidigitali; na kuimarisha matumizi ya Serikali mtandao
katika utoaji huduma kwa umma.
37. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji
huduma, miradi ifuatayo itatekelezwa:
(a) Uzalishaji Viwandani: Katika eneo hili miradi itakayotekelezwa ni pamoja
na: kiwanda cha Mashine na Vipuri KMTC; kuboresha Shirika la Tanzania
Automotive Technology Centre (TATC); kiwanda cha Kuunganisha Matrekta
ya URSUS – TAMCO – Kibaha; eneo la Kongano ya Viwanda – TAMCO; na
mradi wa mashamba na viwanda vya mazao ya mafuta. Aidha, Serikali
itaendeleza Maeneo Maalumu ya Uwekezaji (SEZ/EPZ) ya Tanga, Kigoma,
Kahama, Bunda, Songwe, Manyara, Arusha na Mtwara; kuimarisha taasisi za
utafiti na maendeleo ya viwanda na kilimo zikiwemo CAMARTEC, TIRDO,
SIDO na TEMDO; na kuimarisha uzalishaji viwandani kupitia Programu ya
Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II).18
(b) Ubiasharishaji wa Mazao ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kupitia ASDP II
(i) Kilimo: Maeneo yatakayopewa msukumo ni ujenzi na ukarabati wa
miundombinu ya umwagiliaji; kuimarisha huduma za upimaji matabaka na
ubora wa udongo; kuwezesha uanzishwaji wa mashamba makubwa ili kuwa
kitovu cha teknolojia bora kwa wakulima wadogo; kuongeza matumizi ya
teknolojia na mbinu za kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi;
kuongeza matumizi ya teknolojia bora katika uzalishaji wa mazao ili
kuongeza uzalishaji na tija; na kuimarisha vituo vya utafiti wa mbegu bora,
vyuo vya mafunzo na vituo vya mafunzo ya wakulima na huduma za ugani.
Aidha, Serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa pembejeo za
kilimo ikiwemo zana za kilimo, mbegu bora za mazao, mbolea na viuatilifu;
kuimarisha miundombinu ya kuhifadhi mazao ya kilimo; uongezaji wa
thamani ya mazao ya kilimo; na kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya ndani
na nje ya nchi. Vilevile, Serikali itaendelea kuhamasisha uzalishaji wa mazao
yakiwemo mazao ya kimkakati ya mkonge, chikichi, tumbaku, pareto,
korosho, kahawa na pamba.
(ii) Mifugo: Serikali kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya
Pili (ASDP II) itaendelea kuimarisha huduma za ugani, tafiti, tiba na udhibiti
wa magonjwa ya mifugo; kuboresha huduma za uhimilishaji mifugo;
kuimarisha Kampuni ya Ranchi za Taifa; kujenga machinjio ya kisasa na
minada ya mifugo; kuboresha huduma za unyweshaji mifugo, malisho na
vyakula vya mifugo; na kuimarisha vyuo vya mafunzo ya mifugo.
(iii) Uvuvi: Miradi itakayotekelezwa inajumuisha kufufua Shirika la Uvuvi
Tanzania – TAFICO; kuimarisha na kuendeleza ulinzi wa rasilimali za uvuvi
na mazingira; kujenga na kuimarisha miundombinu ya mazao ya uvuvi;
kukarabati vituo vya ukuzaji viumbe maji; kuimarisha huduma za ugani,
Taasisi ya Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) na Taasisi ya
Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI).
(iv) Uchimbaji wa Madini, Vito vya Thamani na Gesi Asilia: Serikali itaendelea
na utekelezaji wa mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Madini
(SMMRP) kwa kuwawezesha wachimbaji wadogo na kuanzisha mradi wa
makaa ya mawe ya kupikia (coal briqquette) kupitia Shirika la Madini la Taifa
– STAMICO; na kufanya tafiti za jiolojia kwenye maeneo ya wachimbaji
wadogo na utafiti wa madini ya viwandani (gypsum, iron, graphite,
limestone, coal, radioactive, helium gas) kupitia Wakala wa Jiolojia Tanzania
– GST.19
(c) Huduma
(i) Maliasili na Utalii: Miradi itakayopewa kipaumbele ni pamoja na mradi wa
Kuendeleza Maliasili na Kukuza Utalii katika Maeneo ya Kipaumbele –
REGROW; mradi wa Kukabiliana na Ujangili na Biashara Haramu ya
Wanyamapori Tanzania; mradi wa Kujenga Uwezo wa Taasisi na Mafunzo ya
Misitu na Ufugaji Nyuki; mradi wa Panda Miti Kibiashara; mradi wa
Kuwezesha Mnyororo wa Thamani ya Mazao ya Nyuki – BEVAC; mradi wa
Uendelezaji wa Utalii wa Mikutano na Matukio – MICE; na Programu ya
Misitu na Uendelezaji wa Mnyororo wa Thamani ya Mazao ya Misitu –
FORVAC.
(ii) Huduma za Biashara: Katika kuendeleza huduma za biashara, Serikali
itaweka mkazo katika uendelezaji wa Kituo cha Biashara na Ugavi Kurasini
ikiwa ni pamoja na kuandaa mpango kabambe wa uendelezaji wa eneo hilo
pamoja na kutafuta wawekezaji mahiri.
(iii) Huduma za Fedha: Katika kuendelea kuimarisha huduma za fedha, Serikali
itaendelea na utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Maendeleo ya Sekta ya
Fedha ili kuongeza utoaji wa mikopo ikijumuisha mikopo kwa miradi ya
uhifadhi wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi; utoaji elimu ya fedha kwa
umma; na kuendelea kusimamia masoko ya mitaji. Aidha, Serikali itaendelea
kuboresha na kuimarisha uendeshaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Benki ya
Maendeleo ya Kilimo – TADB, Soko la Mitaji na Dhamana, huduma za bima,
huduma ndogo za fedha pamoja na huduma jumuishi za fedha.
(d) Usimamizi wa Mashirika ya Umma: Serikali itaimarisha usimamizi na
uendeshaji wa Mashirika ya Umma ili kuhakikisha kuwa yanazalisha na
kutoa huduma kwa tija. Lengo ni kuyawezesha kujiendesha kwa faida na
kutoa mchango stahiki (gawio) Serikalini kwa ajili ya kuimarisha utoaji wa
huduma kwa wananchi.
(e) Usimamizi wa Uchumi Jumla: Serikali itaendelea kuimarisha usimamzi wa
viashira vya uchumi jumla ikijumuisha: kudhibiti mfumuko wa bei;
utekelezaji madhubuti wa sera za fedha na bajeti ili kuchochea ukuaji wa
uchumi, kuimarisha uzalishaji na mauzo nje, kuongeza ajira, mapato ya fedha
za kigeni, kupunguza utegemezi wa kibajeti na hivyo kuimarisha ustawi wa
maisha ya watu.
38. Mheshimiwa Spika, katika kukuza uwekezaji na biashara, Serikali itatekeleza 20
miradi na programu mbalimbali zitakazoimarisha masoko ya ndani na kutumia
fursa za masoko ya kikanda na kimataifa katika kukuza biashara. Aidha, Serikali
itaendelea kutekeleza Mpango wa Kuboresha Biashara na Uwekezaji (Blueprint) ili
kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi. Miradi mahsusi itayotekelezwa ni pamoja na:
mradi wa kuboresha mfumo wa kodi; mradi wa uendelezaji wa masoko ya bidhaa;
kuendelea na udhibiti wa ubora wa bidhaa; na kukuza Soko la Bidhaa Tanzania –
TMX kwa kujumuisha mazao ya chai, mkonge, kokoa, kahawa, mpunga, mahindi,
mbao, pamba, mazao ya mifugo na nyanya kwenye soko la bidhaa.
39. Mheshimiwa Spika, katika eneo la kuchochea maendeleo ya watu, Serikali
itaendelea kuhakikisha kuwa ukuaji wa uchumi unaakisi maisha ya watu. Aidha,
Serikali itaendelea kuboresha maisha ya watu kwa kuimarisha upatikanaji wa
huduma za jamii ikiwemo elimu na mafunzo kwa ujumla, afya na ustawi wa jamii,
kinga ya jamii, huduma za maji na usafi wa mazingira. Katika mwaka 2021/22,
Serikali itatekeleza miradi ifuatayo:
(i) Afya na Ustawi wa Jamii: Kuendelea na ujenzi na ukarabati wa hospitali za
rufaa za mikoa za Mount Meru (Arusha), Mbeya, Sekou Toure (Mwanza),
Mwananyamala (Dar es Salaam), Tumbi (Pwani), Maweni (Kigoma),
Manyara, Mawenzi (Kilimanjaro), Katavi, Njombe, Geita, Simiyu, Songwe,
Kwangwa (Mara) na Shinyanga; kuboresha miundombinu katika hospitali za
mikoa; kuimarisha upatikanaji wa damu salama kwa kununua vitendanishi
vya maabara, vifaa vya kuhifadhi damu na kugharamia uendeshaji Mpango
wa Damu Salama; kununua na kusambaza dawa, vifaa, vifaa tiba na
vitendanishi; kuendelea na mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI, Kifua
Kikuu na Ukoma na magonjwa ya kuambukiza; kuimarisha vyuo vya
mafunzo ya afya; kuimarisha tafiti za afya, huduma za tiba asili na tiba
mbadala; kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma za
afya nchini; kuendelea na ujenzi na ukarabati wa hospitali za halmashauri,
vituo vya afya na zahanati. Aidha, Serikali itaendelea na ujenzi na ukarabati
wa vyuo vya maendeleo ya jamii pamoja na kuwezesha huduma za ustawi
wa jamii.
(ii) Elimu: Kuendelea na utoaji wa elimumsingi bila ada na mikopo kwa
wanafunzi wa elimu ya juu, uboreshaji wa miundombinu ya kufundishia na
kujifunzia katika ngazi zote za elimu na ujenzi na ukarabati wa vyuo vya
ufundi stadi na vyuo vya ualimu vya Ndala, Kitangali, Shinyanga na
Mpuguso. Aidha, Serikali itaendelea na ukarabati wa vyuo vikuu vya Dar es
Salaam, Mzumbe, Sokoine (SUA), Ardhi, Ushirika Moshi, Chuo Kikuu
Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu
Mkwawa (MUCE), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili na 21
Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).
(iii) Ardhi, Mipango Miji, Nyumba na Maendeleo ya Makazi: Katika kuendelea
kupanga, kupima na kumilikisha ardhi mijini na vijijini, Serikali itaendelea
kutekeleza miradi ya uimarishaji wa mipaka kati ya Tanzania na nchi jirani,
uimarishaji wa miundombinu ya upimaji na ramani na uboreshaji wa milki za
ardhi na upangaji wa matumizi ya ardhi.
(iv) Huduma ya Maji Safi na Maji Taka: Serikali itaendelea kuboresha huduma
za maji mijini na vijijini kwa kutekeleza miradi ya maji katika miji mikuu ya
wilaya, miji midogo na miradi ya kitaifa; kujenga na kukarabati miradi ya
maji katika miji mikuu ya mikoa; kuendelea na utekelezaji wa miradi ya maji
ya Masasi – Nachingwea, Same – Mwanga – Korogwe, Ziwa Victoria –
Igunga, Nzega na Tabora, Ziwa Victoria - Kahama – Shinyanga; kuboresha
huduma za maji katika Jiji la Dar es Salaam; na kuendelea na ufuatiliaji na
uratibu wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji – WSDP II.
(v) Hifadhi ya Jamii: Shughuli zitakazotekelezwa ni pamoja na kuimarisha
Programu ya Kusaidia Kaya Maskini na kuboresha huduma za hifadhi ya
jamii kwa kuendelea na utekelezaji wa Mpango wa Maboresho ya Sekta ya
Jamii (2019/20 - 2022/23).
(vi) Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi: Serikali itaendelea kuwezesha wananchi
kiuchumi kupitia utekelezaji wa mipango na programu mbalimbali ikiwemo:
kuwezesha upatikanaji wa mikopo kwa wanawake, vijana na wenye
ulemavu; kuwezesha taaasisi za fedha zinazogharamia maendeleo ambazo ni
Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) na Benki ya Maendeleo TIB. Kupitia
uwezeshaji huu, shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile kilimo,
uzalishaji viwandani na biashara zinatarajiwa kukuzwa na kuendelezwa.
(vii) Kuongeza Mapato katika halmashauri: Serikali itaendelea kutekeleza miradi
ya kimkakati ya kuwezesha halmashauri kujitegemea kimapato ikijumuisha
miradi ya masoko ya kimkakati, stendi, maegesho ya malori, viwanda ili
kuongeza wigo wa utoaji huduma, kuimarisha ukusanyaji wa mapato na
hatimaye halmashauri kujitegemea.
40. Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza rasilimali watu, msukumo wa pekee
utawekwa katika miradi na programu ambazo zinalenga kuendeleza maarifa na
ujuzi wa rasimali watu nchini. Miradi na programu hizo ni pamoja na: ukuzaji ujuzi
wa nguvukazi na kuimarisha upatikanaji wa takwimu za soko la ajira; kukuza
ubunifu na kuwezesha uhawilishaji wa teknolojia kwa vijana na watu wenye 22
ulemavu; na kuwawezesha vijana kiuchumi kwa kuwapatia mikopo yenye masharti
nafuu.
41. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha tasnia ya habari, burudani na
michezo, Serikali itaendelea kuongeza wigo wa usikivu wa Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC); kukusanya na kusambaza habari na taarifa kwa wananchi kuhusu
mafanikio ya utekelezaji wa miradi na programu mbalimbali za maendeleo nchini;
kujenga vituo vya mazoezi na kupumzikia wananchi katika mikoa ya Dar es Salaam,
Dodoma na Geita; kuimarisha Mfuko wa Utamaduni na Sanaa nchini; na upanuzi
wa Chuo cha Michezo cha Malya.
42. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua mchango na umuhimu wa Sekta Binafsi
katika ugharamiaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Serikali itaendelea
kushirikiana na Sekta Binafsi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa utaratibu
wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi. Baadhi ya miradi itakayotekelezwa
ni: ujenzi wa viwanda vya dawa muhimu na vifaa tiba; uendeshaji wa huduma ya
usafiri wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam awamu ya kwanza; ujenzi
wa hoteli ya nyota nne na kituo changamani cha biashara katika kiwanja cha ndege
cha Kimataifa cha Julius Nyerere; kusambaza gesi asilia katika mikoa ya Dar es
Salaam, Lindi na Mtwara; na ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza simu za mkononi
chini ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Aidha, Serikali itaendelea
kuishirikisha sekta binafsi zikiwemo taasisi za fedha katika kugharamia na
kutekeleza miradi ya maendeleo.
43. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuimarisha mashirikiano ya kikanda
na kimataifa ikijumuisha kukarabati na kujenga majengo ya ofisi za balozi katika
nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Oman na Ethiopia. Aidha, Serikali
itaendelea na ujenzi wa vyumba tisa (9) vya mihadhara katika Chuo cha Diplomasia
Kurasini Dar es Salaam.
44. Mheshimiwa Spika, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22
utaendelea kuzingatia umuhimu wa kuimarisha Muungano wetu. Miradi
itakayotekelezwa kwa pamoja Tanzania bara na Visiwani ni pamoja na:
(i) Kukarabati na kujenga Ofisi na Makazi ya Makamu wa Rais Wete - Pemba na
Kilimani – Dodoma na kukamilisha ukarabati wa Ofisi na Makazi ya
Makamu wa Rais Tunguu – Zanzibar;
(ii) Kuongoa ardhi iliyoharibika na kuboresha kingo za mito katika maeneo ya
Kaskazini A (Unguja) na Kishapu (Shinyanga) katika maeneo ya mradi kwa
kutekeleza mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi kwa kupitia mifumo
ya ikolojia; na23
(iii) Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Awamu ya Tatu ya Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF III) ambapo shughuli zilizopangwa ni kutambua
na kutathmini hali za ustawi wa maisha ya kaya 886,724 za walengwa wa
Mpango na kuhawilisha ruzuku kwa kaya maskini 1,146,723 katika maeneo
186 ya utekelezaji kwa mizunguko sita (6) ya malipo Tanzania bara na
Visiwani.
45. Mheshimiwa Spika, maelezo ya kina kuhusu miradi ya kipaumbele
yanapatikana katika Kitabu cha Mpango, Sura ya Nne.
Vihatarishi vya Utekelezaji wa Mpango wa Mwaka 2021/22
46. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mpango unaweza kuathiriwa na
vihatarishi vya ndani na nje. Vihatarishi vya ndani ni pamoja na: rushwa; uharibifu
wa mazingira; ushiriki mdogo wa sekta binafsi; na kutotabirika kwa upatikanaji wa
rasilimali fedha kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa maeneo ya kipaumbele ya
Mpango. Vihatarishi vya nje ni pamoja na: mabadiliko ya tabianchi; mtikisiko wa
uchumi wa kikanda na kimataifa; majanga asilia; na mlipuko wa magonjwa
yanayoathiri dunia.
47. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na vihatarishi vya utekelezaji wa
Mpango, Serikali itachukua hatua mbalimbali ikijumuisha: Kuendelea kuchukua
hatua za kisheria kwa wanaobainika kuhusika na vitendo vya rushwa; kuendelea
kuboresha mazingira wezeshi ya biashara ili kupunguza gharama za uwekezaji;
kuimarisha maandalizi ya miradi; kuwezesha sekta binafsi kushiriki katika
utekelezaji wa miradi; kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani ikiwa ni pamoja
na urasimishaji wa sekta isiyo rasmi kwa lengo la kuongeza wigo wa kodi;
kuimarisha taasisi za ndani za kugharamia maendeleo ili kuwezesha upatikanaji wa
mitaji; na kuimarisha usimamizi na udhibiti wa mifumo ya kieletroniki ya Serikali.
Mikakati mingine ni pamoja na: Kuhamasisha uwekezaji wa ndani katika kujenga
viwanda vya kuzalisha pembejeo za kilimo, ikijumuisha kuimarisha kilimo
kinachohimili mabadiliko ya tabianchi – Climate Smart Agriculture; kuongeza ubora
wa bidhaa zinazozalishwa ndani ili kuongeza ushindani katika masoko ya nje;
kuimarisha mifumo ya utatuzi wa migogoro kwa njia ya majadiliano ili kuzuia
matukio yanayoweza kuhatarisha amani nchini; na kuendelea kuimarisha
ushirikiano wa kibiashara na maendeleo ya kiuchumi ya kikanda na kimataifa.
Ugharamiaji wa Mpango 2021/2224
48. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2021/22, shilingi bilioni 13,326.8
zinakadiriwa kutumika ili kugharamia miradi ya maendeleo. Kiasi hicho ni sawa na
asilimia 37 ya Bajeti yote ya Serikali. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 6,180.0 ni
matarajio ya mapato ya ndani, shilingi bilioni 4,190.9 ni mikopo ya ndani na nje
yenye masharti ya kibiashara na shilingi bilioni 2,955.9 ni misaada na mikopo nafuu
kutoka nje. Sehemu kubwa ya bajeti ya maendeleo itatumika kugharamia utekelezaji
wa miradi ya kielelezo. Aidha, miradi mingine ya maendeleo, itaendelea
kugharamiwa kupitia utaratibu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi
(PPP) pamoja na utaratibu wa Kampuni Maalum (Special Purpose Vehicles).
49. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato ya
kodi na yasiyo ya kodi kwa kufanya yafuatayo: kuboresha mazingira ya kufanya
biashara na uwekezaji ili kukuza biashara ndogo na za kati kwa ukuaji endelevu wa
uchumi utakaowezesha kupanuka kwa wigo wa kodi; kuimarisha mazingira ya
ulipaji kodi kwa hiari ikiwemo kuboresha na kuhimiza matumizi sahihi ya mifumo
ya TEHAMA na kutoa elimu kwa umma; kuendelea kurasimisha sekta isiyo rasmi;
kuimarisha usimamizi wa ukusanyaji wa mapato; kuimarisha usimamizi wa sheria
za kodi ili kutatua changamoto za ukwepaji kodi na kupunguza upotevu wa
mapato; na kuoanisha na kuboresha tozo na ada mbalimbali. Aidha, Serikali
itaendelea kutekeleza Mfumo wa Dirisha Moja la Kielektroniki (Tanzania Electronic
Single Window System - TeSWS) ili kurahisisha upitishaji wa mizigo katika vituo vya
mipakani pamoja na kupunguza gharama za kufanya biashara nchini; kuendelea
kusimamia Mfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato
(Government Electronic Payment Gateway - GePG); kusimamia malipo ya tozo na ada
mbalimbali ili kuhakikisha kuwa michango stahiki inawasilishwa kwa wakati
kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali. Vilevile, Serikali itaimarisha usimamizi
wa fedha kutoka kwa Washirika wa Maendeleo zinazopelekwa moja kwa moja
kwenye miradi ya maendeleo kupitia mfumo wa uratibu wa fedha zinazopelekwa
moja kwa moja kwa watekelezaji wa miradi ya maendeleo (D-fund Management
Information System) pamoja na kuimarisha maandalizi ya miradi ya maendeleo.
Ufuatiliaji, Tathmini na Utoaji wa Taarifa za Utekelezaji
50. Mheshimiwa Spika, ufuatiliaji, tathmini na utoaji taarifa ni moja ya nyenzo
muhimu inayowezesha utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo. Katika mwaka
2020/21, Wizara ya Fedha na Mipango ilifanya ufuatiliaji na tathmini ya miradi 248
katika sekta za Uchukuzi, Viwanda, Elimu, Afya, Ujenzi, Utawala Bora, Kilimo,
Mifugo, Maji na Biashara inayotekelezwa Tanzania Bara na Visiwani. Serikali
itaendelea kutumia mbinu na viashiria vilivyoainishwa katika Mkakati wa 25
Ufuatiliaji na Tathmini wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka
Mitano 2021/22 – 2025/26 ili kupima utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa
kipindi cha mwaka 2021/22 na kuchukua hatua za kutatua changamoto
zitakazobainika katika utekelezaji. Aidha, Serikali itaendelea kuzingatia miongozo
mbalimbali ya ufuatiliaji na tathmini ya Mpango ikiwemo Sheria ya Ununuzi wa
Umma, SURA 410, Sheria ya Bajeti, SURA 439 na Sheria ya Fedha za Umma, SURA
348. Vile vile, Serikali itatoa Mwongozo wa Ufuatiliaji na Tathmini kwa ajili ya
kuongoza uratibu wa ufuatiliaji na tathmini ili kupata matokeo tarajiwa.
51. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia umuhimu wa wadau, Serikali kupitia
Wizara ya Fedha na Mipango itashirikiana na Wizara, Idara Zinazojitegemea,
Wakala za Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na
Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na sekta binafsi katika kuratibu na kusimamia
ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Mpango. Aidha, Wizara ya Fedha na
Mipango itapokea na kuchambua taarifa za ufuatiliaji na tathmini kupitia Mfumo
wa Kitaifa wa Kusimamia Miradi ya Maendeleo – NPMIS. Vilevile, Wizara itaandaa
na kutoa taarifa ya mwaka ya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi ya
maendeleo.
52. Mheshimiwa Spika, Serikali inazielekeza Wizara, Idara Zinazojitegemea,
Wakala za Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na
Mamlaka za Serikali za Mitaa kutafsiri malengo na viashiria vya utekelezaji wa
Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26
katika Mipango na Bajeti za kisekta kwa mwaka 2021/22. Aidha, Wizara, Idara
Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za
Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zinaelekezwa kuandaa Mpango Kazi pamoja
na kuimarisha mifumo ya ndani ya ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo,
kufanya ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo na kuwajengea uwezo
watumishi katika tasnia ya ufuatiliaji na tathmini.
53. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Taifa ya Takwimu itaendelea kuandaa na kutoa
miongozo mbalimbali ya ukusanyaji, uchambuzi na uchakataji wa takwimu za
viashiria vinavyosaidia katika ufuatiliaji, tathmini na utoaji wa taarifa za utekelezaji
wa Mpango. Miongozo hiyo itapaswa kuzingatiwa na Wizara, Idara
Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za
Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na sekta binafsi wakati wa kuandaa taarifa za
kitakwimu za mwenendo na matokeo ya utekelezaji wa Mpango. Aidha, Wizara,
Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma zitaandaa
taarifa za ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na
programu na kuziwasilisha Wizara ya Fedha na Mipango. Vilevile, Ofisi ya Rais –26
TAMISEMI itaratibu ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa
katika ngazi za Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na
kuwasilisha taarifa za utekelezaji Wizara ya Fedha na Mipango.
MAJUMUISHO
54. Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza hapo awali, Mpango huu ni wa
kwanza katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka
Mitano 2021/22 – 2025/26 wenye dhima ya “Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda
kwa Maendeleo ya Watu”. Kama inavyofahamika, nchi yetu imefanikiwa kuingia
katika kundi la nchi za hadhi ya uchumi wa kipato cha kati kupitia utekelezaji wa
Mipango iliyotangulia. Utekelezaji wa Mpango wa Mwaka 2021/22 unalenga
kuendeleza mafanikio yaliyopatikana kwa kuimarisha utulivu wa viashiria vya
uchumi jumla na kasi ya ukuaji wa uchumi, kuimarisha uwezo wa uzalishaji
viwandani na kuongeza uwekezaji wa viwanda vinavyotumia nguvukazi na
malighafi zinazopatikana kwa wingi nchini hususan mazao ya kilimo, mifugo na
uvuvi, madini na gesi asilia, kuendeleza ujenzi wa miundombinu wezeshi na
kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.
55. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuhamasisha uwekezaji wa sekta
binafsi katika sekta mbalimbali ikijumuisha sekta ya viwanda na kuendeleza maarifa
na ujuzi wa rasilimali watu nchini hususan katika kuwajengea vijana stadi za kazi ili
waweze kujiajiri na kuongeza tija katika uzalishaji; na kuchochea maendeleo ya
watu kwa kuimarisha utoaji wa huduma za afya, elimu, maji na umeme vijijini.
HITIMISHO
56. Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Serikali ninaomba kutumia fur