Parliament of Tanzania

TAARIFA KUHUSU WABUNGE WA CHADEMA AMBAO HAWAJAHUDHURIA BUNGENI KWA MUDA WA WIKI MBILI

Ofisi ya Bunge inatoa taarifa kwamba katika siku za hivi karibuni baadhi ya Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamekuwa watoro kwa kutohudhuria vikao vya Bunge bila ruhusa ya Spika kwa muda wa wiki mbili kinyume na masharti ya Kanuni ya 146 inayosisitiza wajibu wa kila Mbunge kuhudhuria vikao vya Bunge.

Aidha, tunapenda ifahamike kwamba Wabunge hao walisusia vikao vya Bunge huku wakiwa wamelipwa posho ya kujikimu ya kuanzia tarehe 1-17 Mei, 2020. Kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 5 ya Kanuni za Bunge, Mheshimiwa Spika alitoa masharti mawili kwa Wabunge hao kama ifuatavyo: -

a) Kuwataka Wabunge hao kurejea Bungeni au kurudisha fedha walizolipwa mara moja.

b) Kwa kuwa haijulikani Wabunge hao walipo, watalazimika kuwasilisha ushahidi kwamba wamepimwa na hawana maambukizi ya Virusi vya Covid-19 kabla ya kuruhusiwa kuingia Bungeni. Wabunge hao ni hawa wafuatao:-

1. Mhe. Freeman Aikael Mbowe

2. Mhe. Ester Amos Bulaya

3. Mhe. Halima James Mdee

4. Mhe. John Wegesa Heche

5. Mhe. Joseph Osmund Mbilinyi

6. Mhe. Peter Simon Msigwa

7. Mhe. Rhoda Edward Kunchela

8. Mhe. Pascal Yohana Haonga

9. Mhe. Catherine Nyakao Ruge

10. Mhe. Devotha Mathew Minja

11. Mhe. Joyce John Mukya

12. Mhe. Aida Joseph Khenan

13. Mhe. Upendo Furaha Peneza

14. Mhe. Grace Sindato Kiwelu

15. Mhe. Joseph Leonard Haule.

Hivyo basi, kwa taarifa hii, na kwa mujibu wa Kanuni ya 144 ya Kanuni za Kudumu za Bunge inayohusu usalama katika maeneo ya Bunge, Mheshimiwa Spika ameagiza Kitengo cha Usalama cha Bunge KUTOWARUHUSU WABUNGE WALIOTAJWA HAPO JUU KUINGIA KATIKA MAENEO YA BUNGE KUANZIA LEO JUMATANO TAREHE 13 MEI, 2020 mpaka watakapotimiza masharti tajwa hapo juu.

Imetolewa na: Ofisi ya Spika,

S.L.P 941,

DODOMA.

13 Mei, 2020.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's