Parliament of Tanzania

SPIKA WA BUNGE AREJEA KUTOKA INDIA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai amerejea kutoka nchini India alikokuwa akifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Mheshimiwa Ndugai alisema kwa sasa afya yake iko imara kabisa na anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu na Madaktari waliokuwa wakimfanyia uchunguzi Nchini India.

Mhe. Ndugai pia amewashukuru watanzania wote kwa dua na sala zao katika kipindi alichokuwa India ambazo zimemuwezesha kuimarika kwa afya yake na hatimaye kurejea nchini salama.

Mbali na kutoa shukrani hizo Mheshimiwa Ndugai pia amewatakia Watanzania wote kheri na nafaka ya sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

Sambamba na hilo Mhe Ndugai amewakumbusha pia Waheshimiwa Wabunge kujiandaa na shughuli za Bunge ambazo zinatarajia kuanza hivi karibuni.

Katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere Mhe. Ndugai alilakiwa na Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt Tulia Ackson ambaye aliambatana na Viongozi wengine wa kitaifa akiwemo Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Merdad Kaleman, Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura, Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Godbless Lema na Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

Hon. Shabani Hamisi Taletale

Morogoro Kusini Mashariki (CCM)

Questions / Answers(1 / 0)

Supplementary Questions / Answers (1 / 0)

Profile

Hon. Kabula Enock Shitobela

Special Seats (CCM)

Contributions (2)

Profile

Hon. Kavejuru Eliadory Felix

Buhigwe (CCM)

Questions / Answers(1 / 0)

Profile

View All MP's