Parliament of Tanzania

SPIKA ATOA RAI KWA WABUNGE.

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amewataka wabunge kutumia mafunzo
waliyoyapata kupambana na changamoto watakazokutana nazo wakati wa
kufanya kazi za kamati.

Ndugai alitoa kauli hiyo jana wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa
wajumbe wote wa Kamati za Kudumu za Bunge yaliyoanza Januari 8 mwaka
huu.

“Ni matumaini yangu mafunzo haya yatatumika kama nyenzo muhimu katika
utendaji kazi wa siku hadi siku katika kamati zenu.

“Mafunzo haya yanaibua changamoto ambazo kamati inakumbana nazo pamoja
na kupata ufafanuzi wa masuala ya msingi kutoka katika Wizara, Idara,
Taasisi na Wakala wa Serikali ambazo watakuwa wadau katika utekelezaji
wa majukumu ya kamati,” alisema.

Akizungumzia kuhusu mafunzo ya jinsi ya kufanya tathimini kuhusu
ufuatiliaji na utekelezaji wa bajeti, Spika alisema yatawapa uelewa
wabunge wa masuala yanayohusu uchambuzi wa bajeti na mipango ya
Serikali.

“Naamini mpaka siku ya leo (jana) itakapomalizika wabunge wa Bunge la
11 tutakuwa na ujuzi wa msingi wa kuchambua masuala ya bajeti na
mipango ya Serikali,”alisema.

Alisema mipango pamoja na Bajeti ya Serikali ina uhusiano wa moja kwa
moja na wananchi katika majimbo wanakotoka wabunge.

“Mipango na bajeti ndiyo inatoa taswira ya Tanzania tunayoitarajia na
wabunge tunao mchango mkubwa katika kuandaa mipango na bajeti kwa
sababu ndiyo tunawakilisha wananchi,” alisema.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

Hon. Irene Alex Ndyamkama

Special Seats (CCM)

Profile

Hon. Zulfa Mmaka Omar

Special Seats (CCM)

Profile

Hon. Amb. Dr. Bashiru Ally Kakurwa

Nominated (CCM)

Profile

View All MP's