Parliament of Tanzania

Naibu Spika atoa wito kwa wakuu wa nchi za maziwa makuu kudumisha umoja na amani

Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb), amefungua kwa niaba ya Spika wa Bunge Mkutano wa vikao vya Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR) katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Mhe. Zungu ametoa wito kwa wakuu wa nchi za ukanda wa maziwa makuu, kudumisha umoja na amani kwa kuwa kwani njia ndio njia kuu itakayosaidia katika kuwalinda raia na pia kukuza uchumi wa ukanda huo.

Alisema migogoro katika baadhi ya nchi za ukanda wa Maziwa Makuu una athari kubwa si tu kwa nchi husika lakini pia kwa nchi jirani.

Aliongeza kuwa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia, inaamini kuwa amani ndio msingi pekee wa maendeleo.

“Wazo letu la msingi ni kwamba amani, usalama na maendeleo haviwezi kutenganishwa, watu wetu wanaweza kufanikiwa iwapo nchi itakuwa na amani,” alisema.

Alisema ustawi wa kiuchumi, kijamii na kimazingira unahitaji kiasi kikubwa cha ushirikiano na uaminifu ndani ya jamii na bila amani na usalama hakuwezi kuwa na maendeleo endelevu.

“Eneo letu hili la maziwa makuu tuna watu takribani milioni 312 na tuna GDP ya bilioni 325 ni uchumi mkubwa sana. Tukiamua kuwa na amani tutasaidia wananchi wetu, tukiamua kupigana watanufaika wanaoleta ugomvi, wengi tuliobaki tutaumia,” alisema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jukwaa hilo, Balozi Onyango Kakoba alisema ni wakati muafaka sasa kwa Viongozi wote wa kanda hiyo kufanya kazi ya kusaidia kuleta amani Mashariki mwa Congo na Sudan kwani hali hiyo inaleta athari kubwa kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Jukwaa hilo lina nchi wanachama 12 ambazo ni Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Uganda, Angola, Tanzania, DRC, Jamhuru ya Kongo, Jamhuri ya Kati, Zambia na Sudan.

Kamati za Jukwaa hilo zinazotarajiwa kufanya vikao kwa nyakati tofauti ni Kamati ya Ulinzi na Usalama na Kamati ya Demokrasia na Utawala Bora.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's